Wito wangu kwa nyie walimu mnaodhani mna wito. Tusije laumiana baadaye

Mkuu Walimu nchi nzima tumesainishwa mikataba ya kufuta daraja F...

Serikali imetusainisha tufute F utadhani imeleta watoto waliofaulu kumbe imewavusha..

Sasa ukisema tuwaache tu si balaa...
Wakipata F watawafanya nini watawafuta kazi nchi nzima na hata ufundishaje daraja F uwezi kulikwepa kwa wanafunzi hawa . hila timiza majukumu fundisha wanaotaka kusoma watasoma tu lakini kulazimisha watoto wafate vile maadili yanataka itakua changamoto naona wazazi na wenye nchi awapo upande wa mwalimu kweli likikifika jambo utashughulikiwa kwa kebei na dharau
 
Una point kubwa , siku hizi habari za mtoto wa mwenzio ni wako ilishaisha ! Usichape mtoto wa mtu ! Muelekeze tu akikaza fuvu achana nae kikubwa asikuvunjie heshima !! Pia zama za fimbo ziko ukingoni walimu msipokua makini utapata shida ! Malezi ni kuanzia ngazi ya familia wewe kazi yako umjaze maarifa dogo ! Mengine achia wazazi !! Halafu madogo muwaonee huruma wamekaa kinyonge sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wana mishono kila sehemu ! Unaweza ukasema utamchapa bakora moja kumbe unapiga kwenye mshono !!! Sio zama zetu uko below 40 walimu wanapanga msitari kama 15 unapita kila mmoja unakula fimbo 3 za ujazo mpaka ufike wa mwisho dadeki , mkimaliza mnaenda kong'oa visiki na kupasua kuni !!!
 

Mnapenda kuyakuza! Hali halisi haiko hivyo mashuleni kama ambavyo zile video zinasambaa huko mitandaoni.

Matukio yale hutokea mara moja-moja tu(Sporadic and Isolated Incidents), lakini huwa yanatumika kukashifu waalimu wote na kupenyeza ajenda za kijinga dhidi ya taifa. Hili halikubaliki hata kidogo.

Mimi sitetei ukatili dhidi ya watoto, ila ni lazima watoto waadhibiwe ili wawe na adabu. Wazazi siku hizi wanajidai kuiga Umagharibi kwenye malezi, ilhali hawafahamu kinachoendelea nyuma ya pazia.

Ila kama nilivyosema mwanzo, hutaki mtoto wako apigwe peleka akasoma GCSE, tuachieni sisi NECTA yetu.
 
Ok sawa, mimi kama mwalimu nafuata kanuni za ufundishaji, kwa maana kwamba nafundisha wanafunzi wenye utayari wa kujifunza. Hawa wanafunzi watukutu walioshindikana kupokea ushauri nasaha siwalazimishi kufanya kazi za darasani. Ya nini kupiga wanafunzi wa hivyo? Kama darasa lina wanafunzi wengi ni watukutu na mmoja ni msikivu anayefanya kazi za darasani huyo huyo anatosha kunihalalishia malipo ya mshahara wangu. By the way kichapo kitaendelea kuwepo, siwezi kulea ujinga shuleni, mzazi akija nae anachezea kichapo akafundishe mtoto wake nyumbani kwake. Siwezi kulea jamii iliyokengeuka kimaadili, lazima nitimize jukumu langu la kuonesha jamii njia nzuri katika malezi na makuzi ya mtoto
 
Kwa hali ya sasa ilivyo, ualimu hasa sekondari ni hatari ya danger! Usipowapiga wao wanakupiga! Ukiwapiga ndivyo tulivyoyasikia
Usichape mtoto shule , kama anazingua bifu lirudishe kitaa ukampe vitasa huko nje ya shule mkaupange mkono huko huko , usimwachie jerahaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ akirudi shule atasambaza taarifa kwa madogo wenzie !!
 
Kwa jinsi walimu watakavyo Acha kuwaonya watoto inabdi niende shule niwalipe binafsi wanipgie mwanangu anapozingua ila kwa sasa walimu waache kuchapa aisee wazazi wenyewe ndo sisi ma single father na masingle mother unafikiri ata tunaweled wa malezi basi .
 
Tutafuata ushauri wako, ni kweli kufaulu au kufeli kutabaki kuwa jukumu la mwanafunzi kwa %100.
 
Ni bora wazazi na walezi waelimishwe faida ya viboko na sio kwamba viboko anavyochapwa mwanajeshi ndio achapwe mtoto Kama wewe ni mkristo soma kwenye biblia mithali 23:13(usimnyime mtoto mapigo) pia soma mithali 22:15(ujinga wa mtoto umefungwa kwenye fimbo) hata yesu aliwachapa watu ndani ya kanisa (yohana 2:12-25)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…