SoC03 Wizara ya Afya iunde mfumo mmoja wa kompyuta wa afya utakaotumika katika ngazi zote za hospitali za Serikali ili kurahisihsa rufaa na mengineyo

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
UTANGULIZI.

Kutokana na kukua kwa teknolojia kwa sasa mambo mengi yanafanyika kwa njia ya mtandao na mifumo ya kompyuta, sekta ya afya inatumia mifumo ya afya kukamilisha huduma kwa wagonjwa ambapo taarifa zote zinakuwepo katika mfumo huo.

Kila hospitali inatumia mfumo wake kulingana na mahitaji yake ,na mifumo ipo ya aina nyingi kulingana na ubunifu wa waunda mifumo na haiwezi kuingiliana katika utendaji.

Hospitali za serikali zimegawanyika katika Zahanati za kijiji, Zahanati ya kata, Hospitali ya wilaya, Hospitali ya mkoa, Hospitali ya Kanda, Hospitali ya taifa, na hospitali maalumu. Hospitali hizi zinapangwa kulingana na uwezo wa huduma zinazotolewa kwamba kuna tatizo haliwezi kutatuliwa na zahanati ya kijiji inabidi liende zahanati ya kata,likishindikana zahanati ya kata liende hospitali ya Wilaya,kisha Mkoa,Kanda na hatimae Taifa,hii nikutokana na ubora wa miundombinu na rasilimali watu katika ngazi husika.

Kwa kawaida mgonjwa anapotoka ngazi ya chini kwenda ya juu huwa hapewi faili la matibabu isipokuwa kama amesafirishwa kwa dharura kwa gari ya wagonjwa kitu kinachopelekea kuanza upya kuchukua maelezo ya mgonjwa ambayo kwa namna moja ama nyingine huongeza gharama za matibabu kwa mgonjwa maana utakuta katika siku moja ileile anapimwa kipimo kimoja zaidi ya mara mbili ndani ya muda mfupi tu,ama kumcheleweshea matibabu kwa sababu yakuchukua historia upya.

Sambamba na hilo kuna wale wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda hospitali za juu kabisa wamekuwa wakiingia gharama na kupoteza muda kwenda kutafuata matibabu ambayo anaweza kukaa hata miezi mitatu akisubiri huduma kwa sababu tu hakuna mfumo maalumu wa rufaa za wagonjwa,ndugu wakilazimika kulala kwenye mabaraza na mara nyingine na mgonjwa wao wakisubiri siku wamuone daktari ama wapate majibu ya vipimo vipya.

Mara nyingi mgonjwa anapotoka hospitali ya mkoa kwenda ya kanda mathalani vipimo huwa vinakwenda kufanyika ni vile vile labda kama kipimo flani hakuweza kupatiwa hapo awali, swali najiuliza kuna ulazima gani wa mgonjwa kupoteza muda katika hatua ya juu ya matibabu kwa kurudia kuchukua taarifa na vipimo vilevile upya hata pasipo sababu za msingi?

MAPENDEKEZO ILI KUBORESHA HUDUMA ZA RUFAA.

Kwa kuwa hospitali zote 80% hutumia mifumo ya kompyuta,basi serikali kupitia wizara ya afya iunde mfumo mmoja wa afya wa kompyuta ambao utatumika na hospitali zote za serikali nchi nzima na isitishe matumizi ya karatasi katika zahanati, ambapo taarifa za mgonjwa zitaweza kuonekana katika mfumo kuanzia hatua ya awali kabisa,
na kabla mgonjwa hajafika hospitali taarifa zake za rufaa ziwe zimeshatumwa ngazi inayofuata na mgonjwa ataambiwa aende hatua ya juu mpaka pale itakaporudishwa taarifa kwamba rufaa yake imepokelewa na mgonjwa aende ili asipoteze muda na gharama za usafiri,na malazi atakapokuwa huko,yaani siku atakayopangiwa ndio hiyo afike na apate huduma na taarifa zake zote zinakuwa tayari zimepitiwa na daktari aliyepangiwa, isipokuwa kwa waonjwa wa dharura tu ambao taarifa zao zikitumwa zitaonekana kama dharura na mgonjwa atapelekwa tu hata kama hakuna majibu yeyote ila faili lake tayari litakuwa limefika huko.

Kwa kuwa kuna vijiji vingi ambavyo umeme wa gridi ya taifa hakuna,serikali isambaze vishikwambi maalumu vilivyowekwa mfumo huo kwa ajili ya kutolea huduma,na viwe na uwezo mkubwa wa kutunza chaji.

MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA MFUMO.


