misasa
JF-Expert Member
- Feb 5, 2014
- 14,244
- 10,073
Wewe ndio unaleta siasa mkuu.unaleta siasa sasa
Unahisi kila anayehusika wizara ya afya yupo humu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ndio unaleta siasa mkuu.unaleta siasa sasa
Unajiitaje detective na maswali unayouliza mepesi hivo. Unamaanisha tokea ugonjwa uibuke mpaka leo hujui kuwa mtu anakuwa isolated mpaka siku 14 zifike ndo wajue hana.
Wee tulia watu wafanye kazi zao , usiwafundishe kazi kama kufa utakufa tu kelele za nini.Tatizo linguine nchi nzima vipimo vinafnyikia national lab, hili ni tatizo, sababu mgonjwa yeyote mwenye. Ugonjwa wa mlipuko hutakiwi kurefer, so unakaa nae pale ukisubiri majibu toka national lab kulikojaa siasa unagegemea watakuletea positive result kweli,, CCM hivi ndio mmeamua kutumaliza
Sent using Jamii Forums mobile app
Tume survive Ebola, Nzige....nina imani hata hili litapita.
Mtanzania ukigundulika na huo ugonjwa walai madaktari wanakuzika ukiwa hai useendelee kuueneza
View attachment 1388084
Leo hii hata ukienda Uchina nchi ambayo mlipuko ulianzia, lazima wakuweke karantini siku kumi na nne haijalishi umepimwa umekutwa na virusi vya corona au hukukutwa navyo.
Kitu kingine wataalamu wanasema Mtu mwenye Corona anaweza kuonyesha dalili za Corona Corona lakini ukampima mara kadhaa usione kama ana kirusi lakini vipimo vya baadae ndo huonyesha ana kirusi.
Cha ajabu nimesoma taarifa za wizara ya afya juu ya washukiwa wa kuugua Corona kutoka nchi fulani za Ulaya, Wizara inasema eti pamoja na hao watu kuonyesha dalili za mafua huku mmoja na mwongine akionekana kulegea isivyokawaida wamewapima na kuwakuta negative KISHA WAKAWAACHIA WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO.
Naishangaa sana wizara kuwaachia hao watu kipindi hiki badala ya Kuwashuku na kuwaweka kwenye Karantini huku wakiendelea kumonita maendeleo ya afya zao.
Hivi Waziri Ummy Mwalimu anavyoona mpaka Trump anafunga mipaka na kuzuia wazungu wenzie kutoka ulaya wasiingie marekani anaona hii ni hali ya mchezomchezo?
Wizara ya afya na serikali wanatuangusha sana jinsi wanavyochukulia hili jambo bila userious sana.
Iwapo hili janga litaibuka nchini, wananchi wakaanza kufa, hawa viongozi wa serikali wanaocheza na maisha yetu watawajibika kwa hakika, wananchi hatutokubali hata kidogo incompentency ya aina hii kuweka rehani maisha yetu, kwa hakika watawajibika.
Serikali haiko serious kabisa na hili janga!
Missile of the nation(Kombora hatari kabisa la ulinzi wa Taifa)
Katiba mpya.Kwanini wizara hizi nyeti walau wasiwe wanapewa watu wenye taaluma husika?
Wee tulia watu wafanye kazi zao , usiwafundishe kazi kama kufa utakufa tu kelele za nini.
Wewe huko kazini kwako nani anakuingiliaga maamuzi???
Ummy Mwalimu amepiga sheria pale UDSM akafanya masters ya sheria kule Pretoria South Africa.Naibu waziri Dr.Faustine Ndungulie yeye ndio Medical Doctor(MD) na MPH,waziri hatoi maamuzi peke yake anajadiliana na makamu wake.Ujue hii nchi inaendeshwa Kiswahili swahili sana! Nchi za wenzetu mwenye kuonyesha dalili anakuwa in isolation angalau kwa siku 14. Huku kwetu eti vipimo vimepelekwa Dar leo kesho mtu anaruhusiwa kwenda na mambo yake.
Hivi huyu waziri wa afya taaluma yake ni mambo ya afya au? Maana unaweza kukuta ni fundi mchundo alafu anapewa wizara nyeti namna hiyo.
kama hukumuelewa rais usikurupuke kumbeza!Ni heri ithibitike kuwa ipo ili watu waanze kutumia akili. Rais mzima anasema hata usiku msipigane mabusu na patakuwa na raha tu halafu anasema eti tunapambana na corona? Naona sasa wana show zao za kusalimiana kwa miguu!
Basi washauri wa huyo waziri hawako makini. Au na yeye hashauriki kama mzee baba?Ummy Mwalimu amepiga sheria pale UDSM akafanya masters ya sheria kule Pretoria South Africa.Naibu waziri Dr.Faustine Ndungulie yeye ndio Medical Doctor(MD) na MPH,waziri hatoi maamuzi peke yake anajadiliana na makamu wake.
Kuwa waziri hakuitaji huwe mtaaram wa sekta uliyopewa,japo sijawahi kuwa waziri ila natamani sana hicho cheo .
Ukae nao siku 14 utawalipia chakula na accommodation siku hizo zote ????watu washakuwa tested waachwe waende zao we wasiwasi wako nn,ushaambiwa uchukue tahadhali hauelewi Tu,waTanzania mna vichwa vizito kweli.
Makamu ndio anamshauri waziri na ndiye mtaaramu kwenye hiyo sekta,yeye ndio kasomea udktari wa binadamu na afya ya jamii sasa unasemaje kwamba hamshauri vizuri au unakitaka cheo cha unaibu huwe mshauri wa waziri???Basi washauri wa huyo waziri hawako makini. Au na yeye hashauriki kama mzee baba?
Soma mada ya mleta uzi kisha soma comment yangu.Makamu ndio anamshauri waziri na ndiye mtaaramu kwenye hiyo sekta,yeye ndio kasomea udktari wa binadamu na afya ya jamii sasa unasemaje kwamba hamshauri vizuri au unakitaka cheo cha unaibu huwe mshauri wa waziri???
Fuatilia uelewe huo ugonjwa.Jmn si wamewafanyia uchunguzi wakagundulika hawana. Tatizo liko wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app