Uchaguzi 2020 Wizara ya Mambo ya Ndani yawataka Viongozi wa Dini kutofanya kampeni

Uchaguzi 2020 Wizara ya Mambo ya Ndani yawataka Viongozi wa Dini kutofanya kampeni

Duu, tatizo hii serikali haielewi wapi pa kusimama,, mambo yakifanyika upande wao hata kama ni kinyume cha sheria wanayanyamazia, jambo hilo hilo likifanyika upande wa pili ni kosa, hii haiwezi kukubalika kwa kwa watu wenye akili. Yaani wangekuwa serious Gwajima asingepewa fomu ya kugombea cheo cha kisiasa (ubunge).
 
Chadema mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Naona na nyie mmenda kuomba kura huku
images.jpeg.jpg
 
Mzee Ponda na Bagonza Keisha habari yao! Viongozi wasimamie viapo au kama vipi wavue kora wavae magandwa, sio kujificha nyuma ya migongo ya madhabahu!

Hahahaha kwa chadema tu, ila kwenu nyie ccm ni poa kabisa
 
Yan ilitakiwa watumishi wote wa mungu wasiwe hata kwenye majukwaa wala kwenye vipindi vyovyote vya TV kuongea mambo yoyote ya siasa

Hili tamko limekuja kwa sababu ya Shekhe ponda tu

Hapo kabla mbona hakukuwa na barua za katazo kama hili
Mbona Gwajima anagombea siyo kiongozi wa dini?
 
Mambo yamekuwa magumu eee. CCM poo nyingine hiyo!! Sheikh Ponda kashawapiga bao la kisigino....too late... uamuzi ushafanyika tayari waislamu tunaojitambua na tunaolilia HAKI zetu miaka nenda rudi tunakwenda na Tundu Antipas Lissu.
 
Aanze kwanza kumzuia Askofi Dr Rashid Josephat Gwajima kujihusisha na mambo ya siasa
 
Kwanini hili linakuja baada ya Shekh Ponda kuanza kumsuport Lissu?

CCM ndiye kivuruge wa yote, alafu wakiona wameanza kuelemewa, haraka sana wajenga mazingira ya kujinusuru!

Wamejuwa Ponda akipita na Lissu Pwani, akamalizia Dar, hawatapona! Basi wamekimbilia kuomba msaada wizara yenye dhamana!
Huwa najiuliza hivi siku CHADEMA watakapoingia madarakani na kuanza kuishi na CCM kama jinsi CCM inavyoishi nao sasa, hivi watakimbilia wapi?
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja..
Kuingilia kati kwa Wizara katika suala hili ni sahihi kabisa. Wizara ingekuwa imetoa onyo hilo mapema zaidi. Ikumbukwe kwamba waumini wanaunga mkono vyama tofauti.

Utakuwa unawaweka njia panda wale ambao wanaunga mkono mwanasiasa tofauti na yule unayemhubiria wewe. Hivyo bora kiongozi wa dini ajikite kwenye kuhubiria dini tu ingawa yeye binafsi anabakia na maono yake kuhusu nani atampigia kura.

Hiyo ibakie siri yake ili asiwakwaze waumini wake wenye maono tofauti.
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja...
Kuna neno HAKI huwa linarukwa sana kutajwa wanapo ongelea amani na upendo sijui kwanini halitajwi wakati nalo ni muhimu.
 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja...
Hii leo? Ilikuwa wapi siku zote walipokuwa wanatupigia debe CCM? Mkuki mtamu kwa ngurue; kwa binadamu mchungu
 
Bishop Gamanywa, bishop Gwajima na sheikh mkuu wa Dar walikwisha toa maelezo kwa waumini wao wala hamkukemea
Ponda Isa Ponda kaibuka juzi tu ndipo mkaleta huo waraka, pole zenu mmechelewa sana kutoa onyo
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaasa viongozi wa kidini kutojihusisha na kampeni za kisiasa kwa kuwaambia waumini wao kuhusu viongozi wa kuwachagua bali wabaki kuhubiri amani, upendo na umoja...
 
Back
Top Bottom