KERO Responded Wizara ya Kilimo tuambieni wakulima kuwa Tanzania hakuna mbolea tujue moja ila sio kwa mateso haya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
4,994
Reaction score
9,625
Habari zenu wakuu!!!

Naiomba wizara ya kilimo kupitia mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Mbolea Tanzania, TFRA ijitokeze hadharani kuhabarisha zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania ambao shughuli zao kubwa ni kilimo kuwa mbolea haipatikani ndani ya mipaka ya Tanzania.

Wakulima tunahangaika kutafuta mbolea maeneo mbalimbali bila ya mafanikio yoyote, mazao yanadumaa mashambani kwa kukosa mbolea ( za viwandani) . Nchi hii inajinasibu kuwa sekta ya kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa ila ukitazama kwa makini utagundua kuwa mkulima ndiye mtu wa mwisho kujaliwa ndani ya Taifa hili.

Ni zaidi ya miezi 3 sasa suala la upatikanaji wa mbolea limekuwa ni kipengele na hata ukifanikiwa kusikia sehemu kuna mbolea inauzwa basi bei ya mfuko mmoja sio chini ya shilingi 120,000 za kitanzania.

Kwa hali hii mnataka wakulima waache kulima ili utokee mfumuko wa bei ya mazao na maisha yazidi kuwa magumu. Wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji wanateseka kwa gharama za uzalishaji kuwa juu...Mbolea bei juu, Petroli , Dizeli na gesi bei zake zipo juu mno.

Wito wangu kwa serikali kupitia waziri wake wa kilimo ni kuwa wajitokeze hadharani kutupa majibu yakinifu kuwa ni lini mbolea itapatikana nchini Tanzania.?

Jambo la ajabu kabisa ni kuwa mbona majirani zetu wote wana mbolea? Kampuni za mbolea kama ETG Zambia ,Kenya , Uganda n.k ina mbolea ya kutosha ila kwa Tanzania ukiuliza unaambiwa mbolea hakuna.

JAMANI VIONGOZI SIKIENI VILIO NA MACHOZI YA WAKULIMA.
BILA YA WAO KULIMA NYIE MTAKULA NINI?
Asanteni.

Pia soma ~ TFRA: Tumekamata Wafanyabiashara kwa kuuza mbolea kinyume na maelekezo ya Serikali
 
Chongolo asipoangalia ataliwa kichwa kwenye hili eneo.

Achukue hatua haraka. Haiwezekani nchi inayohubiri kilimo kuwa ni uti wa mgongo haina upatikanaji wa mbolea.

Serikali iyalipe makampuni makubwa yanayoleta mbolea hata 70% tu.

Iachanane na ukopoji unaoua biashara. Inashindwa vipi kuwa inalipa wazabuni kila mwezi kuwatia moyo.

Leo mtaani hakuna mbolea muhimu kama Urea, CAN n.k. mfumo wa ruzuku ni kama umekata moto.

TFRA nayo ni kama haina uongozi, haijielewi zaidi kujifanya polisi dhidi wauzaji wa mbolea.

Kama serikali haiwezi kusimamia ruzuku iache utaratibu huo, sisi wakulima tutanunua kwa bei ya sokoni.
 
tutanunua kwa bei ya sokoni ila nao wasiingilie kati kutupangia bei ya mazao.
 
Kwanini mkulima apangiwe bei ya kuuza mazao yake wakati kwenye masuala ya mbolea, umwagiliaji, gharama za mbegu n.k hakuna anayemjali?

Mkulima anapovuna tu watu kati wanaingilia kupanga bei ya mazao ya mkulima bila ya kujali muda na gharama ambazo mkulima amezitumia kuzalisha mazao yake.
 
Tangu walipo ingiza siasa za mbolea ya ruzuku ukiritimba (bureaucracy) ukaingia kwenye mbolea.
Ikaanza kuwa bidhaa adimu na ya magendo.
Tukaanza kuuziwa kwa kificho kwa bei aghali toka kwenye maduka yaleyale tuliyokuwa tukinunua kwa uwazi na ya kutosha kwa bei rahisi.
Haipatikani kwa wakati, unaipata tayari mazao yamedumaa.

