DOKEZO Wizara ya Ardhi, huu usajili mlioutoa kwa kwa kampuni ya KMM ni kwa faida ya nani?

DOKEZO Wizara ya Ardhi, huu usajili mlioutoa kwa kwa kampuni ya KMM ni kwa faida ya nani?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

NGOSWE2

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
1,323
Reaction score
1,608
Vitendo vya utapeli vinavyofanywa na kampuni ya KMM LAND USE CONSULTING CO.LTD, yenye namba ya usajili 0359-T0218, iliyo na ofisi Sinza - Dar es Salaam. Kampuni hii ilipewa kibali cha upimaji katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, lakini imeshindwa kutoa huduma kwa wananchi kwa mujibu wa malalamiko yaliyotolewa.

Kampuni ya KMM LAND USE CONSULTING CO.LTD inashutumiwa kwa kuchukua fedha kutoka kwa wananchi bila kutoa huduma zinazohitajika. Wananchi walikuwa na imani kwamba watapata huduma za upimaji na upangaji wa ardhi, lakini baada ya kulipa pesa, hawajapata huduma yoyote. Ingawa wananchi wamejaribu kutoa malalamiko yao ya kazi, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya kampuni hii.
Mbaya zaidi, kampuni hiyo imeajiri wanaopita mitaani kuwasihi wananchi kutoa fedha tena ili waweze kuendelea na kazi zao. Hata hivyo, bado hakuna maendeleo au huduma zinazotolewa kwa wananchi baada ya kulipa pesa hizo.

Serikali imejua kuhusu malalamiko haya kwa muda mrefu kupitia barua na taarifa kutoka kwa mitaa mbalimbali. Ingawa wamejaribu kupata msaada kutoka kwa ofisi za serikali, hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya kampuni hii. Wananchi wanajiuliza kwa nini serikali inakumbatia kampuni hii licha ya vitendo vya utapeli inavyovifanya.

Kwa nini serikali haichukui hatua dhidi ya kampuni ya KMM LAND USE CONSULTING CO.LTD licha ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi? Kampuni hii inahudumia maslahi ya nani, na kwa nini haifuatiliwi kwa makini na serikali?
Naiomba serikali ichukue hatua za haraka dhidi ya kampuni hii ili wananchi waweze kupata haki zao. Ni kuboresha mfumo wa usajili na udhibiti muhimu zaidi muhimu ya upimaji na upangaji ili kuhakikisha huduma zinazotolewa ni za kweli na zinakidhi viwango vilivyowekwa.

Wananchi wanatarajia hatua za haraka kuchukuliwa ili kumaliza tatizo hili na kuhakikisha kuwa haki za wananchi zinaheshimiwa.
 
Back
Top Bottom