Uandishi gani huu umejaa bold nyingi hivyo?
Siku 11, wamechanja watu 105,000, maana yake kwa siku wanachanja watu 9,535. Kwa mikoa 26 maana yake kila mkoa kwa siku unachanja watu 367. Hilo la kwanza.
La pili, kama kwa siku wanachanja wastani wa watu 9,535, iwao watanzania 50% watatakiwa kuchanjwa, yaani watu milioni 30 itahitajika siku 3,146 ama miaka 9 kuwachanja wote. Hilo halitoshi bado birth rate ni kubwa sana Tanzania maana yake hii chanjo haitaisha, itakua ni kuchanja for life.
Tukumbuke kabla ya kumaliza hata 1% ya watanzania, yaani 600,000 imeanza chanjo nyingine inaitwa booster shot ya kuipa nguvu hii chanjo iliyopo. Kwa maana kwamba kamaumechanjwa, utahitaji kuchanjwa tena hiyo booster vaccine.
Kwaa hiyo iwapo tutahitai kumaliza hizi zilizopo halafu tuanze booster ama tunaenda nazo concurrently itakua shughuli pevu.
Mimi nitakua wa mwisho kuchanja.