Nimelalamika sana hapa JF kwa miaka mitatu juu ya hilo.
Hata ukifanikiwa kupata ya ruzuku basi huwezi kupata mbolea za kampuni bora mfano za kampuni ya Yara Ltd.
 
kuna ukiritimba mkubwa sana kwenye hii sekta. Unakuta mbolea haiuzwi kwa bei ya ruzuku ila mfuko wa mbolea umeandikwa ni wa Ruzuku.

Rais Magufuli wakati anaingia madarakani mfuko wa mbolea yoyote ulikuwa hauzidi 50,000 tsh. Sasa hv tunaaambiwa 120,000 tsh.
 
Ni kweli mbolea imekua adimu tangu machi,ila mie nilinunua kiwango nilichohitaji tangu February,ambapo ilikua nyingi tu
 
kuna ukiritimba mkubwa sana kwenye hii sekta. Unakuta mbolea haiuzwi kwa bei ya ruzuku ila mfuko wa mbolea umeandikwa ni wa Ruzuku.

Rais Magufuli wakati anaingia madarakani mfuko wa mbolea yoyote ulikuwa hauzidi 50,000 tsh. Sasa hv tunaaambiwa 120,000 tsh.
Magufuli aliondoa ruzuku,mbolea na mafuta vilianza kupanda bei mwishoni 2020
 
ChoiceVariable akirudi kutoka Russia atawaletea mbolea.
Habari zenu wakuu!!!

Naiomba wizara ya kilimo kupitia mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Mbolea Tanzania, TFRA ijitokeze hadharani kuhabarisha zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania ambao shughuli zao kubwa ni kilimo kuwa mbolea haipatikani ndani ya mipaka ya Tanzania.

Wakulima tunahangaika kutafuta mbolea maeneo mbalimbali bila ya mafanikio yoyote, mazao yanadumaa mashambani kwa kukosa mbolea ( za viwandani) . Nchi hii inajinasibu kuwa sekta ya kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa ila ukitazama kwa makini utagundua kuwa mkulima ndiye mtu wa mwisho kujaliwa ndani ya Taifa hili.

Ni zaidi ya miezi 3 sasa suala la upatikanaji wa mbolea limekuwa ni kipengele na hata ukifanikiwa kusikia sehemu kuna mbolea inauzwa basi bei ya mfuko mmoja sio chini ya shilingi 120,000 za kitanzania.

Kwa hali hii mnataka wakulima waache kulima ili utokee mfumuko wa bei ya mazao na maisha yazidi kuwa magumu. Wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji wanateseka kwa gharama za uzalishaji kuwa juu...Mbolea bei juu, Petroli , Dizeli na gesi bei zake zipo juu mno.

Wito wangu kwa serikali kupitia waziri wake wa kilimo ni kuwa wajitokeze hadharani kutupa majibu yakinifu kuwa ni lini mbolea itapatikana nchini Tanzania.?

Jambo la ajabu kabisa ni kuwa mbona majirani zetu wote wana mbolea? Kampuni za mbolea kama ETG Zambia ,Kenya , Uganda n.k ina mbolea ya kutosha ila kwa Tanzania ukiuliza unaambiwa mbolea hakuna.

JAMANI VIONGOZI SIKIENI VILIO NA MACHOZI YA WAKULIMA.

BILA YA WAO KULIMA NYIE MTAKULA NINI?

Asanteni.
Kwa taarifa Yako tuu Serikali Kwa Sasa Ina kiburi Kwa sababu uzalishaji wa mazao imeongezeka mara dufu.

Mathalani mazao ya msimu wa 2025/26 yamejaa hakuna Kwa kupeleka kuanzia maghala ya serikali Hadi watu binafsi.

Pili msimu huu wa 2026/27 ndio kabisaa mvua zimenyesha Nchi nzima Kila zao lipo ndio maana mazao yoote ya chakula bei zimeporomoka.

Kwa muktadha huo Serikali imeondoa ruzuku kwenye aina nyingi sana za mbolea hususani za Yara na kubakiza kampuni chache za mbolea za hovyo za ndani kama Minjingu na Fomi (Intracom) na chache sana za DAP na Urea.

