Wizara ya Katiba na Sheria Yahudumia 3,000 Msaada wa Kisheria Sabasaba

Wizara ya Katiba na Sheria Yahudumia 3,000 Msaada wa Kisheria Sabasaba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

Wizara ya Katiba na Sheria Yahudumia 3,000 Msaada wa Kisheria Sabasaba​

Watu zaidi ya 3,000 wamepatiwa msaada wa kisheria na Wizara ya Katiba na Sheria, ndani ya siku 13 kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), Sabasaba, yanayoendelea.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro wakati alipotembelea banda la wizara hiyo na kutoa huduma ya msaada huo wa kisheria kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo.

Amesema kuanzia Juni 28, mwaka huu yalipoanza maonesho hayo mpaka Julai 10, mwaka huu, wametoa msaada wa kisheria kwa watu zaidi ya 3000 ambao wametembelea katika viwanja vya maonesho hayo.

Amesema kati ya hao waliopatiwa msaada wa kisheria, wanawake ni 1,899 na wanaume ni 1,630.

Kadhalika, amesema migogoro zaidi ya 500 imeshatatuliwa katika viwanja hivyo.

"Na mimi nimekaa pale naendelea kutatua hiyo migogoro.Tutumie fursa hii kuendelea kuwakaribisha wananchi wote wa Dar es Salaam kwamba siku zote za maonesho huduma ya msaada wa kisheria itaendelea kutolewa katika viwanja hivi."

"Mimi mwenyewe nimeshiriki kutoa msaada wa kisheria na nitaendelea kuifanya kazi hiyo katika siku zote."
 

Attachments

  • Screenshot 2025-07-16 at 13-55-31 Instagram.png
    Screenshot 2025-07-16 at 13-55-31 Instagram.png
    914.9 KB · Views: 37
Back
Top Bottom