Wizara ya Kilimo imesema imekusudia kutoa ajira Milioni 3 Kwa vijana

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Serikali ya Rais Samia Suluhu kupitia Wizara ya Kilimo imesema imekusudia kutoa ajira Milioni 3 Kwa vijana na wanawake kupitia Programu ya (Building Better Tomorrow) kwa kushiriki Kilimo biashara kupitia mashamba ya pamoja (block farms).

WAZIRI wa Kilimo Husein Bashe, ametangaza majina ya vijana 812 waliochaguliwa kujiunga katika Programu ya Building Better Tomorrow, Youth initiative in Agribusiness (BBT-YIA ), huku Rais Samia Suluhu akitarajia kuzindua Shamba lenye ekari 1,000 lililopo jijijini Dodoma 20/3/2023

Vilevile Waziri wa kilimo ameongezea kuwa " Wizara tayari imekamilisha uchambuzi wa kuwapata vijana hao watakaoshiriki katika mafunzo hayo ya awamu ya kwanza , huu mchakato wakuchagua vijana unaendelea hii ni awamu ya kwanza nyingine itakuja"

Watanzania tunaendelea kuwa na imani na serikali yetu maana tunaona inaendelea kutatua changamoto yetu kubwa ya ajira vijana huu ni wakati wa kuchangamkia fursa utajiri unapatikana shambani.
 
Serikali kwa huu mpango wake inastahili pongezi, naona ni kama imeua ndege wawili kwa jiwe moja, kwanza wataajiri vijana wengi kwa wakati mmoja, lakini pia, hao vijana watakaopatiwa hayo mafunzo nao wataenda kuwa walimu wa wengine maeneo mbalimbali ya nchi yetu, kwa mtindo huu naiona sekta ya kilimo ikija kuwa mkombozi siku za mbeleni.

Suala la namna gani hao vijana watawezeshwa kugawana kile kitachopatikana kwenye shughuli hizo ili waweze kukidhi mahitaji yao, naona litakuwa suala lingine la msingi zaidi, wasije kurundikwa wengi sehemu moja, walime, wavune, halafu mwisho wa siku wakose wanunuzi wa mazao yao, au wanunuzi wapatikane kwa bei ndogo, kwasababu bado bei itategemeana na hali ya soko kwa wakati husika.
 
Kwenye mpango huu wa BBT nafasi 824 tu nchi nzima ndio zimetoka kuna wilaya zimetoa watu 20 na wengine chini
 
Serikali kwa huu mpango wake inastahili pongezi, naona ni kama imeua ndege wawili kwa jiwe moja, kwanza wataajiri vijana wengi kwa wakati mmoja, lakini pia, hao vijana watakaopatiwa hayo mafunzo nao wataenda kuwa walimu wa wengine maeneo mbalimbali ya nchi yetu, kwa mtindo huu naiona sekta ya kilimo ikija kuwa mkombozi siku za mbeleni.

Suala la namna gani hao vijana watawezeshwa kugawana kile kitachopatikana kwenye shughuli hizo ili waweze kukidhi mahitaji yao, naona litakuwa suala lingine la msingi zaidi, wasije kurundikwa wengi sehemu moja, walime, wavune, halafu mwisho wa siku wakose wanunuzi wa mazao yao, au wanunuzi wapatikane kwa bei ndogo, kwasababu bado bei itategemeana na hali ya soko kwa wakati husika.
Ni suala la muda tu wote hao watageuzwa kuwa cheap labors/tenants ma landlords ndo watakaofaidi huu mradi, iko cku hao vijana watarudi makwao bila viatu na hata nauli watatumiwa na ndugu zao kwa jinsi watakavyo chakaa
 
Serikali ya Rais Samia Suluhu kupitia Wizara ya Kilimo imesema imekusudia kutoa ajira Milioni 3 Kwa vijana na wanawake kupitia Programu ya (Building Better Tomorrow) kwa kushiriki Kilimo biashara kupitia mashamba ya pamoja (block farms).

WAZIRI wa Kilimo Husein Bashe, ametangaza majina ya vijana 812 waliochaguliwa kujiunga katika Programu ya Building Better Tomorrow, Youth initiative in Agribusiness (BBT-YIA ), huku Rais Samia Suluhu akitarajia kuzindua Shamba lenye ekari 1,000 lililopo jijijini Dodoma 20/3/2023

Vilevile Waziri wa kilimo ameongezea kuwa " Wizara tayari imekamilisha uchambuzi wa kuwapata vijana hao watakaoshiriki katika mafunzo hayo ya awamu ya kwanza , huu mchakato wakuchagua vijana unaendelea hii ni awamu ya kwanza nyingine itakuja"

Watanzania tunaendelea kuwa na imani na serikali yetu maana tunaona inaendelea kutatua changamoto yetu kubwa ya ajira vijana huu ni wakati wa kuchangamkia fursa utajiri unapatikana shambani.
VIPI KUHUSU ZANA ZA KULIMIA AU NI JEMBE LA MKONO?
 
Back
Top Bottom