Wizara yakemea adhabu kwa wanafunzi nchini

Wizara yakemea adhabu kwa wanafunzi nchini

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Akifungua mkutano wa Tisa wa Maafisa Elimu Mikoa na Halmashauri nchini unaofanyika jijini Mwanza, Kamishna wa elimu nchini Dkt. Lyabwene Mtahabwa amewataka walimu kutoa adhabu ambazo hazitaleta madhara kwa wanafunzi.

Kamishna Dkt. Mtahabwa amewataka walimu nchini kuacha kutoa adhabu kali kwa wanafunzi na badala yake kuongeza juhudi kwa kutumia mbinu mbadala za ufundishaji kwa wanafunzi zitakazowaongezea weledi wanafunzi.

Nini maoni yako juu ya hatua hii mwanajamvi?
 
Watoto wa siku hizi ni tofauti sana na wa zamani,wamejaa ukorofi,ujuaji,utindio wa ubongo.Hawa watoa maagizo wawe wanajipa japo muda kidogo kutembelea mashuleni waone hali halisi ilivyo.

Hatupendi kabisa kuchapa ila kunamuda watoto wanakupanda kichwani unajikuta umetoa maamuzi ambayo baadae unabaki unawaza kama ni wewe ndiye uliyefikia hatua hiyo.NB,miundombinu iongezwe,mishahara,na waajiriwe waalimu wa kutosha.
 
Tatizo ni maneno tu hakuna sheria
Wenzetu wakiamua kitu huwa wanalijadili na kuamua na sio kutoka na kutoa rai au maombi

Kinachotakiwa ni sheria sio bla bla
 
Back
Top Bottom