Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Naibu Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega amesema bidhaa zote za kigeni zinazoingia nchini zitafutiwe utaratibu wa kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.
Na bidhaa ambazo zinazalishwa nchini ziwekewe utaratibu wa kuwa na maelezo ya Kiswahili ili kumrahisishia mtumiaji wa bidhaa ambaye anafahamu Kiswahili.
Ametoa mfano wa Dawa ambazo mtumiaji anapaswa ajue tahadhari za kutumia dawa hiyo na sio kuishia kujua idadi ya vidonge vya kutumia kwa siku. Malezo hayo yakiwa kwa Kiswahili itasaidia hili.
Amesema hayo ni kwa mujibu wa Kanuni zilizopo hivyo Wizara ya Habari itakaa na Mamlaka ili kuhakikisha utekelezaji wa Kanuni inayotaka bidhaa ziwe na maelezo ya Lugha ya Kiswahili.