Wito: Watu Wenye Uwezo, Tujitokeze Tujitolee Kumsaidia TAL na Kuisaidia Chadema to Play Real Politics, No Reforms No Election ni Utopian Politics!.

Hizo Siasa Unazozitaka wewe Mbowe alishazifanya sana ila CCM bado inatamba, huo wakati ulishapita, Hivi unaamini kwa hizo siasa unazozitaka wewe CCM inaweza kuondoka? Kwa tume hii ya uchaguzi? Kwa katiba hii? Unajidanganya! Hizo zama zimeshapita, Sasa Lazima harakati na Nguvu kubwa itumike kuing'oa CCM kwa kuanza na 'NO REFORM, NO ELECTION' Tuone itakuwaje! Miaka mingi mabadiliko ya sheria za uchaguzi yameombwa na kuombwa na kuombwa! Lakini wapi! Mpaka sasa tunafika kwenye uchaguzi, HOLA! sasa kama mbwai wacha iwe mbwai! 'NO REFORM NO ELECTION'
 
Lisu siasa hauwezi anaweza uharakati tu.CHADEMA ya sasa imejaa vibaka na matapeli wa kisiasa
Taja kibaka angalau mmoja basi ili kifanya hoja yako iwe relevant, vinginevyo utakuwa unaupa mdomo kazi ya kuupanua halafu kinachotoka ni taka.
 
Hivyo vyote ulivyoviandika, ni kipi ambacho CCM tangu kuzaliwa kwake imekipatia solution!!??
 
Lisu siasa hauwezi anaweza uharakati tu.CHADEMA ya sasa imejaa vibaka na matapeli wa kisiasa
Kama una akili na ufahamu ulio sawasawa hebu eleza tofauti kati ya SIASA & HARAKATI..

Nimekuuliza swali hili kwa sababu nyie watu ni mazoba mnaokaririshwa na kulishwa chochote kwa sbb ya ujinga wenu. ..

Hamtumii akili zenu binafsi kuchakata mambo na kuyaelewa na kisha kuwaeleza wengine..

Mwanasiasa halisi siku zote ni MWANA - HARAKATI (activist). Na maana rahisi ya mwanaharakati ni MPIGANIA HAKI..

Ndio maana kuna wanaharakati wa kupigania

➡HAKI ZA KISIASA na KIRAIA- Mfano Hayati Mwl Nyerere na TANU yake hadi tukapata uhuru wa Tanganyika 1961, Martin Luther Junior mpigania haki za watu weusi maarufu huko Marekani; Tundu Lissu na CHADEMA yake ktk Tanganyika ya leo nk

➡HAKI ZA KIDINI - Mfano Martin Luther (Ujerumani) hadi kuzaliwa kwa kanisa la Lutheran duniani..

➡Wanaharakati wapigania Haki za kibinadamu, haki za kimazingira na uchumi nk nk

Bado huelewi tu..??
 
...ki kwetu tunaita Wivu!TAL ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Chadema na wewe ni wewe..40 years ijayo hutakuwa na legacy nzuri kutokana na kuitizama nchi kwa jicho hili..huoni shida yoyote kwenye Katiba ya nchi yetu...
 
Lissu kichwa resi alafu wasaidizi vichwa resi tupu changanya na bange!!
Chama wanaropoooka na kuvuta mibange Sasa kitafika wapi?
Kiukweli chadema chini ya lisu ni hamna kituu baada ya miaka mitano watavuruganaaa na wataishia kumwomba Mbowe arudi... tupo hapa!
Uhuni wakijinga wa Lema nagenge lake na mipango yao ya kukusanya mihela kwa wanachama kihuni itabomoa stutus ya chama kabiiisaaa
 
Chadema wakiamua kwenda kwenye uchaguzi kwa sheria za tume hii watakuwa wasindikizaji tu na watakachoambulia ni kutambiwa na masisiyemu kwamba tumewashinda kwa kishindo .Kama watawala hawataki mabadiliko ni bora wawaachie wajishindie
 
hivi mnapewaga hela ngapi huko fisiem kujizima data na hizo pesa zinamaliza matatizo au zinapooza njaa tu tafuteni mashamba mulime kilimo kinalipa na utaheshimika.
Nimeona wasanii pia wanazitafuta fursa za pesa walivyo na akili hizi fursa kumbe zinapatikana wakati wa uchaguzi, wamegundua ndiyo wakati wa mavuno, wajinga Ndiyo waliwao
 