Kutokana na hivyo na kwamba agro dealers Wana dai madeni kibao hakuna kiwanda kinazalisha mbolea ya ruzuku wakati hawajalipwa Kwa hiyo mbolea ambazo Hazina ruzuku Zenye bei kubwa ndio ziko sokoni ni Juu Yako wewe mkulima ununue au uache.

Mwisho kabisa Nchi zoote ambazo unazijua wewe zilikuwa soko la Tanzania zimezalisha Kwa kiwango kikubwa hasa mazao ya Nafaka kuanzia South Africa Hadi Kenya,so hakuna soko zaidi ya soko la ndani.

Mimi binafsi ni mkulima Hadi saizi Sina Kwa kupeleka mahindi yangu ,bei ni za kutupa na wanunuzi hawapo.Msimu ujao nimeamua kuachana kabisa na mahindi nitalima ulezi Mashamba yangu yote Kwa sababu gharama zake ni nafuu na huenda bei ikawa afadhari kuliko mahindi.
 
Acha porojo zako,
Kama uzalishaji wa mazao umeongezeka mara dufu kwa nini bei za vyakula zinazidi kuongezeka badala ya kushuka??
 
Mambo kama mbolea,mbegu Bora,matrekta yalipaswa usiwe issue hata ya kuwaza!Wizara ya kilimo ingekuwa inahimiza wakulima hata kwa mikopo.
 
Habari zenu wakuu!!!

Naiomba wizara ya kilimo kupitia mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Mbolea Tanzania, TFRA ijitokeze hadharani kuhabarisha zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania ambao shughuli zao kubwa ni kilimo kuwa mbolea haipatikani ndani ya mipaka ya Tanzania.

Wakulima tunahangaika kutafuta mbolea maeneo mbalimbali bila ya mafanikio yoyote, mazao yanadumaa mashambani kwa kukosa mbolea ( za viwandani) . Nchi hii inajinasibu kuwa sekta ya kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa ila ukitazama kwa makini utagundua kuwa mkulima ndiye mtu wa mwisho kujaliwa ndani ya Taifa hili.

Ni zaidi ya miezi 3 sasa suala la upatikanaji wa mbolea limekuwa ni kipengele na hata ukifanikiwa kusikia sehemu kuna mbolea inauzwa basi bei ya mfuko mmoja sio chini ya shilingi 120,000 za kitanzania.

Kwa hali hii mnataka wakulima waache kulima ili utokee mfumuko wa bei ya mazao na maisha yazidi kuwa magumu. Wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji wanateseka kwa gharama za uzalishaji kuwa juu...Mbolea bei juu, Petroli , Dizeli na gesi bei zake zipo juu mno.

Wito wangu kwa serikali kupitia waziri wake wa kilimo ni kuwa wajitokeze hadharani kutupa majibu yakinifu kuwa ni lini mbolea itapatikana nchini Tanzania.?

Jambo la ajabu kabisa ni kuwa mbona majirani zetu wote wana mbolea? Kampuni za mbolea kama ETG Zambia ,Kenya , Uganda n.k ina mbolea ya kutosha ila kwa Tanzania ukiuliza unaambiwa mbolea hakuna.

JAMANI VIONGOZI SIKIENI VILIO NA MACHOZI YA WAKULIMA.

BILA YA WAO KULIMA NYIE MTAKULA NINI?

Asanteni.
Mkuu mnalalamika sana kwasababu tu ya ushungi wa mama. Vita dhidi ya Iran vimeathiri duniani kote. Kikubwa fanyeni kazi.

gallow bird ChoiceVariable (Dogo my take) Jagina mdogoee

adriz de mbusii
 
Magufuli aliondoa ruzuku,mbolea na mafuta vilianza kupanda bei mwishoni 2020
Lakini ilipatikana kwa uhakika madukani wakati wote tena kila aina ya mbolea.
Pesa yako tu.
Sasa hata uwe na pesa kuna wakati haipatikani madukani.

Wakati wa Kikwete pia mbolea ilikuwa inapatika kwa uhakika kila wakati kwa bei nafuu. Ile kweli ilikuwa 'kilimo kwanza'.
 
Back
Top Bottom