Habari zenu wakuu!!!
Naiomba wizara ya kilimo kupitia mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Mbolea Tanzania, TFRA ijitokeze hadharani kuhabarisha zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania ambao shughuli zao kubwa ni kilimo kuwa mbolea haipatikani ndani ya mipaka ya Tanzania.
Wakulima tunahangaika kutafuta mbolea maeneo mbalimbali bila ya mafanikio yoyote, mazao yanadumaa mashambani kwa kukosa mbolea ( za viwandani) . Nchi hii inajinasibu kuwa sekta ya kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa ila ukitazama kwa makini utagundua kuwa mkulima ndiye mtu wa mwisho kujaliwa ndani ya Taifa hili.
Ni zaidi ya miezi 3 sasa suala la upatikanaji wa mbolea limekuwa ni kipengele na hata ukifanikiwa kusikia sehemu kuna mbolea inauzwa basi bei ya mfuko mmoja sio chini ya shilingi 120,000 za kitanzania.
Kwa hali hii mnataka wakulima waache kulima ili utokee mfumuko wa bei ya mazao na maisha yazidi kuwa magumu. Wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji wanateseka kwa gharama za uzalishaji kuwa juu...Mbolea bei juu, Petroli , Dizeli na gesi bei zake zipo juu mno.
Wito wangu kwa serikali kupitia waziri wake wa kilimo ni kuwa wajitokeze hadharani kutupa majibu yakinifu kuwa ni lini mbolea itapatikana nchini Tanzania.?
Jambo la ajabu kabisa ni kuwa mbona majirani zetu wote wana mbolea? Kampuni za mbolea kama ETG Zambia ,Kenya , Uganda n.k ina mbolea ya kutosha ila kwa Tanzania ukiuliza unaambiwa mbolea hakuna.
JAMANI VIONGOZI SIKIENI VILIO NA MACHOZI YA WAKULIMA.
BILA YA WAO KULIMA NYIE MTAKULA NINI?
Asanteni.