Wizara ya afya imetoa muongozo kwa watumiaji wa magari ya Mwendokasi

Wizara ya afya imetoa muongozo kwa watumiaji wa magari ya Mwendokasi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa muongozo kwa watumiaji wa Magari ya mwendokasi ili kujikinga na maambukizi ya #CoronaVirus.

Wasafiri wanaotumia magari ya mwendokasi wanatakiwa kuvaa barakoa hususani asubuhi na jioni, kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu wakati wa kusubiri usafiri.

Vituo vya Mabasi ya Mwendokasi vinawekewa maji na sabuni ambayo kila msafiri atatakiwa kunawa mikono. Pia wametakiwa kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya.

Aidha wasafiri wanatakiwa kusubiri basi lingine ikiwa basi lililofika limejaa.

1614078157701.png
 
Si waruhusu magari binafsi yapewe vibali vya kusafirisha abiria. Hawaoni kuwa mwendokasi haitatosha. Au wanataka mpaka watu waanze kufa vituoni nchi ipate aibu kimataifa. Latra ruhusuni magari binafsi.
 
Bongo social distance ngumu sana kutekelezeka

Msongamano ndiyo zetu kushikanashikana bambiana

Ova
 
Haya matamko ya nini wakati mlisema hakuna corona kuna changamoto na mkatusihi tuibadili kuwa fursa?
 
Slowly but surely measures zinaanza kuchukuliwa. Ingependeza pia wangetoa muongozo kulazimisha kila anayeingia ofisi za Serikali kuvaa barakoa maana sasa hivi kila manispaa inafanya kivyake.

Ilala huingii bila (1) barakoa (2)kunawa mikono mlangoni kwa maji tiririka na sabuni chini ya uangalizi mkali wa Mlinzi wakati Ubungo Municipal unaweza hata kuingia ukiwa uchi
 
Naona ni Wizara ya Afya na DART, je UDART anasemaje? atakubali kuondoka na abiria walioko kwenye viti pekee?
 
... kwani kuna Corona? Wengine wanasema Tanzania haina Corona! Hatua ya kwanza ya kukabiliana na tatizo ni kukiri kwamba lipo. Mengine yanafuata.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Si waruhusu magari binafsi yapewe vibali vya kusafirisha abiria. Hawaoni kuwa mwendokasi haitatosha. Au wanataka mpaka watu waanze kufa vituoni nchi ipate aibu kimataifa... Latra ruhusuni magari binafsi.
... magari binafsi yapi? Noah au? Maana hata madaladala yaliyopo hayatoshi.
 
Mdogo mdogo tumeanza kuelewana, mbona heicher hazijazungumziwa all in all Mungu ni mwema kila wakati!
... mwandishi wa barua ni DART; anazungumzia kilicho ndani ya mamlaka yake kiutendaji; daladala (Either) sio mamlaka yake! Ndio maana tunasema for proper enforcement, inatakiwa hii kitu (Corona) lead itoke from higher authorities badala ya hizi rejareja ambazo hazitamaliza tatizo.
 
Farao ameanza kuelewa lakini asichokijua ni kwamba bado kuna mapigo mengi sana mpaka akiri kwa kinywa chake bila shuruti kuwa Corona ipo kwa wingi sana na ni tatizo kubwa sana!
 
Farao ameanza kuelewa lakini asichokijua ni kwamba bado kuna mapigo mengi sana mpaka akiri kwa kinywa chake bila shuruti kuwa Corona ipo kwa wingi sana na ni tatizo kubwa sana!
... hilo ni pigo la ngapi Mkuu? Nakumbuka Farao alitekeleza agizo la Mungu kupitia mjumbe wake Musa baada ya wa nyumbani kwake kuanza kutafunwa. Mapigo mengine yote alishupaza shingo lakini walipoanza "kuliwa" wazaliwa wa kwanza wakiwemo wanae na wanyama wake, pozi lilimwishia.
 
Back
Top Bottom