Wizara ya Afya: Hakuna tishio la UVIKO-19, likiwepo tutatoa taarifa

Wizara ya Afya: Hakuna tishio la UVIKO-19, likiwepo tutatoa taarifa

Naunga mkono Tamko LA Serikali Kuwa Hakuna tishio la Corona.

Walitoa waraka wakati mwingine wanapokea maagizo kutoka nje
 
Sasa kama hatuna maambukizi ya COVID-19, mbona tahadhari iliyopo kwa sasa ni ndogo sana?

Ni kama vile tunalala milango wazi, tukiamini hakuna wezi wala wadudu pori wataovamia ndani ya nyumba yetu...
 
Kanimaliza kusema tuache wanasayansi wafanye kazi yao. Sijui ana maanisha wana sayansi hawa wa kwetu au wale original? Nchi hii kazi tunayo ngoja niandike kwa herufu kubwa. HATUTAKI LOCKDOWN TUNATAKA KUAMBIWA UKWELI ILI TAHADHARI ZIWE KWA WATU WOTE BILA KUCHAGUWA WEWE UNAAMINI NINI, TO DEAL NA FACTS SIO MAONO YA MTU KAMA TUNABISHANA SIMBA NA YANGA.
 
Wakati Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) likiwataka waumini wake kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya corona ambavyo vimeshambulia nchi kadhaa, Serikali imewataka wananchi kutoingiwa na hofu bali wasubiri maelekezo ya Serikali.

Waraka wa tahadhari wa TEC ulitolewa jana na Rais wa Baraza hilo, Gervas Nyaisonga akiwaandikia Kardinali, maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu wastaafu ikiwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Tahadhari juu ya maambukizi mapya ya virusi wa korona na ugonjwa wa Uviko-19 (covid-19)”

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi jana, Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Dk Goodluck Mollel alisisitiza msimamo wa Serikali kuwa hakuna tishio la ugonjwa wa Covid-19 na likitokea watatoa taarifa.

Katika waraka huo, Askofu Nyaisonga alisema tangu mwaka 2020 kumekuwa na hatua za kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona na zilizoonekana kufanikiwa.

“Kwa mwaka jana nchi yetu ilifanikiwa katika mapambano haya dhidi ya corona. Visa vya maambukizi ya corona vilipungua na baadaye tukaamini tumeshinda,” alisema Nyaisonga katika waraka huo.

Hata hivyo, alieleza mwaka huu kumekuwa na wimbi jipya la maambukizi ya corona duniani.

“Nchi kadhaa zimethibitisha kuwa zinapitia kwenye kipindi kigumu cha kuenea kwa corona na kutokea kwa vifo vya watu. Nchi yetu sio kisiwa,” alisema Askofu huyo.

Aliendelea; “Kwa uhalisia huo, tusiache kuwashauri, kuwahimiza na kuwaongoza taifa la Mungu katika mapambano haya dhidi ya virusi vya corona. Tuhimize mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa kutumia silaha zote za kiroho, kimwili, kisayansi na za kijamii. Tusikome kuhimiza sala, kuepuka kugusana, kunawa na kujitakasa kila wakati, kuchukua hatua tuonapo dalili za ugonjwa na kuepuka misongamano hatarishi.”

Akizungumzia barua hiyo, Katibu Mkuu wa TEC, Dk Charles Kitima alikiri barua hiyo kuwa ya Kanisa Katoliki, akisema jukumu la kanisa ni kushughulikia uhai wa watu. “Moja kati ya majukumu ya Kanisa ni kushughulikia uhai wa watu. Serikali labda na vyombo vingine bado vinafanya utafiti na uchunguzi, lakini sisi tunaona watu wanaingiliana na nchi yetu iko huru, kwani watu wanaingia na kutoka nje, yanaweza yakatokea, wanaokuja wakatuletea.

Alipoulizwa kuhusu msimamo wa Serikali kuhusu ugonjwa huo, Dk Kitima alisema; “Serikali yetu itasema, lakini ukienda `airport’ (uwanja wa ndege) Dar es Salaam kuna watu wanaingia kutoka nchi zenye corona. Kwa hiyo sisi siyo kisiwa tunaishi na watu na wengine ni wagonjwa.”

Kauli ya Serikali
Akizungumzia tamko hilo, Dk Mollel alisisitiza hakuna maambukizi ya ugonjwa huo nchini, akawataka wananchi wasubiri maelekezo ya Serikali.

“Hamna kitu kama hicho. Hizo habari mnazosema ni za mitandaoni tu, tuwaachie wanasayansi wafanye kazi zao, subirini Serikali kama kuna tatizo itawaambia. Kwa sasa endeleeni na shughuli zenu kama kawaida,” alisema Dk Mollel alipozungumza kwa simu na mwandishi wa habari hizi.

Alisema suala la kuchukua tahadhari kama kunawa mikono kama wakati wa corona, haimaanishi kwamba corona imerudi.

“Hilo suala lilikuwa linasaidia mambo mengi zaidi ya corona. Sasa hao wanaosema tujikinge na corona ukiwauliza wamepima wapi wakathibitisha kwamba kuna corona, hawawezi kukwambia zaidi ya kusema kuna watu wanaobanwa na kifua. “Waulize, ni leo Watanzania wameanza kubanwa na kifua au ni kwa sababu mvua imeanza? Kwani nimonia imeanza leo?

Tangu umezaliwa si umekuwa ukiambiwa watu wanaumwa kifua wakati wa baridi? Wakati wa baridi na wakati wa joto ni upi kuna kuwa na matatizo ya kifua? “ alihoji. Alipoulizwa kuhusu tahadhari zinazochukuliwa kwenye hospitali za Serikali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili ya watu kuvaa barakoa kwa wanaoingia, Dk Mollel alisema ni utaratibu wa kawaida.

“Kuingia na barakoa hata mimi ninapokuwa natibu wagonjwa natakiwa niingie na barakoa. Ni kitu ambacho kinatakiwa kifanyike, kwani hospitalini kuna magonjwa hayatakiwi yavaliwe barakoa?”
Hizo taarifa rasmi za serikali azisubiri yeye sisi tunachukua tahadhari zote za kujikinga na korona.
Hivi anafikiri hawa maaskofu hawasimamii mahospitali tena za maana kuliko hizo za serikali na kwamba wanajua in and out ya kile kinachoendelea huko mahospitalini kwa sasa?
 
IMG_9627.jpg

Magufuli kajubali korona ipo basi na ccm watakubali kweli corona ipo , ivi kweli mtu mmoja anasemea anawaendesha hivi ???
 
Msameheni molleli wa watu bure, asingeweza kusema zaidi ya hicho alichosema kwani uwezo wake wa kusema ulikua unaishia hapo, mlitaka aende zaidi ya hapo afanyiwe ya ndugu yake ndugulile? Raisi Magufuli aliwahi kusema "Watanzania sio wajinga" nafikiri hata sasa kauli hii inatufaa sana mintarafu uviko-19 toleo jipya.
 
Ukiingia kwenye siasa unajifunza kuwa laghai hata kama wewe ni mwanasayansi inaikataa sayansi! Mbaya unawafanya watu wote ni wajinga na kwamba wewe tu ndiyo mwerevu
 
Back
Top Bottom