Mfumo uwe na sehemu zifuatazo,Ngazi ambapo kutakuwa na ngazi kuanzia Zahanati, hospitali ya wilaya, mkoa, kanda na taifa na Maalumu, katika kila ngazi ya Zahanati zipatikane kwa kuzingatia mkoa, wilaya, kata kisha kijiji yaani muhudumu akifungua kitufe cha Zahanati, aweze kuchagua mkoa aliopo, kisha wilaya, kisha kata na hapo ataona majina ya zahanati za vijiji na kuchagua kijiji chake na hapo ataweza kuingia katika mfumo kwa nywila yake,nakupata huduma zote muhimu kulingana na ngazi yake,huduma atakazoweza kuziona hapo ni zile ambazo wizara imejiridhisha kwamba zinaweza kutolewa katika ngazi hiyo.

Kwa ngazi ya wilaya yeye akifungua kitufe cha ngazi ya wilaya basi ataona orodha ya mikoa na kuchagua mkoa aliopo,kisha wilaya aliyopo hapo ataweza kuingia katika akaunti yake na kutoa huduma, mfumo huo huo kwa ngazi za juu ndio utakaotumika.

Daktari ataweza kutoa rufaa kupitia mfumo ambapo kutakuewepo kitufe cha “Option”
katika sehemu ya kuchapa maandishi kwa chini kulia ama vyovyote ambapo,akichagua “Referal” basi mfumo utamtaka kuandika sababu ya rufaa hiyo na itampatia chaguo lakuonesha kama ni Dharura ama ni ya kawaida na kuituma,mfumo utaielekeza rufaa hiyo wapi kwa kwenda kulingana na ngazi inapotoka rufaa hiyo,nakatika kila ngazi ya juu kutakuwepo na muhudumu maalumu kwa ajajili ya kushughurikia taarifa zote za rufaa zinazotumwa kutoka chini ili kuhakikisha zinafanyiwa kazi kwa wakati na muhudumu huyu atakuwa ni mtaalamu wa kuhifadhi taarifa za afya (HEALTH DATA RECORDER),rufaa inapotumwa mfumo utatuma faili zima la mgonjwa ambalo taarifa ikifika ngazi ya juu na kupokelewa ,mfumo uweze kutengeneza faili la mgonjwa husika na kushikiza faili dogo lilotoka ngazi ya chini ndani ya faili hilo.

Daktari ambaye atapewa jukumu la kushughulikia mgonjwa aliyepewa rufaa husika baada yakupitia faili lake yeye ndio atafanya maamuzi ya kwamba mgonjwa aonane naye lini, na kama hakuna sabau ya kumuona,atafanya mawasiliano na daktari aliyeandika rufaa na kumpatia maelekezo nini chakufanya, kisha ata “REJECT” rufaa hiyo na kuandika sababu ya Ku “REJECT” na maelezo kamili hapo ambapo ataweza kuandika “procedures” za kumuhudumia mgonjwa husika(Sharti awe na uhakika wa kwamba zinaweza kufanywa katika ngazi husika),lakini pia mfumo uweze kuruhusu mawasiliano kwa njia ya video ambapo daktari wa ngazi ya juu anaweza kuwasiliana na wa ngazi ya chini na kuwasiliana na mgonjwa ikibidi.

Rufaa ikikataliwa na kukubaliana basi fumo utaliondoa faili katika kanzi data ya ngazi husika.

Mfumo pia uwe na sehemu ya “DATA RECORD” na QUALITY ASSURANCE” ambapo mfumo utaweza kuhakiki taarifa zote za ubora huduma kwa kila ngazi ,lakini pia wadhibiti ubora kufuatilia taarifa za ubora kwa kila ngazi na kuchapa taarifa mbalimbali.

Mfumo umruhusu DMO na RMO kukagua kituo chochote katika wilaya ama mkoa wake.

FAIDA ZA KUTUMIA MFUMO MMOJA KWA NGAZI ZOTE.
  • Itarahisisha rufaa.
  • itaepusha gharama zisizo na ulazima kwa wagonjwa .
  • Huakikisha uwepo wa taarifa zote za mgonjwa kuanzia ngazi ya chini.
  • Huokoa muda kwa pande zote.
  • Mpangilio wa matibabu kwa mgonjwa unakuwa mzuri.
  • Huakikisha upatikanaji wa taarifa bora na sahihi za kitabu kwa wakati.
  • Huimarisha uhusiano mzuri baina ya watendaji wa afya kuanzia ngazi ya chini mpaka juu.
  • Huongeza ujuzi haraka kwa wataalamu wa ngazi ya chini hususani kwa kufanya mawasiliano na kuzuia rufaa nakutoa muongozo wa nini kifanyike.
 
Upvote 6
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…