Msigazi Mkulu
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 4,184
- 3,421
Kama kawaida kila nikipita pale kivukoni huwa naangalia mapungufu, nilianza na la chenji ya mia mia kutorudishwa. Na leo nimebaini abiria wakinunua tiketi pale dirishani pale sehemu ya kuscania inawekwa nyuma ya tiketi nyingine huku ikitunzwa vizuri bila kuharibiwa. Hii inamaanisha zinarudishwa tena dirishani kuuzwa tena. Ndo maana baadae mtasikia kuna hasara kubwa kumbe pesa zinaishia mifukoni mwa watu.