Kesi ya Buthelezi ni tofauti. Mongosutu alikuwa Waziri wa mambo ya ndani na kukaimu Urais wa Nchi.
Mandela alipoulizwa kwanini anamwachia Buthelezi madaraka alijibu '' Tatizo liko wapi! Mimi ndiye Rais wa S.Africa, na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa. Maana yake ni kuwa kulikuwa na 'guard rails''
''State organs'' zote zilikuwa chini ya Mandela

TAL kwanza ni Mhanga wa Risasi 32 , lazima uelewe saikolojia kwamba anaishi kwa hofu, rightly so!
TAL anataka watu anaowaamini si kwasababu ya hofu bali pia Historia.
Yuko wapi Petrobas Katambi, Cecil Mwambe, Silinde ! Wako wapi COVID 19.

Ukizingatia ''state organs' ndizo zinafanya madudu tunayojua, nani amwamini mtu aliyesimama na kusema '' huyu ni mropokaji hafai'' akamdhalilisha sana!
Narudia madhila yaliyomkuta TAL na Historia havitoi nafasi kwa Ntobi kukaa meza moja kama viongozi. Wanaweza kukaa pamoja kama Wanachama
TAL angepoteza uchaguzi Mbowe angemweka pembeni. In fact kumweka Wenje ilikuwa ni mbinu.
Lema kasema, Msigwa ni Mhanga n.k. Tofuati ya FAM na TAL ni moja, TAL ni 'straight shooter' FAM ni '' silent killer''
Alisema hajawahi kuchangia chochote toka aingie Bungeni. Kwangu mimi ni ishara ya alivyo petty. Nadhani hajamsamehe kwa kusimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bawacha ambapo chaguo lake lilishindwa pamoja na kuwa aliwaomba wazi wajumbe wampigie kura.
No! kama alisema ni makosa. Aida Kenan amefanya kazi katika mazingira magumu sana. Nilimsikia sakata la DP na ndiye aliyetuwekea wazi ziara za Wabunge huko nyumbani kwa DP World.
Kasimamia uchaguzi wa BAWACHA vizuri. Ukimtazama ni kiongozi anayekua kifikra na kiungozi.
Atamdhalilishwa vipi? Hivi seriously anategemea Mwenyekiti mwenzake ambai ni Rais afanye debate nae?
Hee! huko Duniani Urais na Ugombea ni vitu viwili tofauti. Mkapa alifanya debate
Aliyeua debate ni Kikwete kwasababu ya udhaifu wake wa kujenga hoja.
Tunapaswa kurudisha utamaduni huo. Kwamba TAL aka debate nA Wassira ni kupoteza muda
Nawashauri Waandamizi wa TAL wafanyE debate kuonyesha madhaifu, TAL amsubiri Mwenyekiti wao
Wajiandae kwa kujikita zaidi kwenye grassroot na kuchagua wagombea ambao kweli watawakilisha matumaini ya watakaompigia kura. Watumie nafasi hiyo kuonyesha mapungufu ya CCM on the ground.
Please! Mbowe kashindwa kule HAI tena kabla ya uchaguzi. OC-CID wa Hai kamweleza wazi '' Wewe huwezi kumshinda wa CCM''. Huu ni mfano tu. Nitajie kiongozi mmoja wa CDM aliyejiandaa na kushinda 2020

Wakurugenzi wanakimbia Ofisi ili wasipokee Fomu!. Maboksi ya kura feki yanakamatwa Polisi wanasema hawana mamlaka ya kuchukua hatua! Akina Mawazo wanacharangwa mapanga. Leo unataka wajiandae ! Hivi kuandika fundi mchundo badala ya Fundi Mchundo kuna tatizo gani kisheria na wapi imeonyeshwa

Zitto Kabwe na ACT wameshiriki chaguzi zote ndogo! mwisho wa siku wametoa kilio cha mbwa koko.
umesahau ya Jecha ! Please unaweza kuisadia CCM kujenga hoja si kiwango hiki, you're better than this


