Mwanadamu yoyote yule bila kutishiwa adhabu hawezi kuishi kiungwana na binadamu wenzake. Iwe ni kijana au mzee, muungwana au mshenzi, mweupe au mweusi.
Lengo la nchi ni kutengeneza nguvu-kazi yenye maadili na uwajibikaji. Ninyi mnaotaka watoto wenu wasipewe adhabu wanavyokaidi pelekeni watoto wenu shule za GCSE, au huko Ulaya, lakini kama wakiwepo hapa Tanzania watachapwa viboko tu.
Tunachokataza ni ukatili uliodhidi juu ya watoto, tena ambao kiuhalisia hutokea mara chache mno. Tena bahati mbaya hukuzwa na vyombo vya habari na asasi za kiraia zenye mlengo wa kushoto kuliko uhalisia wenyewe ulivyo huko mashuleni.
Nimesoma shule za Kikatoliki, wanafunzi walikuwa ni watoto wa kizungu, waarabu, wahindi na weusi tulikuwa wakuhesabika. Ila tunasulubishwa kwa adhabu kali mno na mapadri wa kikatoliki hadi tukatia akili.
Halafu siyo lazima kila mtu asome...