Wizara ya Mifugo na Uvuvi na SUA Kutekeleza Maagizo ya Rais Samia

Wizara ya Mifugo na Uvuvi na SUA Kutekeleza Maagizo ya Rais Samia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WIZARA YA MIFUGO & UVUVI, SUA ZATEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA

Kufuatia maelekezo aliyoyatoa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ishirikiane na Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kuwawezesha vijana kujiajiri yaanza kutekelezwa baada ya pande hizo mbili kusaini makubaliano ya ushirikiano kuinua sekta za mifugo na Uvuvi.

Akiongea muda mfupi baada ya kushuhudia tukio la kusaini makubaliano lililofanyika mkoani Morogoro katika Siku ya Kumbukizi ya 18 ya Hayati Edward Moringe Sokoine Mei 23, 2023, Waziri wa Mifugo na Uvuvi alisema tukio hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais, Dkt Samia aliyotoa katika kilele cha Maadhimisho ya NaneNane yaliyofanyika Mkoani Mbeya Agosti 8, 2022.

Alisema kuwa Dkt Samia anataka kuona mabadiliko katika sekta za uzalishaji, hivyo fursa zilizopo katika sekta za uzalishaji zikitumika vizuri manufaa makubwa yatapatikana ikiwemo kulia kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja.

Aidha, Waziri Ulega alimshukuru, Rais, Dkt. Samia kwa jitihada zake za kuhamasisha vijana na wanawake kushiriki kwenye kilimo kupitia progamu mbalimbali.

Alisema kuwa Mifugo na Uvuvi ni utajiri kwa sababu matokeo yake ni ya haraka na biashara yake ni ya haraka pia.

Pia, alitoe wito kwa sekta binafsi na washirika wa maendeleo kuendelea kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo ili vijana waweze kushiriki katika shughuli za uzalishaji kupitia nyanja za kilimo, mifugo na uvuvi.

"Nitoe rai kwa Wadau wa sekta Binafsi na Wadau wa maendeleo kuunga mkono jitihada za Mhe, Rais kwa kutoa mitaji ya fedha, vitendea kazi, mafunzo, na teknolojia
zitakazowezesha vijana kushiriki katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa tija na ufanisi zaidi", alisema.

WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.35(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.35(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.36(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.37.jpeg
WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.37(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-05-24 at 18.17.37(2).jpeg
 
Tumechoshwa na mikataba utekelezaj. Zero
 
SUA ni sleeping giant, yaani wataalamu wao hawajitambui kabisa......wanachokijia.. ni kufundisha kama ilivyoandikwa kwenye vitabu tu............i wish wangenda ku learn kwa Egerton University kenya....Miaka nenda rudi SUA ni blablaa tu....

i wish ningekuwa na na namna ya kuwaamsha
 
Back
Top Bottom