Ni kuwa pragmatic tu kuwa hamna namna CCM itakubali Katiba Mpya kabla ya uchaguzi wa Mwaka huu.
Kwanini CCM wasikubali kuahirisha uchaguzi
Please JK alishindwa kumbuka hilo. CCM survival yao ni kupitia hii Katiba ndio maana hawataki kusikia chochote. Kwanini wasikubali kukaa chini na Wapinzani na kufanya hizo ''minimal reforms''
Mimi nadhani ni sign ya frustration baada ya kutosikilizwa na wenzake. Mchome hajasema hana imani na uongozi bali anataka taratibu zifuatwe. Ni hilo tu na ni rahisi ku sahihisha.
Mchome hana tatizo la kuhoji. Tatizo ni pale anapopeleka suala hili kwa Msajili wa Vyama.
Mbona hunielewi nikikupa mifano ya CUF na NCCR.
Niambie kulikuwa na sababu gani za Mbatia kuondolewa uongozi kwa hoja za Selasini. Nani alikuwa nyuma ya hilo. Unakumbuka Maalim Seif na Mahakama! na Msajili pia

CCM ni Chama dola kina Taasisi zote za Umma kinaweza kuzi abuse kadri kinavyotaka.
Hao Majaji 'data base' yao iko Ikulu wakisubiri kuteuliwa. Msajili anateuliwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais
Mchome ni kama anatoa fursa ya kuvurugwa chama
Amekikaanga vipi kwa kusema akidi ya kupitisha wateule haikutimia?
Hivi hili suala ni la kufika kwa Msajili wa Vyama tukijua Historia ya Taasisi hiyo
Hii ni nafasi nzuri ya uongozi kuonyesha kuwa kila mwanachama ana haki ya kukisoa bila kuhofia repercussions.
Nimeandika mara nyingi sana, Mchome ana haki ya Kuhoji, lakini kupeleka suala dogo kama hili kwa Msajili ni kuitafutia CDM matatizo ! hili litasimamiwa vema( wametoa taarifa ya kupokea barua) wala si viroja vya Mkutano Mkuu wa Dodoma. Kesho utasikia watu wanavyo toa maonyo na kufoka! subiri
Watu kama Mchome waanahitajika zaidi kuliko chaa waliojitokeza kwa kutaka kumuingiza Mbowe katika ishu nzima.
Wanahitajika lakini si kwa kuuza Chama! kulitoa suala hili nje ya Taasisi ni kuialika CCM na vyombo vyake kuwaondoa CDM katika agenda zao. Ni jambo la hovyo sana! kiongozi kama Mchome alipaswa kuona madhara yake unless ametumwa kama inavyosemwa
Amandla...

Mag3 JokaKuu
 
Zakayo.

Chadema imefanya Uchaguzi wake wa Kitaifa majuzi tu hapa, ni uchaguzi ambao umefuatilia na vyombo vyote vya habari vya ndani na nje. Matokeo ya uchaguzi ule ulikuwa ni habari kuu ya vyombo kama DW na BBC, bado una mashaka na Nguvu ya chama hiki? Unatumia vigezo gani kusema chama hiki hakina nguvu?

Issue ya Vyombo vya ulinzi na Usalama.
Unakosea kudhani kuwa Vyombo na Ulinzi na Usalama ni 'alien thing'. Hawa ni watanzania na raia kama sisi. So, hawa ni sehemu ya jamii, kinachotokwa kwa jamii kuhusu upinzani, rest assured hata kwenye vyombo hivi kipo vivyo hivyo. Tofauti tu hawa hawawezi itisha press na kuunga mkono hadharani. ALL IN ALL, WHAT MATTERS IS A PUBLIC SUPPORT, WENGINE HATA WASIPOUNGA MKONO, HAWAWEZI SHINDA NGUVU YA UMMA. This is fact. Historical fact.
 
MWANASIASA NI MWANAHARAKATI KWENYE SEKTA YA SIASA. WAPO WENGINE KWENYE SEKTA NYINGINE MFANO JAMII AFYA N.K. Kwa hiyo haijalishi, muhimu zaidi kule alichosimamia kina mantiki????
Jiulize maswali yafuatayo;
1. NI kwa kiasi gani wananchi tunapata nafasi kuchagua viongozi wetu? Na je viongozi wetu wanajali hilo?

2. Hitaji la time huru na katiba NI la wananchi au la chadema?
3. Lina mashiko au la kubeza Tu? No muda gana sasa hoja hii imepuuzwa na CCM hasa viongozi kisingizio maendeleo! Hakuna asiyetaka wala hakuna mwisho WA maendeleo!
 
