Wizara ya Mifugo ichunguze. Vijana wa viatamizi waliomaliza Mafunzo wanatupwa maporini utafikiri wao ndo wananenepeshwa na siyo ngombe

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,153
Reaction score
3,800
Kuna uwezekano Mama yetu Samia anahujumiwa. Serikali ichunguze wasimamizi wa Mradi wa vijana BBT- Mifugo.

Kuna haya mambo yanayotia kinyaa;

1. Vijana waliahidiwa kukaa mwaka mmoja kambini wakipata mafunzo ya unenepeshaji mifugo. Kinyume, wamekaa mwaka mmoja na nusu kwa mahangaiko yasiyo ya lazima.

2. Waliahidiwa kila mmoja kunenepesha ngombe 10 kwa kila mmoja kwa awamu zaidi ya 3 kwa mwaka. Hilo halikufanikiwa, wameishia awamu moja au mbili zenye kutia hasara au faida kiduchu isivyotarajiwa.

3. Waliahidiwa na kwa mikataba kuwa faida ambayo ingepatikana kwa mauzo ya ngombe watakaowanenepesha ingekuwa ya kwao. Kwa maana kuwa kila mmoja angeingiziwa faida ile kwenye akaunti zao binafsi kama mtaji wa kuanzia watakapomaliza mafunzo. Ni hali ya kusikitisha,hadi wanamaliza mafunzo, hakuna aliyewekewa hata senti. Wanapigwa sound. Wengi wamekata tamaa kufuatilia, na haijulikani watapewa lini.

4. Kubwa na la ajabu zaidi, bila maandalizi yoyote ya maana, wameondolewa makambini na kumwagwa kwenye mapori ya mashamba ya NARCO ambako kwa wasiojua ni maeneo yasiyo na huduma bora za msingi za kibinadamu. Sehemu nyingi hazina maji, huduma za afya, usalama mdogo nk. Ikumbukwe hawa vijana wamepelekwa bila kulipwa chochote kwa ajili ya kujikimu. Na kama wamepewa, siyo linganifu na gharama ambazo watatumia kujiandaa kabla ya kuanza biashara ya unenepeshaji.

5. Serikali ifanye uchunguzi wa aina ya mikataba waliyopewa vijana hawa, haina uhalisia wa wanachoenda kufanya kwenye mapori hayo. Hasa kiwango cha fedha wanachohitaji na wanachoenda kukopeshwa na mabenki. Swali la kujiuliza ni kuwa,endapo walikaa mwaka na nusu chini ya Uangalizi wa karibu Wizara ya Mifugo iliyobuni Mradi huo na wakashindwa kupata faida ghafi ukilinganisha na gharama zilizotumika(ushahidi upo, vituo vingi havikupata faida iliyotarajiwa kulingana na muda walioutumia), vipi wakiwa wenyewe na kwenye mazingira yasiyoboreshwa kama Makambi au Vituo walivyotoka?

Lengo na nia yangu ni kuona Miradi hii ya Kimkakati ya Mama yetu Rais Samia haikwamishwi na maharamia. Ni jukumu letu sote kumsaidia pale tunapoona inafaa kufanya hivyo.

Mwisho, Vijana ndo nguzo muhimu ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi nchini. Wakiwezeshwa vizuri wataweza.
 
Vijana wa CCM lazima wawe na ujasiri wa kuishi na nyoka porini, huko kunawafaa kujijengea huo ukakamavu.
 
Acha majungu. Umesoma hiyo mikataba au umekurupuka tu. Fanya kazi acha fitina miaka inaenda wenzio badaye watakuwa na mashamba Yao ya mifugo uanze kuwaonea wivu. Aibu kubwa
 
Wewe umeisoma? Au unaandaka usichokijua?
 
Acha majungu. Umesoma hiyo mikataba au umekurupuka tu. Fanya kazi acha fitina miaka inaenda wenzio badaye watakuwa na mashamba Yao ya mifugo uanze kuwaonea wivu. Aibu kubwa
 
Picha ya hao vijana wakiwa wametupwa porini.
 
Mbona unajibu tofauti nimeuliza picha Iko wapi??
 
Back
Top Bottom