Wito: Watu Wenye Uwezo, Tujitokeze Tujitolee Kumsaidia TAL na Kuisaidia Chadema to Play Real Politics, No Reforms No Election ni Utopian Politics!.

Kwa no reform no election chadema na lissu Wako sahihi sana. Uchaguzi kwa tume hii ni maigizo tusidanganyane
 
Kuipeleka chadema kwenye uchaguzi huu wa maigizo ni kukimaliza, kwa tume hii hakuna kitu
 
Aisee nimesoma mpaka nimechanganyikiwa wazee huyu jamaa ambition yake ni kuwaconfuse wapinzani na nimegundua analipwa rasmi kwa kazi hiyo

Yuko deadly kwenye uandishi wake kuhakikisha anaonekana kama mpinzani flani in the mean time anawa notify wana ccm wenzake kwamba yeye ni mfuasi mwenzao so ili asije lose trust ya hao akaonekana sio mwenzao tena yaani amerudia uzamani wake.

This dude ashaona kabisa kwamba ni maji ya shingo yaani imeshakuwa jioni sana so ni vema apambanie sana tumbo lake and so he doesn't care anymore.
 
Lissu ni tapeli tu. Sasa hivi wakisema kura zirudiwe hapati hata asilimia 20% ya kura zote. Watu walimuamini lakini matarajio yamekuwa tofauti mno, TAL hana utulivu pia uanaharakati ni mwingi. TAL ana tatizo la akili, he's somehow psychopathic!
 

Ubunge na udiwani kwa sheria hizi ni kupoteza muda. Chaguzi za Polisi na usalama wa taifa kwenda kwenye ubunge hivi ni kupoteza muda. Kati ya vitu vya kizalendo walivyo fanya Chadema ni hii ya no reform no election kwasababu
1. Kwanza watatoa elimu ya chaguzi
2. Wana data za kuongesha kwa chaguzi tatu

Hakuna njia ya kushinda hii debate vs chadema kwasababu kuna data. Sasa makada wanakuja na agenda na topic kama hizi ambazo hazieleweki. Wananchi watapata elimu na kuhundua Chadema wapo sawa ni muda tu
 
Lissu ni tapeli tu. Sasa hivi wakisema kura zirudiwe hapati hata asilimia 20% ya kura zote. Watu walimuamini lakini matarajio yamekuwa tofauti mno, TAL hana utulivu pia uanaharakati ni mwingi. TAL ana tatizo la akili, he's somehow psychopathic!

Jidanganyeni tu jamaa wanaanza kutoa elimu ya kura nyie propaganda😂
 
Kwanini badala ya kumzuia TAL kufanya harakati zake. Kwanini msiifumue tume ya uchaguzi na kuitengeneza ionekane kuwa iko fair. Hamna haja ya kuogopa wala, ukweli ni huu CCM inakubalika na kuaminika zaidi kuliko vyama vyote vya upinzani.

Na nionavyo mimi wanaotoa hoja kama hizi ni kwasababu deep down wanaamini kwenye mfumo wa chama kimoja na hawataki mabadiliko. Na pengine watanzania walio wengi wanaamini kwenye mfumo wa chama kimoja. Basi tu wanauvumilia upinzani kwasababu unafaida flani flani hasa kuiwajibisha serikali ya chama chao kipenzi CCM inapojisahau.

Amini nakuambia ukiwajaribu watanzania kisawasawa utathibitisha kuwa wanapenda mfumo wa chama kimoja. Na tena wamekwishajaribiwa na jaribu lenyewe lilikuwa ni hili. Mwaka jana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa CCM walishinda kwa asilimia 99 nasikia hadi kura za ndio na hapana zilirudishwa. Lakini je uliona maandamano yoyote najua utasema wanaogopa polisi, lakini je ulisikia manung'uniko yoyote ya kutisha vijiweni, sanasana mm nilikuwa nikiwauliza watu walikuwa wanasema tushasahau.
 
Kama tumejitokeza ama tutajitokeza sii lazima kifanana na matendo au tabia za wale chawa wa kijani,tutajitokeza bila kujitangaza wala kijigamba wala kujimwambafai.
 
Sasa na utofautishe weupe na kuwauzia ubongo wako walio pelekea uwe chawa.
 
Nafikiri misingi yote ya demokrasia ikiwa sawa basi tutasahau migomo kama hii ya uchaguzi. Ila ni kweli, ni muda muafaka kwa wana CHADEMA kuanza kuzungumzia ajenda yao ya maendeleo
 
Nafikiri misingi yote ya demokrasia ikiwa sawa basi tutasahau migomo kama hii ya uchaguzi. Ila ni kweli, ni muda muafaka kwa wana CHADEMA kuanza kuzungumzia ajenda yao ya maendeleo
Naunga mkono hoja, Chadema wafanye siasa za kimikakati na sio siasa za ki harakati na siasa za utopia!.
P
 
Pascal Mayalla uyu jamaa ana akili kuliko wewe na mzee wasira.uchaguzi wa Nini kama Kila kitu wanasimamia ccm??
 
Jibuni hoja za Lissu.
Kabla hata ya kujibu hoja, Chadema wasaidiwe kufundishwa kujenga hoja zenye nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu!.
Waende kwenye uchaguzi kwa sheria hizi baada ya 2019,2020 na 2024 ili iweje?.
Sheria mbovu ipo toka 1995, Chadema imeitumia imeingiza wabunge karibu 100, what did they do kutaka mabadiliko?.
Bila kujibu hizi hoja hii topic nzima haina hoja
Huku sio kulitendea haki bandiko langu, hili ni bandiko la kuiombea msaada, TAL asaidiwe, Chadema wasaidiwe, kuachana na utopian politics na kufanya real politics
No reforms no election is utopian!

Hakuna ubishi kuhusu umuhimu wa reforms, lakini huwezi kusema no election, kwasababu, si TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi usifanyike!. Kusema kitu ambacho huna uwezo nacho, ni utopia!, ni hadaa!, Chadema isaidiwe!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…