ANC na IFP walichinjana sana kabla ya uchaguzi. Kwazulu Natal ilikuwa ni war zone. Ndio maana watu walimshangaa Mandela alipompa uwaziri kiongozi wa IFP (ingawa hakuwajibika kwa sababu IFP haikupata kura nyingi nchini isipokuwa tu Kwazulu Natal) mtu aliyekuwa mortal enemy wa chama chake. Aidha, pamoja na hizo guard rails waziri wa mambo ya ndani na acting president angeweza kufanya fujo sana.
Alichofanya Mandela ni kumthibitishia kuwa nchi yao ni kubwa kuliko tofauti zao. Hivyo hivyo Lissu angeweza kutumia nafasi ile kuonyesha kuwa kwake yeye chama chao ni kikubwa kuliko tofauti zao.
TAL kwanza ni Mhanga wa Risasi 32 , lazima uelewe saikolojia kwamba anaishi kwa hofu, rightly so!
TAL anataka watu anaowaamini si kwasababu ya hofu bali pia Historia.
Yuko wapi Petrobas Katambi, Cecil Mwambe, Silinde ! Wako wapi COVID 19.
Kwa hiyo alikuwa anaamini kuwa FAM alikuwa na mpango wa kumpiga risasi? Ndio maana alikuwa anavaa bullet proof vest akiwa katika maeneo ya Chadema? Hao uliowataja hamna aliyedhuru unywele wa kiongozi wa CDM. Cha ajabu, rafiki yake ambae haujamtaja anashutumiwa kuwa alihusika katika yaliyompata mmoja wa viongozi wa Chadema.

Aliyosema Ntobi ina tofauti gani na waliyosema yeye na surrogates wake kuhusu Mbowe? Kuwa Mbowe ni corrupt, ni mwizi wa ruzuku, amewasaliti, muongo n.k. Kwa hiyo argument yake ni kuwa kwa vile Ntobi ( na Nyerere) walisema wazi kuwa wanaamini kuwa hana sifa za kuongoza CDM basi walikuwa tayari kumdhuru? Kwangu mimi ni ishara ya pettiness hasa ukilinganisha na FAM ambae pamoja na kuteswa na kupoteza mengi alikuwa tayari kushirikiana na watesi wake kwa manufaa ya chama na taifa lake.
TAL angepoteza uchaguzi Mbowe angemweka pembeni. In fact kumweka Wenje ilikuwa ni mbinu.
Lema kasema, Msigwa ni Mhanga n.k. Tofuati ya FAM na TAL ni moja, TAL ni 'straight shooter' FAM ni '' silent killer''
TAL angeshindwa angesema uchaguzi haukuwa wa haki na angelianzisha. Na tayari alishaanza kuweka mazingira ya kudai kuwa kaibiwa uchaguzi. Mimi hiyo straight shooting ya TAL siioni. Yeye anatumia sana surrogates na insinuations ili kukwepa lawama. Na sasa hivi ameanza kuweka mazingira ya kumuangushia jumba bovu FAM kama hatafanikiwa. Tumeona chawa wake wanavyojitahidi kumuunganisha Mbowe na barua ya Mchome. Na yeye mwenyewe kuongea kwa mafumbo kuhusu hali mbaya ya kifedha aliyoikuta CDM. Mbowe ni ruthless kwenye afya ya chama chake. Alimstukia Msigwa akamshughulikia. Matendo ya Msigwa baada ya kukosa alichotaka ni uthibitisho kuwa alikuwa sahihi.

