Wizara yetu ya michezo iache kukaa kisiasa

Wizara yetu ya michezo iache kukaa kisiasa

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Posts
2,180
Reaction score
1,291
hii wizara ndiyo baba wa wa kuleta furaha kitaifa. Kwa mtaji huu wa furaha ili utunufaishe lazima TFF na Chama cha riadha viwekewe malengo na hayo malengo yafuatiliwe. nashangaa sana sijaona waziri wa michezo akihoji hadharani kwa nini TFF haileti makocha bora wa kueleweka kuinoa timu ya taifa.

Ilifikia mahala TFF ilimchukua kocha mrundi aliyetemwa na AZAM eti akafundishe timu yetu ya taifa. Hivi kweli waziri wa michezo alishindwa kuingilia uteuzi huo na kuwaonya TFF wasiwe wababaishaji katika swala zima za ufundi ? Yanga ili kucheza makundi mwaka huu imewekeza sana kuanzia kuajili makocha na kutafuta wachezaji.

TFF pamoja na ruzuku nzuri ya FIFa inashindwa hata kumleta kocha mstaafu Philipe scolali kutoka Brazil ainoe timu yetu? huyu kocha hatakuwa wa gharama kubwa ukitilia maanani kasha staafu kufundisha soka timu kubwa kubwa za ulaya na china. yeye kuja Tanzania itakuwa kama kufundisha tution kwa mwalimu wa shule ya msingi aliyeisha staafu juzi! wizara nyanyua simu leo leo uongee na Filipe Scolari.

Ukija katika riadha kuna ukanda huu wa kuanzia kondoa mpaka arusha na shimiwi pana vijana wana vipaji vizuri sana kukimbia mbio za marathon. hivyo wizara ya michezo inashindwa nini kuwekeza katika kanda hiyo. Kenya na ethiopia karibia wanariadha wake wote wanatoka mikoa ile ile husika baada ya mataifa hayo kuwekeza katika kanda hizo. keep in mind, if you invest in fever diseases is the profit!
 
Back
Top Bottom