Wizara ya Elimu acheni kuwa madalali wa Scholarship za Ubalozi

Ukikutana na wahusika, ukikutana na mapokezi, huwezi kuepuka kuanzia wizarani ambako kuna vigezo vimeongezwa na lugha yako haitakusaidia kuvipita hivyo vigezo.

Kwa mfano, wewe si mfanyakazi wa serikali. Warusi hawana kigezo cha wewe kuwa mfanyakazi wa serikali ili kupata scholarship.

Ukienda kuongea na Mrusi Kirusi wakati Wizara imeweka kigezo cha wewe kuwa mfanyakazi wa serikali, kujua kwako Kirusi kutakupitishaje kwenye hicho kigezo cha kuwa mfanyakazi wa serikali?
 
Natamani Watanzania wapate fursa ya kusoma nje. Kuna mambo mengi ya kujifunza. Pamoja na kutoka familia maskini nilipata fursa ya kusoma nje (Uingereza na sehemu fulani Ufaransa) na wakati wa likizo nilikwenda Ireland na likizo nyingine Poland na nilijifunza mambo mengi ambayo yamenisaidia kuwa kama nilivyo leo. Nilisoma kwenye chuo ambacho tulikuwa wanafunzi kutoka mataifa 27 duniani na kila mwaka chuo kili'organise' cultural day - siku ambayo kila taifa/continenti walionyesha utamaduni wao. It was very interesting. Kwa kifupi, kusoma nje ni eye-opener.
 
Nielewe Mkuu nimetumia Urusi kama case study ila sidhani kama ukienda kukutana na Watu wa ubalozi moja kwa moja ukazungumza nao lugha yao watakuacha! Kumbuka kuwa ukienda nchi ambazo lugha ya vyuo vyao sio kiingereza ni lazma usome lugha yako kwanza ndo uendelee na masomo. Sasa wewe ndo unayechagua nani aende na nani asiende, kuna mmoja ana cheti cha level B1 cha lugha na mwingine hana, utamchagua nani?1​
 
Ila sio kila mtu anataka kila mtu aende kuosha macho nje
 
Hujaelewa au unapuuza point ya msingi.

Unazungumzia kwamba ukijua Kirusi ubalozi hautakuacha.

Wakati mchakato wa scholarship umehodhiwa na serikali wizarani.

Serikali wizarani imeweka vigezo vya figisu kibao. Mfano kigezo cha mtu kuwa mfanyakazi wa serikali.

Sasa, kwa mfano wewe si mfanyakazi wa serikali, kirusi unakijua. Utapenya vipi hapa wizarani ambapo kuna kigezo cha kuwa mfanyakazi wa serikali, ili uweze kufika ubalozini kujionesha unakijua Kirusi?

Kumbuka, kwa mchakato wa sasa wizarani ndio wanakupitisha uende ubalozini. Mchakato wa schokarship unaanza wizarani, si ubalozini.

Sasa, unaongeleaje kuwa impress watu wa ubalozini kwa Kirusi chako wakati watu wa wizarani hawajui wala kujali kirusi, wana vigezo vyao tofauti kama uwe mfanyakazi wa serikali, ambavyo wewe hujavifikisha?

Huoni kwamba una address kigezo cha ubalozini kabla ya cha wizarani wakati mchakato unaanzia wizarani?
 
Kwa hoja yako ni kwamba Wizara ndo inawaomba ubalozi kuwa inahitaji kuwapeleka watanzania nje au!?
 
Hapa kwa nilivyomuelewa ni kwamba hata kama mchakato unaanzia wizarani ila kitendo cha kujua culture yao ya kujua lugha yao ya kirusi basi kuna uwezekano ubalozi husika wakati wa kuselect watu ukapewa kipaombele regardless ujaenda wizarani.
 
Ni kweli Mkuu! Nimekuelewa! Na hoja kuu ni kuwa Wizara isaidie tu kufanikisha watu waende sio kuwa wachambuzi tena na madalali.
 
Huelewi wapi?

