polokwane
JF-Expert Member
- Dec 16, 2018
- 3,361
- 5,842
Sijui ni kwanini Serikali kwenye suala la manunuzi ya mali zake huwa haipo makini kila manunuzi ya Serikali yanapofanyika kuna pesa ya wizi inapita huko na kuna njia mbalimbali zinazotumika hapa ili kuiibia Serikali
1. Kuagiza vitu kwa idadi kubwa tofauti na mahitaji halisi ya Serikali sasa hapa kuna mambo, kwanza vinaagizwa vitu vingi na ndani yake inaingizwa order yao binafsi (Mafisadi) kwa hiyo mfano mahitaji ni 200,000 basi vitaombwa 250,000, hivyo elfu hamsini watajua wao watakavyoupeleka mchakato kati ya wanunuzi na watu wa store na record za ledger book ila Serikali itatoa hela ya 250,000 maana yake hapo kuna vitakavyoingizwa kwenye ledger na kuonekana vimetoka au visiingizwe kabisa kwenye ledger book.
2. Kuongeza gharama za manunuzi mara mbili au zaid ya bei halisi kama kitu kinauzwa Tsh.200,000/ basi serikali itauziwa kati ya Tsh.300,000 hadi Tsh. 350,000/- au zaid
3. Kununua vitu ambavyo ni low quality wakati vinavyohitajika na pesa iliyotoka serikalini ni ya vifaa vyenye high quality ( hili lilijitokeza kwenye vishkwambi, mashine za kusajili wapiga kura, mifumo ya kimtandao ya serikali , servers nk ndio maana mifumo mingi ya Derikali haiishi kusumbua kila mara)
4. Kuchanganya bidhaa original na feki zake, hasa zile zinazohitajika kwa wingi mf. Vifaa vya afya , vifaa vya kielectronic ,vifaa vya miradi ,vifaa vya kazi maalumu nk.
Yaani hapa iko hivi mfano vinahitajika vifaa 200,000 ambavyo bei yake ni Tsh.600,000/- kila kimoja ambacho ni original na high quality, kitakachofanyika ni kununua vifaa 100,000 original kabisa ambavyo navyo unaweza kukuta bei iliongezwa , halafu hivyo 100,000 vilivyo baki vinatafutwa feki yake vifananavyo na vinavyoweza kufanya kazi ile ile ila sio kwa ubora lakini kwa bei ya chini labda Tsh 250,000/- na hapa huwa order inatolewa China maana ndio kuna local industries zenye ubingwa wa kutoa copy za vitu kwa bei ndogo ili pesa ya juu watu waibe
5. Kuleta vitu vilivyoagizwa kwa mafungu mafungu yani kama vilihitajika vifaa labda 200,000 vinaletwa kwanza 130,000 halafu wanasikilizia kwanza kama kutakuwa na kelele wakiona kimya ndio imetoka hiyo vilivyobaki haviji tena pamoja na kwamba Serikali inakuwa ilishatoa hela ya vyote 200,000 na baada ya hapo wanacheza na watu wa record kwenye ledger book idadi inajazwa lakini vitu havipo.
Zipo njia nyingi zaidi na sitaki kuamini kwamba serikali haijui