Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Leo hii hata ukienda Uchina nchi ambayo mlipuko ulianzia, lazima wakuweke karantini siku kumi na nne haijalishi umepimwa umekutwa na virusi vya corona au hukukutwa navyo.
Kitu kingine wataalamu wanasema Mtu mwenye Corona anaweza kuonyesha dalili za Corona Corona lakini ukampima mara kadhaa usione kama ana kirusi lakini vipimo vya baadae ndo huonyesha ana kirusi.
Cha ajabu nimesoma taarifa za wizara ya afya juu ya washukiwa wa kuugua Corona kutoka nchi fulani za Ulaya, Wizara inasema eti pamoja na hao watu kuonyesha dalili za mafua huku mmoja na mwongine akionekana kulegea isivyokawaida wamewapima na kuwakuta negative KISHA WAKAWAACHIA WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO.
Naishangaa sana wizara kuwaachia hao watu kipindi hiki badala ya Kuwashuku na kuwaweka kwenye Karantini huku wakiendelea kumonita maendeleo ya afya zao.
Hivi Waziri Ummy Mwalimu anavyoona mpaka Trump anafunga mipaka na kuzuia wazungu wenzie kutoka ulaya wasiingie marekani anaona hii ni hali ya mchezomchezo?
Wizara ya afya na serikali wanatuangusha sana jinsi wanavyochukulia hili jambo bila userious sana.
Iwapo hili janga litaibuka nchini, wananchi wakaanza kufa, hawa viongozi wa serikali wanaocheza na maisha yetu watawajibika kwa hakika, wananchi hatutokubali hata kidogo incompentency ya aina hii kuweka rehani maisha yetu, kwa hakika watawajibika.
Serikali haiko serious kabisa na hili janga!
Missile of the nation(Kombora hatari kabisa la ulinzi wa Taifa)