Wizara ya Mazingira fanyeni kazi yenu sawa sawa nchi inageuka Jalala kwa kasi

Nchi yetu kwa ujumla wake ni chafu, unatembea mtaa mzima hakuna sehemu ya kuweka taka unategemea nini? Nitembee na chupa tupu ya maji wakati nilishamaliza kunywa?

Kifupi hata wewe ukipewa madaraka au nafasi ya kuongoza, unless uwe na uthubutu wa yule mwamba, otherwise ni yale yale tu.
 
Yaani jinsi serikali hii inavyofeli katika kumanage vitu basic kama hivi, hapo ndo ujue kuwa kamwe hawewezi kumanage vitu vikubwa, na complex vya kitaifa vya maendeleo ya kiuchumi!
 
Tatizo kubwa LA nchi hii Ni UPIGAJI na TAMAA.

Kazi ya Usimamizi wa masuala ya USAFI wa MAZINGIRA na usimamizi wa sheria za mazingira ulikuwa unafanyika vizuri sana chini ya Halmashauri kupitia Maafisa Afya Mazingira ( Bwana na Bibi Afya ).

Baadaye, ilivyokuja kuonekana Luna pesa za ushuru wa taka na fine, kikatengenezwa Kitengo ndani ya Halmashauri chini ya DED kinaitwa Mazingira na Taka ngumu wakati huo huo, hawa Maafisa Afya wao wako chini ya Idara ya Afya.

Kitengo cha Mazingira wakawepo watu wa Mazingira ambao hawana man power mitaani.

Na to make things worse, pesa za taka zenyewe zinaenda kwenye majukumu mengine ikiwemo kulipa posho madiwani.

Yaani nchi hii ukifikiria unaweza kudhani hakuna MTU mwenye akili kabisa.
 

Attachments

  • Screenshot_20221009-103030.png
    64 KB · Views: 5
Umejibu vema ila sentence zako mbili za mwisho zime wind me down, yes ni wajibu wa Halmashauri kuweka hizi bins kwa kila nyumba na mitaani, nakumbuka Mr.Mrema (rip)alijaribu hili ila matokeo yake yakawa ovyo, zile takataka hazikuzolewa kwa wakati
 
Mzee uzi nau support bahati mbaya sina aatachment ( picha) ila kama kuna mtu amepita pale stand ya NZEGA atakuwa shahidi ..yaani stand imetawaliwa na vi plastik vilivyo zagaa eneo la stand and NO BODY CARES

Hii component ya mazingira ni kama tunajifanyaga hatuijui..ata ukienda ktk halmashauri zetu ipo idara ya mazingira lkn haieleweki mara iitwe afya na mazingira mara misitu na nyuki
 
Wanahangaika kwenda nje kutangaza utalii lakini nchi yenyewe chafuuu.

Matokeo yake hata hao watalii wakija wanatuona kituko na mauchafuuchafu yetu!
 
Ili kuondoa uchafu mmoja wapo ni wafanyao biashara kando ya barabara na kwenye miundombinu ya barabara kuondolewa.
Wakiondolewa hao, wanasiasa wataleta siasa
 
Kuna mji unaitwa bwanga uko chato,mji mchafu ule sijawahi kuona,mji wote unanuka mikojo,vinyesi na maji machafu yanayotiririka
 
Duh! Kweli ccm haitufai kabisa
 
Hilo namba 1 ni uongo mbona huku kwetu sioni hiyo mifuko?

Mengine ni sawa kabisa ila nakushangaa unaacha masuala muhimu yanayoharibu vyanzo vya maji na misitu nacho ni ufugaji wa kienyeji wa kuhama hama..

Mwisho Serikali imebuni mkaa mbadala wa Makaa ya Mawe lakini hakuna anaesisitiza matumizi ya huo mkaa uzalishwe mwingi na kuzuia kukata miti.
 
Mada nzuri Sana kaka.uchafu wa miji yetu unareflect hatuna viongozi kabisaa nchi inajiongoza.
 
Wabongo tumeshindwa kujisimamia hadi katika usafi wetu! Iko shida mahali.
Inasikitisha sana.
 
Atufigwegwe god 😄😄
 
Hiyo ni attitude ya watu, sio serikali.
Serikali kuu ikusimamie hadi utupaji wa taka?

Watu wa mtaa husika kama mnajielewa mnajiwekea utaratibu na kuhakikisha unafuatwa tu, sio Waziri

Hiyo wizara ina staff wangapi hadi waje kusimamia kila mtaa!
Watanzania sio wastaarabu kiasili huu ndo ukweli mchungu na sababu nyingine kutokuwepo kwa upangaji miji inakua ni ngumu sana kudeal na takataka in short dar es salaam ni mji mchafu sana

Kuna migahawa mingi hata choo haina
 
Wabongo tumeshindwa kujisimamia hadi katika usafi wetu! Iko shida mahali.
Inasikitisha sana.
Kuna miaka flani nilikua nimepanga hadi kuosha choo watu wanataka waekew ratiba na kukumbushwa kama watoto ustaarabu bado sana kwa Tanzania
 
Serikali inahitaji kufanya utafiti how Rwanda wameweza. Kigali ni safi kuliko hata baadhi ya miji mikubwa ya ulaya. Pili uchafu ni mindset .umuhimu wa kusafisha mazingira ufundishwe kuanzia elementary schools.kuna nchi huwezi tupa takataka mtoto wa miaka minne akakuacha its just civilization issue .mamlaka zichukue hatua maendeleo yanakuwa defined na mambo mengi la sivyo kuweka ma structure kwenye mi watu michafu haina maana .viongozi fanyeni hata tour hapo Rwanda mkajifunze .ni aibu
 
Nimesoma Ila sijaelewa
Huwezi elewa mada za namna hii mtu wa kaliba yako uliekulia tandale!! Mnakula sebleni huku mbele ya kibaraza chenu kuna mtu anaoga maji machafu yanatiririkia kwenu... ukiingia chumbani kwenu dirisha linatizamana na jalala la jirani yenu... kando kidogo ya kwenu kuna madimbwi ya maji yaliyojaa uchafu unaonuka na condoms zilizotumika kwenye ma guest houses.... kwa hali hii utaelewa vipi mada hii?
 
Serikali itoe amri ya kufanya usafi siku moja kwa saa nane Kila mtu. Inaweza kuwa ijumaa ili siku nyingine watu wafanye kazi. Pia makampuni yanayozalisha uchafu wa plastic wasipewe kibali bila kuweka mpango wao wa kupunguza uchafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…