Uchaguzi 2020 Wizara ya Mambo ya Ndani yawataka Viongozi wa Dini kutofanya kampeni

Huyu Simbachawene sijui amekula maharagwe ya wapi. Shehe wa Dar alimpigia kampeni Magufuli hadharani hakuona, viongozi wa dini wamekusanywa Dodoma na CCM kumuombea Magufuli hakuona, viongozi wamekuwa wakifanywa dua chini ya udhamini wa CCM na Majaliwa haoni!

Baada ya Shehe Ponda kuingia kazini Simbachawene anatoka mafichoni kama amevamiwa na nyuki!
 
Yule anayejiita Rashid kule Kawe mbona kaingia mzima mzima anagombea na ubunge, au yeye hafanyi kampeni ama siyo askofu siku hizi, kuweni serious..
 
Simbachawene acha kutuhadaa. Watanzania wanajua sana. Suala la viongozi wa dini kupanda majukwaani na kuomba kura kwa mgomeba fulani si kosa kisheria. Suala hili liachwe kwa mamlaka ya dhehebu husika kuhusu viongozi wake kufanya au kutofanya kampeni.
 
Naona hii hali inatengenezwa nchini. Wenye maamuzi ya watanzania wasifike huko ni Tume ya uchaguzi kutenda haki tu...
 
Tena naona yule shehe ambaye anahubiri mambo ya Muhamadi na Yesu kwa pamoja wamuite akajieleze.

Amechanganya hata baadhi ya waumini.
Yule ana hadhi moja na musiba,bashite heri James ktk nchi hii hata siro mahera hawezi wagusa Hawa watashinda njaa.
 
Hivi BAKWATA ni chama cha siasa sio??
Bakwata iliasisiwa na ccm lengo kuu ni kuwanyamazisha waislamu wasidai haki zao.
Thus haijawahi shutumu juu ya manyanyaso ya waislamu zikiwemo teuzi, kukamatwa kwa waislamu
 
Siku wakiondolewa madarakani, watafute pa kujificha
 
Mzee Ponda na Bagonza Keisha habari yao! Viongozi wasimamie viapo au kama vipi wavue kora wavae magandwa, sio kujificha nyuma ya migongo ya madhabahu!
Hawa je
 

Attachments

  • Screenshot_20201021_133440.jpg
    91.1 KB · Views: 2
Chadema mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu atapigiwa kura na robert tu
Nakushauri kwa faida yako ya siku za mbeleni kuwa tafuta chuo kinachofundisha propaganda hata kwa njia ya mtandao ukasome upate ujuzi wa kufanya propaganda!
Hili unachokifanya sio propaganda Bali ni person attack kwa uliyemlenga na siku akikupatia nafasi ya kukushughulikia utaiona siasa chungu! Kama anakukera mtafute umwambie ana kwa ana! Mr.polepole propaganda ulisomea chuo kipi? Unafeli Sana ndugu!
 
Rashid Gwajima alijiuzulu nafasi Yake like kwenye kabisa lake? Kila jumapili anaongoza ibada siyo? Wizara inaweza kutuhakikishia kuwa katika mahubiri take hapigi kampeni? Na hili siyo kosa kwa mujibu wa Sheria hiyo?
 
Usaliti ni laana ? Huko Chadema huwa mnashughulikiana?
 
waswahili daima husema mdharau mwiba humchoma. Daima kila alalae huamka. Tuombe uhai tu tuje kuwa mashahidi watu wakiamka.
 
Hii barua haina tofauti na toilet paper! Mmeshachelewa Sheikh Ponda keshatoa maelekezo kilichobaki tarehe 28/10/2020 natekeleza maelekezo yake. Kula yangu na familia yangu ni kwa lissu
 
..Simbachawene ni mgombea ktk uchaguzi huu.

..angekuwa na busara angemuachia Katibu Mkuu wa Wizara atoe taarifa hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…