Ubalozi umepewa masharti kwamba usichukue mtu yeyote ambaye hajapitia wizarani. Wizara imekuwa ndiyo point ya kwanza ya kupitia kabla ya kufika ubalozini.

Isn't that so?

Mbona swali moja la msingi hamlijibu?

Wizara ndiyo inachuja nani wa kumpeleka ubalozini.

Ukijua Kirusi bila kutimiza vigezo vya wizarani, kama kuwa mfanyakazi wa serikali, utapenya vipi wizarani ili ufike ubalozini?

Yani mchakato ni lazima uanzie point 1 (wizarani), watu wa wizarani ndio wanaamua nani aende point 2 (ubalozini), unafikaje ubalozini kuomba scholarship ikiwa hujapenya wizarani?

Hujajibu swali hili.
 
Ni kweli Mkuu! Nimekuelewa! Na hoja kuu ni kuwa Wizara isaidie tu kufanikisha watu waende sio kuwa wachambuzi tena na madalali.
Wizara ime monopolize mchakato, ndiyo first contact ya kuchuja watu wanaoweza kupokelewa ubalozini.

Ukienda ubalozini moja kwa moja unaambiwa pitia wizarani.

Isn't that so?
 
Kwa hoja yako ni kwamba Wizara ndo inawaomba ubalozi kuwa inahitaji kuwapeleka watanzania nje au!?
Siyo kwamba wizara ndiyo inawaomba ubalozi kuwa inahitaji kuwapeleka Watanzania nje.

Wizara imeweka utaratibu kuwa scholarships zote, za nchi zote, mchakato wake unaanzia wizarani.

Kwamba mtu hawezi kujiendea mwenyewe ubalozini tu akachukua schokarship juu kwa juu.

Ukienda ubalozini, unaambiwa fuata mchakato wa kuanzia wizarani.

Umeelewa hapo?
 
Ndugu yangu hapa TZ hakuna anayetaka utoboe zaidi ya mama yako, roho za korosho sana zimejaa huko maofisi ya serikali...hizo nafasi zipo sana tu na Wala hazijazwi sababu ya roho ya kutu, mbongo anaona Bora asijaze mtu kuliko kupata wewe mtu Baki na ndivyo ilivyo si tu kwenye suala kama Hilo bali ni katika masuala chungu nzima, tuna mentality za hovyo za kwamba Bora tukose wote tu.

Adui wa mtanzania ni mtanzania mwenzake.
 
Ok!
Uturuki walitangaza ufadhili wa masomo ambao watu iliwataka kuingia kwenye Türkiye Bursları
Je hapo Wizara inahusikaje wakati ukitazama guidlines zao zipo hivi

Nisaidie Mkuu Wizara ya Elimu inaingia sehemu ipi?!
 
Safi sana!
 
Ok!
Uturuki walitangaza ufadhili wa masomo ambao watu iliwataka kuingia kwenye Türkiye Bursları
Je hapo Wizara inahusikaje wakati ukitazama guidlines zao zipo hivi
View attachment 3059402

Nisaidie Mkuu Wizara ya Elimu inaingia sehemu ipi?!
Hilo ni tangazo la Waturuki kwa dunia nzima.

Kwa Tanzania, mchakato unaanzia Wizarani. Wizara imetaka ku streamline scholarships ukienda ubalozi wa Uturuki watakuuliza kama umepitia wizarani. Hilo ni sharti walilopewa na wizara.
 
Nimekuelewa vyema sana Mkuu! Ndo kitu ambacho ni cha ajabu hiki kwa wizara!
 
Hizo scholarships wametaka kuzi control wizarani kwa sababu wanataka kupeana kindugu.

Hizi ndizo wamesomea hao kina Dr. Hussein Mwinyi.

Mnashangaa watoto wa watu fulani tu wanapata scholarships, wengine hawapati.
Watanzania ni wachoyo sana sijui kwanini!? Hapo unakuta hata watoto wa kina fulani wameshaandaliwa kupewa nafasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…