Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylivia Temu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imesema haina fedha za kutosheleza kuwakopesha wanafunzi wote walioomba mkopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu na kusema imetoa Sh. bilioni 306 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka wizara hiyo, Sylvia Temu, alisema serikali imekwishatoa Sh. trilioni 1.6 kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004.
"Tatizo kubwa, kuna changamoto ya fedha. Serikali haiwezi kukopesha wanafunzi wote wanaopeleka maombi HESLB. Tunaomba taasisi binafsi waunge mkono katika kuchangia elimu," alisema Temu.
Aliwataka wadau, watu binafsi na taasisi mbalimbali katika sekta ya elimu kuchangia elimu kwa kushiriki kusomesha watoto.
Kwa mujibu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), wanafunzi walioomba mkopo ni 58,037 wakati bajeti iliyotengwa na serikali ilikuwa ni kutoa mkopo kwa wanafunzi 30,000 tu mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE