Wanabodi
Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.
View: https://www.youtube.com/live/u5PkOqrHdZI?si=Mtma0U4QBfJ8TJ6x
Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, ana baadhi ya madhaifu ambayo anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo, ili aweze kubadilika na kuachana nayo, abadilike kutoka TAL mwanaharakati awe transformed into TAL mwenye statemanship!.
TAL has always been mwanaharakati wa uchechemuzi, sasa TAL kama kingozi mkuu wa Chadema ni
lazime abadilike kuachana na TAL mwanaharakati, into TAL mwenye leadeship and president in waiting!.
Hakuna binadamu yoyote ni mkamilifu, hivyo hata TAL sio mkamilifu, moja ya weakness yake kubwa, he is not a good team player, as a result he is a bad liability as the top leader, uthibitisho ni huu
Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Ila mtu ukiwa na udhaifu fulani, unaweza kuutumia for your advantage. TAL is a liability ambayo hiyo liability can be transformed into an asset kama nilivyo shauri hapa
Japo Lowassa Alikuwa a Liability CCM, Akawa Asset Chadema. Lissu is a Very Bad Liability, but is The Only Asset Chadema Has Kuwangiza Ikulu!. Je... ?
Hivyo hivi vibwagizo vya uanaharakati, no reforms no election ni utopian politics, Chadema lazima ijikite into real politics , siasa za mikakati, politics of engegement, vinginevyo anakwenda kuizamisha Chadema kwenye a pit latrine!.
Hivyo hili ni bandiko la wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze to play the real politics of reality, hii falsafa ya TAL ya "No Reforms No Election" is not real!, ni utopian politics!.
TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!.
Hizi ni utopian politics, sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.
Mmoja wa washauri hao wa bure wa kujitolea ni huyu Mwana JF Maarufu sana, Mkuu
Mzee Mwanakijiji , msikilizeni hapa amewashauri nini Chadema na amemshauri nini TAL.
View: https://youtu.be/GUjpxNTSdig Ushauri huu ulitolewa kwa TAL miaka 5 iliyopita, Chadema mtafuteni huyu mtu atawasaidia sana!.
Japo wengi humu tunafahamiana kutokana na post za humu, sio members wengi wako real, hivyo sio vibaya from time to time mtu kujitambulisha tena na tena, mimi japo kazi yangu ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitemea kwa kujitolea, pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea, kazi inayoniweka mjini, sio kazi ya uandishi, utangazaji au uwakili, hivi vyote nafanya bure kwa kujitolea tuu kutokana na mapenzi yangu kwa uandish wa habari, utangazaji na uwakili, kazi inayoniweka mjini ni kazi nyingine kabisa, tena mimi ni kada wa chama cha siasa na sio Chadema, lakini nimeguswa kujitokeza kumsaidia TAL na Chadema kwasababu ya uzalendo wangu kwa nchi yangu, TAL na Chadema ni fursa kwa adhimu na adimu kwa uchaguzi wa 2025. Mwanzo niliwashauri wapinzani
Pre GE2025 - Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli 2025, Iachane na Urais, Ujikite Serikali za Mitaa, Ubunge na Udiwani, Urais labda 2030! lakini sasa kama zali tuu, fursa imeibuka kupitia TAL, kama ile fursa ya uchaguzi wa 2015 kupitia ENL, imejirudia 2025!
Mimi nimeisha wasaidia sana Chadema kwa kuwashauri,
- Nilimshauri Lissu aache uanaharakati aonyeshe statemamship JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship
- 2015 Chadema ilikuwa waingie ikulu lakini kuna makosa waliyafanya, Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... sasa Chadema wana fursa tena ambayo imejotokeza kama zali, wasiridie makosa!
- Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua hapa niliwashauri Chadema namna ya kujinasua, ushauri wangu umefuatwa ndio Chadema hii inayoiona sasa, umeutambua uchaguzi na sio uchavuzi, imelitambua Bunge, imemtambua rais, sasa Chadema inalamba ruzuku ndio hii ipo!.
- Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?
- Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane! hapa Chadema walikuwa hawamtambui mbunge wake, baada ya ushauri huu, sasa wanamtambua!.
- Ushauri wa bure: CHADEMA iachane na issue ya Wabunge wake 19, iwasamehe waendelee na Ubunge wao. Kwa muda uliobakia kuwatengua hakuna maslahi yoyote! hapa nimewaombea msamaha hawa wabunge, Chadema haina wanawake wowote wa calibre ya Halima Mdee, Ester Bulaya na Esta Matiko!.
- Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...
- Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini hapa niliilaumu Chadema hawajui wanataka nini na watapataje, hata sasa Chadema chini ya Lissu, bado hawajitambui!.
- CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena! hapa niliwalaumu Chadema hawajipangi!, hadi sasa chini ya TAL, Chadema haijajipanga na isiposaidiwa, haijipangi!. Huu ni mwaka wa uchaguzi, TAL anazungumzia no reforms no election, amepanga kusimamisha uchaguzi kwa maandamano!. Uchaguzi mkuu wa 2025 ni fursa kwa TAL na Chadema, badala ya kupanga mikakati ya kuchangamkia fursa, watu wanapanga kususia!.
- Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition? hili lilikuwa swali la 2020, hata hii 2025 Chadema hawajabadilika!, 2025 Chadema ina fursa, isipobadilika na kuchangamkia fursa, 2025 ni CCM tena!.
- Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli! Kama JPM alikuwa Dikiteta... TAL ni zaidi ya JPM!.
- Elections 2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu! hii ni hoja ya udikiteta Chadema, TAL ni kama JPM, hivyo TAL akipewa nchi 2025, Keko, Ukonga na Segerea kutafurika!.
- Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA hii ni moja ya Sifa njema za TAL
- Lissu apunguze hasira na malipizi, atapendwa na wengi
Natoa wito, kwa watu wowote, wenye uwezo, kutoka popote hata wana CCM, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, kwa kuishauri kuwa uchaguzi mkuu wa 2025, Chadema ina fursa!, hii ni fursa adhimu na fursa adimu kwa Chadema kuichangamkia, muda uliobaki kabla ya uchaguzi, sio rafiki kufanya siasa za kiharakati, huu ni muda wa kufanya siasa za kimikakati ya ushindi, tena namshauri TAL na Chadama wakumbatie falsafa ya pragmatism politics, wawe pragmatic and do what is possible!.
TAL na Chadema Wasaidiwe waachane na utopian politics, wafanye real politics, the time is almost too little too short!, hakuna muda wa kupoteza!.
Paskali