#COVID19 Wizara ya Afya: Hadi Agosti 7, 2021, watu 105,745 walikuwa wamepatiwa chanjo ya UVIKO-19

Unawaza nini mzee? Mbona vitu ni rahisi pia.

Ni factors zipi unatumia?

Changamoto kubwa ni utayari wa watu kuchanjwa na uwepo wa chanjo.

Miundombinu haina shida. Hata wiki tu tunaweza chanja 30m+.
You can't be serious aisee.

Miundombinu gani uliyonayo ya kuchanja 30m kwa wiki moja hata kama wote watakua tayari hapa Tanzania?

Nimekupa mfano wa nchi kama South Afrika ambayo zaidi ya 80% wananchi wake wako tayari kwa chanjo lakini kwa miezi 7 wamechanja 3.5% ya population.

South kwenyewe ambapo kuna miundombinu bora zaidi ya Tanzania haiwezi kuchanja 30m kwa wiki moja sembuse Tanzania?

Naona labda huelewi, ngoja nikusaudie zaidi. Marekani aliacha chanjo mwezi December 2020, watu zaidi ya 200m walikua tayari na radhi kuchanjwa lakini ametumia miezi 8 kuchanja 150m, kwa wastani wa 18m people per month.

Tanzania hiyo miundombinu ya kuchanja watu 30m kwa wiki hata kama wako tayari kiasi gani inapatikana wapi?
 
Nasikia wengine tayari washaanza na Booster....

Muhimu ni let us all respect individual decisions - kuchanja au kutochanja. Maana mwisho wa siku bado kuvaa barakoa, kunawa mikono na tahadhari nyingine lazima ziendelee.
 
Chuo kikuu nilifundishwa kitu kinaitwa MATHEMATICAL REASONING.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…