Ngarob
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 661
- 2,204
Wizara ya Afya / Waziri wa Afya tunawapa pongezi kwa jitihada mbalimbali mnazofanya lengo likiwa ni kuimarisha afya ya mtanzania.
Kuna changamoto kadhaa hasa kwa baadhi ya madaktari katika kutibu wagonjwa mbalimbali kutanguliza maslai binafsi katika hospitali za u make badala ya tiba sahihi kwa mgonjwa. Naomba niorodheshe baadhi.
I) Madaktari wengi hawakai kwa muda sahihi katika kuhudumia wagonjwa, wengi wao huondoka mapema kazini wakikimbilia hospitali binafsi kwa ajili ya manufaa yao
II) Baadhi ya madaktari wa Serikali wasio waaminifu huwaelekeza wagonjwa kwenda katika hospitali binafsi (private clinic) kwa ajili ya maslai binafsi, na baadhi yao huweka appointment huko katika hospitali binafsi.
III) Baadhi ya Madaktari wa Serikali wasio waaminifu huwaelekeza wagonjwa kwenda nje ya kituo kwa ajili ya vipimo (hata vidogo kama ultra sound) kwa ajili ya kujipatia fedha za ziada / Manufaa binafsi.
IV) Baadhi ya madaktari wa Serikali hujihakikishia wakitoka mapema kazini au baadhi yao hukwepa kabisa kwenda kazini kwa ajili ya private clinic.. Hujipatia kipato kikubwa 50,000 kwa siku au zaidi na baadhi yao huwa wanalipwa kwa mwezi 1,000,000 na fedha hizi hazina makato (TRA Hawajui).
V) Baadhi ya Madaktari wa Serikali wasio waaminifu hujaribu kuzuia ajira za madaktari wachanga waliotoka vyuoni wasiajiriwe katika hospitali binafsi kwakuwa wao hutoka mapema mno kazini (Serikalini) ili waje wafanye kazi private hospital.
Waziri / Wizara ya Afya natumaini baadhi ya malalamiko haya yatafanyiwa kazi. Baadhi ya Madaktari hawaridhiki na ajira zao, wanataka kuwa sehemu mbili mpaka tatu kwa wakati mmoja hali ambayo itapunguza ufanisi wa matibabu.