Wizara ya Maji yaomba Bajeti ya Bilioni 756

Wizara ya Maji yaomba Bajeti ya Bilioni 756

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WIZARA YA MAJI YAOMBA BAJETI YA BILIONI 756

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso akisoma hoja ya bajeti Bungeni amesema Wizara ya Maji imeliomba Bunge liidhinishe jumla ya Shilingi 756,205,106,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2023/24.

Akizungumza Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya maji kwa mwaka 2023/24 Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema kuwa Kati ya fedha hizo, Matumizi ya Kawaida ni Shilingi 60,375,474,000 ambapo Shilingi 18,035,561,000 sawa na asilimia 29.87 ni kwa ajili ya kugharamia Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 42,339,913,000 sawa na asilimia 70.13 ni kwa ajili ya kulipa Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara, RUWASA na Chuo cha Maji.

Aidha, Mhe. Aweso amesema Jumla ya bajeti ya maendeleo ni Shilingi 695,829,632,000 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 407,064,860,000 sawa na asilimia 58.50 ni fedha za ndani na Shilingi 288,764,772,000 sawa na asilimia 41.50 ni fedha za nje

Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mijini imeongezeka kutoka wastani wa asilimia 86.5 Desemba, 2021 hadi wastani wa asilimia 88 Desemba, 2022.” – Jumaa Aweso, Waziri wa Maji

Miradi 586 iliyokamilika ipo katika vijiji 1,293 vyenye jumla ya vituo 5,748 na inahudumia wananchi 4,086,442. Upatikanaji wa Huduma ya Maji Vijijini Umeongezeka kutoka 74.5% mwaka 2021 hadi 77% mwaka 2022 na Idadi ya wananchi wanaopata huduma imeongezeka hadi kufikia 30,209,409.

"Upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama vijijini umeimarika kutoka asilimia 70.1 mwaka 2020 hadi asilimia 77 mwaka 2022 na Kutoka asilimia 84 mwaka 2020 hadi asilimia 88 mwaka, 2022 maeneo ya mijini."

Kuhusu Huduma za Usambazaji wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mijini Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema Wizara imeweka historia, amesema Mwaka 2022/23, miradi 175 ilipangwa kutekelezwa ambapo hadi mwezi Aprili 2023, miradi 40 imekamilika na miradi 135 inaendelea

Waziri Jumaa Aweso ameeleza hayo leo Bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

FvwVlVqWYAALTEr.jpg
 
Back
Top Bottom