sinafungu
JF-Expert Member
- Feb 13, 2010
- 1,527
- 865
NI Kampuni yenye jina kubwa na ni konge ktk huduma za usafirishaji hapa Nchini, mmiliki wake ni mbunge wa GAIRO na ni kiongozi anayeheshimika. Nasukumwa kuandika hili kwa matukio ya uonevu anayowafanyia WAFANYAKAZI WAKE.
Wako wengi wanafanya kazi katika kampuni hii miaka kadha lkn hawana ajira ya kudumu, wala ajira ya mikataba. Maana yake wanamfamyika kazi bila ya kuwa na mikataba ambayo kimsingi ni kwa mujibu wa sheria. Kwa maana hii kampuni hii inakwepa kodi sambamba na kuvunja sheria za nchi.
Kwa mfano ana kawaida inapotokea suala la short kwenye mahesabu ya hela, yeye huongea na mkuu wa kituo tu na wafanyakazi anaowakisia hata kama hawahusiki hukamatwa na kuwekwa ndani bila ya kufunguliwa mashitaka, na kulazimishwa kulipa hizo hela nje ya utaratibu. Wakilipa keshi inaishia hapohapo.
Juzi amekamata baadhi ya wafanyakazi wake kwa madai eti wameetengeneza hasara, walipelekwa kituo cha polisi pale Dododma Mjini, wamelala pale bila ya kufunguliwa mashitaka, huku wakilazimishwa walipe.
Hawapelekwi mahakamani kwani mwenyewe anajua akiwapeleka kule kesi itamuelemea, anawafanyisha kazi miaka kadha pasi na kuwatambua kisheria, wafanyakazi hao tangu mwezi Januar hawana mishahara.
Hivi huyu mkuu wa kampuni hii anajua kuwa kesho kuna hukumu toka kwa Mungu?