Wizara: Serikali haina uwezo kuwakopesha wanafunzi wote

Wizara: Serikali haina uwezo kuwakopesha wanafunzi wote

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712

hitimu-sylvia-temu.jpg

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylivia Temu

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema haina fedha za kutosheleza kuwakopesha wanafunzi wote walioomba mkopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu na kusema imetoa Sh. bilioni 306 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara hiyo, Sylvia Temu, alisema serikali imekwishatoa Sh. trilioni 1.6 kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004.

"Tatizo kubwa, kuna changamoto ya fedha. Serikali haiwezi kukopesha wanafunzi wote wanaopeleka maombi HESLB. Tunaomba taasisi binafsi waunge mkono katika kuchangia elimu," alisema Temu.

Aliwataka wadau, watu binafsi na taasisi mbalimbali katika sekta ya elimu kuchangia elimu kwa kushiriki kusomesha watoto.

Kwa mujibu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), wanafunzi walioomba mkopo ni 58,037 wakati bajeti iliyotengwa na serikali ilikuwa ni kutoa mkopo kwa wanafunzi 30,000 tu mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE
 
Si wanatuona sisi wananchi kama misukule yaani sisi sio binadamu na wenyew ndo binadamu pamoja na mitoto yao.
 
Punguza jaziba ndugu yangu mi ndo basi tena kusoma naona kama ndoto yangu itakua inaishia kwenye mikono ya ccm
 
We ngoja dawa yao ndogo,kwani hao watakao pata hizo pesa hawatarudisha?

Hakuna maana yakutoa mikopo kwa wanafunzi wengi huku baadhi yao wakionekana kuhangaika nakujutia kwa nn wamechaguliwa kujiunga na elimu ya juu wakati huohuo hata hiyo pesa wangekopeshwa wangetakiwa kurudisha hapo badae, hichi kitu hua kinaniuma sana japo kuwa na mm mlengwa na sijajua nipo group gani ila hii serikali yetu kwa tabia hii haitaweza kuzalisha wahitimu mbalimbali katika nyanja tofautitofauti katika nchi yetu hii.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki loans board.
 
Halafu CCM wanategemea vijana wakipende chama chao, maweee! Vijana watakowapenda CCM ni wale wanaonufaika moja kwa moja na upuuzi wao.

Vv
 
jamaa wanachekesha sana,ndio maana mi husema watu wamesoma ila hatuna wasomi jiulize yani heslb, moevt, nacte, tcu na m.finance hawana demand forecast.

Mfano mama anadai hajui idadi ya watoto wake,na atawalishaje wakati chakula kimejaa nyumbani!

Mfano, mwingine watu 28000- 8000 unapata watu 20000 jumlisha na wa 2016/2017 mpaka 2020! je si watakuja kukosa mkopo wanafunzi kama100,000. Wauze uranium tusome wote!.
 
mwanzo wa kutuma maombi walisema wamejipanga kutoa mikopo wa kwa wanafunz 35000. sa hv wanadai wametoa kwa watu 30000, plz Bodi jarib kutusaidia watoto wa hali ya chin
 
Tanzania kweli bado. Yaani mambo ya muhimu kama haya ya kupata mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu wenye vigezo badala kupewa kipaumbele kwa kutenga fungu kubwa zaidi, ikiwa ni hata kwa kuomba msaada wafadhili kutoka nje wawasaidie, serikali wao wanaelekeza nguvu yao katika mambo mengine yasiyo hata na tija kubwa kwa taifa., mfano.safari za mheshimiwa nje ya nchi akisindikizwa na timu yake ya watu wapatao 60 hivi.

Sina hakika mpaka sasa safari zake za nje zimefikia ngapi na zimegharimu kiasi gani cha mapesa ya walipakodi. Kama mtakumbuka vizuri gazeti la M.wa.na.ha.li.si miaka minne iliyopita lilishawahi kuanika uozo huu.

Kwa kukumbushia kidogo,Kwa viwango vya serikali, watu wanaosafiri kwenye msafara wa rais hulipwa kiasi cha kati ya dola 350 na 500 (Sh. 600,000 kwa siku).

Sasa zidisha mara jumla ya idadi yao: halafu zidisha na siku wanazokaa huko nje: gharama za hoteli na usafiri:na jumla ya safari zote: HAKIKA UTACHOKA.
 
Ila inauwezo ya kuwakopesha wabunge woote tena mamilioni ya shilingi na dolali
 
hitimu-sylvia-temu.jpg

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylivia Temu

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema haina fedha za kutosheleza kuwakopesha wanafunzi wote walioomba mkopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu na kusema imetoa Sh. bilioni 306 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara hiyo, Sylvia Temu, alisema serikali imekwishatoa Sh. trilioni 1.6 kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004.

“Tatizo kubwa, kuna changamoto ya fedha. Serikali haiwezi kukopesha wanafunzi wote wanaopeleka maombi HESLB. Tunaomba taasisi binafsi waunge mkono katika kuchangia elimu,” alisema Temu.

Aliwataka wadau, watu binafsi na taasisi mbalimbali katika sekta ya elimu kuchangia elimu kwa kushiriki kusomesha watoto.

Kwa mujibu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), wanafunzi walioomba mkopo ni 58,037 wakati bajeti iliyotengwa na serikali ilikuwa ni kutoa mkopo kwa wanafunzi 30,000 tu mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE

Bahati Tweve na wana UDSM wengine waliliona hili back in 2004 lakini Maghembe alimtukana na kumdhihaki bungeni!!
 
Tanzania kweli bado. Yaani mambo ya muhimu kama haya ya kupata mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu wenye vigezo badala kupewa kipaumbele kwa kutenga fungu kubwa zaidi, ikiwa ni hata kwa kuomba msaada wafadhili kutoka nje wawasaidie, serikali wao wanaelekeza nguvu yao katika mambo mengine yasiyo hata na tija kubwa kwa taifa., mfano.safari za mheshimiwa nje ya nchi akisindikizwa na timu yake ya watu wapatao 60 hivi.

Sina hakika mpaka sasa safari zake za nje zimefikia ngapi na zimegharimu kiasi gani cha mapesa ya walipakodi. Kama mtakumbuka vizuri gazeti la M.wa.na.ha.li.si miaka minne iliyopita lilishawahi kuanika uozo huu.
Kwa kukumbushia kidogo,Kwa viwango vya serikali, watu wanaosafiri kwenye msafara wa rais hulipwa kiasi cha kati ya dola 350 na 500 (Sh. 600,000 kwa siku). Sasa zidisha mara jumla ya idadi yao: halafu zidisha na siku wanazokaa huko nje: gharama za hoteli na usafiri:na jumla ya safari zote: HAKIKA UTACHOKA.

Duh! pole pole sn comrade!una hasira sana lakn membo ndo hayo.Miaka ya nyuma niliwahi kupata shida sana juu ya hili mpaka nikaamua kujitosa kusoma diploma japo nilikua na ufaulu mzuri tu.

Baada ya kupata kaajira changu nkaamua kujisomesha mwenyewe na kwa sasa sina deni na mtu na najisomesha masters salsa.Kitu ni malengo ndugu yangu, hii ndo bongo bhana.

Nilipata uchungu sana kuona wenzangu ambao wazazi walikua na unafuu wakipata loan me mlala hoi kila siku nasaga kandambili zang kufalia loan ofisini.

Nawashaur waliokosa wasikate tamaa waangalie na plan B kama nilivyo fanya Mm japo hata diploma ya ualim saiv ni 600,000.
 
Back
Top Bottom