Sio kama. Alisema in public. Hautaki kukubali lakini ni ushahidi wa vindictiveness yake. Hajamsamehe kwa kumruhusu mtu ambae hakumtaka ashinde uchaguzi wa BAWACHA. Na utaona jinsi BAWACHA watakavyokuwa sidelined ukilinganisha na BAVICHA. Aidan, sio tu suala la DP bali alikuwa anaibua kila wakati suala la kesi ya FAM. Amekuwa pia akipambana na Lijualikali bila uoga wowote. Yote hayo Lissu hakuyaona? Hata mapambano ya Aisha wa Dodoma nayo hayaoni? Yeye anawaona wakina Rehema na Hilda tuu!
Hee! huko Duniani Urais na Ugombea ni vitu viwili tofauti. Mkapa alifanya debate
Aliyeua debate ni Kikwete kwasababu ya udhaifu wake wa kujenga hoja.
Tunapaswa kurudisha utamaduni huo. Kwamba TAL aka debate nA Wassira ni kupoteza muda
Hapo ndipo mnapokosea. Debate na Wassira ni nafasi ya kipekee ya kuweka wazi mapungufu ya chama chake. Hawatakiwi kupuuza nafasi yeyote ya kufanya hivyo. Kungojea mpaka debate ya wagombea urais ni kupoteza muda. CDM hawana luxury ya muda na resources.
Nawashauri Waandamizi wa TAL wafanyE debate kuonyesha madhaifu, TAL amsubiri Mwenyekiti wao
Hamna mjadala utakaoangaliwa na watu wengi kama wa TAL na kiongozi yeyote wa CDM. Heche ni debator mzuri lakini hatakuwa na impact kama Lissu.

CDM wanahitaji pesa. Na njia mojawapo ni kupitia kura watakazopata katika uchaguzi hata kama watadhulumiwa. Pesa hizo pamoja na kampeni zao zitawaweka vizuri kwa ajili ya 2029 ambapo kutakuwa na mpambano mkubwa ndani ya CCM.
Hivi kuandika fundi mchundo badala ya Fundi Mchundo kuna tatizo gani kisheria na wapi imeonyeshwa
Sielewi unataka kusema nini hapa.
Zitto Kabwe na ACT wameshiriki chaguzi zote ndogo! mwisho wa siku wametoa kilio cha mbwa koko.
umesahau ya Jecha ! Please unaweza kuisadia CCM kujenga hoja si kiwango hiki, you're better than this
Pamoja na kuuawa na kuonea bado wamo kwenye serikali ya GNU ya Zanzibar. Wao ni pragmatic na walijifunza kutokana na yaliyowakuta waliposusia uchaguzi. Mimi ni realist. Ni kujidanganya kudhani kuwa CCM watatishwa na slogans.
Mmeonyeshwa lakini hamtaki kukubali. Mnatakiwa mcheze chess sio checkers. Hicho ndicho alichokuwa anafanya FAM.
Kwanini CCM wasikubali kuahirisha uchaguzi
Sijaaona bado faida ya kuahirisha. Hivi mnadhani mkiwapa muda zaidi Bunge pamoja na serikali ya CCM ndio kutakuwa na mabadiliko yeyote. Njia bora ni kuwa na uchaguzi in the hope kuwa kutakuwa na mabadiliko bungeni ambayo yatawapa momentum katika madai ya Katiba Mpya. Ukweli ni kuwa hakuna Mwenyekiti wa CCM atakayekubali kuwa Rais wa kwanza ambae hakumaliza term mbili.
Please JK alishindwa kumbuka hilo. CCM survival yao ni kupitia hii Katiba ndio maana hawataki kusikia chochote. Kwanini wasikubali kukaa chini na Wapinzani na kufanya hizo ''minimal reforms''
Nashangaa jinsi ulivyo na imani na CCM. Mmedai Tume Huru wao wakaongeza neno "Huru" bila kufanya mabadiliko yeyote. Watashindwa nini kuwaletea Katiba Hii hii na kuiita Katiba Mpya ambayo itapitishwa na hili bunge ambalo wamekalia zaidi ya asilimia 90 ya viti. Mbunge wa CUF akiwaunga mkono watasema kuwa ina bi partisan support.
Mchome hana tatizo la kuhoji. Tatizo ni pale anapopeleka suala hili kwa Msajili wa Vyama.
Mbona hunielewi nikikupa mifano ya CUF na NCCR.
Mchome amepeleka nakala kwa Msajili baada kugonga ukuta kwenye chama chake. Mchome hataki Mapinduzi na hajaomba Msajili abatilishe uchaguzi wa uongozi wa juu. Ni arrogance ya uongozi mpya ndio uliomfikisha pale. Au mngefurahi mtu angeliibua hili suala karibu kabisa na uchaguzi? Sasa hivi muda wa kumjibu upo. Kama Lissu alivyokuwa anawaambia wakina FAM kuhusu tuhuma za Msigwa, jibuni tuhuma zake.
Niambie kulikuwa na sababu gani za Mbatia kuondolewa uongozi kwa hoja za Selasini. Nani alikuwa nyuma ya hilo. Unakumbuka Maalim Seif na Mahakama! na Msajili pia
Mbatia hahusiki hapa. Lakini wote Hao context ilikuwa ni tofauti. Hebu niambie Msajili anaweza kukidhuru vipi CDM kutokana na nakala ya barua aliyopewa. Kumbuka Mchome amesema wazi kuwa ana imani kabisa na walioteuliwa, shida yake ni ukiukwaji wa taratibu. Mjibuni hoja zake badala ya kushinda mkimtafuta puppet master.
CCM ni Chama dola kina Taasisi zote za Umma kinaweza kuzi abuse kadri kinavyotaka.
Hao Majaji 'data base' yao iko Ikulu wakisubiri kuteuliwa. Msajili anateuliwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais
Mchome ni kama anatoa fursa ya kuvurugwa chama
Uoga wenu tu. Chama kitavurugwa kama kitaendeleza arrogance na visasi. Hamtaki kuwwasikiliza wanao washauri lakini wakikaq kimya mnasema wamesusa kwa sababu mtu wao ameshindwa. Kuna thread humu ikimsema Boni Yai kuwa ushiriki wake sio kama zamani! Chama kinatakiwa kuonyesha maturity kwenye hili. Unfortunately, ni Makamu Mwenyekiti peke yake ndie anayeonekana kujitahidi kupoza moto na kujenga daraja. Akimzungumzia Mbowe, anamzungumzia kwa heshima. Na ana Sisilia kuwa hakuna atakayeonewa au kupendelewa kutokana na kambi aliyokuwemo wakati wa uchaguzi. CDM inatakiwa ifuate uongozi wake.
Mchome amesema hapakuwa na akidi. Katibu Mkuu akithibitisha kuwa akidi ilikuwepo hamna kitu ambacho Msajili anaweza kufanya. Hata kama hapakuwa na akidi, CDM inawezs kuita kikao haraka chenye akidi na kuliweka sawa jambo hilo.
Wanahitajika lakini si kwa kuuza Chama! kulitoa suala hili nje ya Taasisi ni kuialika CCM na vyombo vyake kuwaondoa CDM katika agenda zao. Ni jambo la hovyo sana! kiongozi kama Mchome alipaswa kuona madhara yake unless ametumwa kama inavyosemwa
Mlitake afanye nini kama hamkutaka kumsikiliza? Kuna kama mmoja wa CDM ambae amedai kuwa hata wazo la upatanishi lilipuuzwa. Makosa hapa ni ya uongozi, sio Mchome.

