Wakati watanzania wanalia kwa ajili ya tozo na wengine wakizozana kuhusu mikopo, na ugumu wa maisha, Wizara ya fedha inaufisadi wa kutisha. Waziri mkuu alitangazia taifa kugundua wizi wa mabilioni ndani ya miezi 3. Kuanzia March 2021, hadi Mei 2021. Miradi mingi imekwama, na mashirika mengine ya umma yana suffer, lakini fedha zinaibiwa wizara ya fedha kwa njia ya kalamu as if hakuna auditors, hakuna supervision wala regulations.
Tangu Waziri mkuu atoe agizo la uchunguzi, taarifa gani imetoka? Ni kweli mtindo huu umeanza mwezi March baada ya Rais Magufli kufariki au umekuwepo kabla? Ni wizara hii tu ama ni mtindo wa Serikai yote? Kama haya mambo yanaokana ni kawaida, maana yake uvunjaji wa kanuni na sheria ni donda ndugu katika Serikali. Kama sivyo, serikali inachukua hatua gani za kulinusuru taifa na Wizara inayohalalisha ubadhilifu wa namna hii, hasa ukizingatia ni Wizara inayotarajiwa kutunza raslimali za taifa?
Serikali inawezaje kuwa na imani na Wizara ya namna hii, hata kuendelea kuwaamini wafanye maamuzi kwa ajili ya maslahi ya taifa? Ushauri wangu kwa Serikali, ifumue hii wizara na kuweka watu wapya wanaojali maslahi ya taifa. La sivyo ninanusa harufu kali ya rushwa ili kupotosha maamuzi, ushauri mbaya kwa serikali na conspiracy kubwa ya wizi wa mali za Umma.
Hii wizara ni msiba mkubwa kwa Watanzania maskini.