Uchaguzi 2020 Wizara ya Mambo ya Ndani yawataka Viongozi wa Dini kutofanya kampeni

Uchaguzi 2020 Wizara ya Mambo ya Ndani yawataka Viongozi wa Dini kutofanya kampeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja

Wizara imesema jumuiya za kijamii na taasisi za dini husajiliwa na Wizara ya Mambo ya ndani kwa mujibu wa Sura ya 337 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 3 ya mwaka 2019

Wizara imesema kiongozi wa dini kutoa maelekezo kwa waumini juu ya mgombea wa kumchagua ni kinyume na kifungu cha 17(c) cha Sheria ya Jumuiya

Wizara imewataka viongozi wa dini wazingatie sheria za Jumuiya ambayo inakataza viongozi wa kidini kujihusisha na vitendo hivyo, kwa kuwa vinaingilia uhuru wa kikatiba wa kila mtu kumchugua mgombea anayemtaka.

1603348026777.png
 
Yani cha ajabu matamko hutolewa pale tu wapinzani wakifanya jambo. BAKWATA usiku na mchana inahamasisha watu wachague CCM hilo halikuwa kosa na maisha yaliendelea kama kawaida. Kwa vile Ponda kapanda jukwaa la upinzani basi ghafla sheria imechukuwa mkondo wake.
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja...
Ila matatizo mengine serkali inayatengeneza,nikwanini wanawaita viongozi wa dini kwenye majukwaa ya kampeni?

Mbona bungeni kuna dua maalum kila siku kukiwa na vikao vya bunge lakini hakuna shehe wala padri anayeomba dua hizo kwenye chombo hicho nyeti.

Acheni kutengeneza matatizo halafu yakawasumbua kuyatatua
 
I

Hapo sasa, kwanza wanaombea wanasiasa kwenye mikutano, bungeni ni sehemu ya siasa. Dini na siasa ni part and parcel kwasababu zote zinahusu mustakabari wa maisha ya binadamu.
Kishindo cha shehe Ponda kimetikisa haswa
 
Huyo Simbachawene kaandika hiyo barua kama nani...
Kaandika kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Mawaziri bado wapo tuu mpaka siku Rais atakapojisikia kuvunja Baraza lake. Tena anaweza kuwaacha hawa waendelee kupiga hela za mwisho mpaka siku Rais mpya akiapishwa.

Hivi hiyo Sheria anayoirefer Waziri inasemaje kuhusu wale viongozi wa dini (Kama yule Gwajima/Rashid) walioamua kugombea Ubunge kabisa?
 
Viongozi wa dini waliitisha kongamano na mgeni akawa waziri mkuu,lengo la kongamano ni azimio lao la kumuunga mkono JPM katika uchaguzi mkuu huu!
Hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya jambo hilo na ilikuwa halali kabisa!
Mara kwa mara tumewaona viongozi wa dini wakiipigia chepuo CCM!Hakuna aliyefungua mdomo!
Shekhe Ponda kapanda jukwaani mara moja,naona wanamjia juu kama nyuki!

Hapa ndio tunasema hakuna haki na usawa katika utekelezwaji wa sheria!
 
Kama nihi
Hapo sasa, kwanza wanaombea wanasiasa kwenye mikutano, bungeni ni sehemu ya siasa. Dini na siasa ni part and parcel kwasababu zote zinahusu mustakabari wa maisha ya binadamu.
Kishindo cha shehe Ponda kimetikisa haswa
Kama nihivyo hata bungeni kuwe na zamu za viongozi waongoza sala au dua kama vile waislamu,wakristo,wapagani nk
Hahahaaa hapo sipati picha
 
Chadema mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
 
Wakati wanaomba dua baadhi ya viongozi hao wa dini wanafanya kampeni kwenye dua zao. Nadhani nimeeleweka
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja..

Yaani ilitakiwa watumishi wote wa mungu wasiwe hata kwenye majukwaa wala kwenye vipindi vyovyote vya TV kuongea mambo yoyote ya siasa

Hili tamko limekuja kwa sababu ya Shekhe Ponda tu

Hapo kabla mbona hakukuwa na barua za katazo kama hili
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja..
Mzee Ponda na Bagonza Keisha habari yao! Viongozi wasimamie viapo au kama vipi wavue kora wavae magandwa, sio kujificha nyuma ya migongo ya madhabahu!
 
Back
Top Bottom