Naona umemtaja Mag3. Kwa taarifa ni kuwa sitaweza kusoma majibu yake kama ataongezea jambo maana nimemuweka kwenye orodha yangu ya watu ninao wa ignore. Aidha, sitaweza kuchangia kwenye chochote atakacho changia.

Amandla...
 
Hata Lisu asipofanikiwa lakni anapanda mbegu kwa wakati ujao. Sasa hivi hadi wazee wamekuwa machawa, hadi wasomi wamekuwa wajinga, Viongozi wa Dini hawakemei tena unyang'anyi wa haki. Tusipokuwa makini Serikali yetu itakuwa Mobutu Incarnated. Uchawa kila mahali mpaka nyinyi wazee.
 
Huu ni wakati wa Lisu kubadilika kwa asilimia kubwa mno, la sivyo CHADEMA inaweza kutoweka katika ramani ya kisiasa kama vlivyotoweka vyama vingine,itakuwa ajabu kuona CDM kila nyakati za uchaguzi inapotea kwenye ramani.
 
Mayala kwa kisukuma ni Njaa
 
Hongera Wakili Msomi Mayala kwa andiko fikirishi ingawa ingependeza mwanzoni kabisa ungedeclare interest( licha ya haya yote nitakayo yawasilisha, mm ni mwanachama kindakindaki wa CCM na hata pengine mzee wa kaunda suti) hii ingefanya ANDIKO lako lisomwe kwa angles zote

Labda nikuulize, unaridhika na Mchakato mzima wa Uchaguzi Tanzania?
Kama jibu ni HAPANA hiyo fursa kwa CDM inatoka wapi?

Inawezekana Lissu ( isomeke CDM) amekuja na gear kubwa ambayo labda inawakwaza wakuu wa nchi, shauri kama u mzalendo wa mama Tanzania, nini kifanyike ilikuboresha Mchakato mzima wa Chaguzi Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…