chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Nashauri wizara ya fedha, wizara ya teknokojia ya habari na mawasiliano zijikite katika kupenyeza na kueneza masuala ya uchumi ya kijiditali(digital economy).
Waitwe wataalamu kutoka nyanja zote wafanye presentation na michakato ya jinsi watanzania wanaweza kufaidika na kuutumia uchumi wa kidijitali.
Sawa, tumezoea kilimo, tufanye, ufugaji, tufanye, uchumi wa bluu, tufanye, uchumi wa madini na kadhalika, ila tujikite katika hili pia.
Naona vijana hutumia fedha nyingi kununua bando ambalo mwisho wa siku hulitumia kwa mambo ambayo hayana faida kiuchumi. Ifanyike survey tu ya matumizi ya bando, utakuta kwa mwezi mtu anatumia Malaki, lakini si kwa faida yoyote kiuchumi zaidi ya kumuangalia mwijaku na makasa yake, au baba levo.
Angalia vijana hawa hapa chini wanavyochoma fedha kuongea upuuzi mitandaoni bila kujua hapo fedha imekwenda. Ni faida gani wangepata endapo wangejadili fursa za kiuchumi?