Wizi mpya waibuka

Wizi mpya waibuka

Mtakuwa wa mikoani nyie...au wanafunzi wapya jijini...
Mkiwa na watoto baadae muwe mnawapa nauli waje kutembea mjini, mpe hela ya kula na nauli tu...
pakulala..fuata miongozo ya mpwayungu village
mjini ni shule....
 
Hao watu nawajua, kuna hp spectre x360 walikua wanauza kwa 450k, wakasema wapo dom jengo hilo hilo, kidg nitume hela, bt kuna ndugu yangu yupo jengo hilo hilo nikamuomba anichunguzie, ndo kunishtua kwamba kweli wapo kwenye jengo hilo, na hiyo pc ipo, ila ni 3.5mil, huyo jamaa anamfaham ni tapeli, ukimtumia hela tu imekula kwako...hiyo ndo ilikua pona yangu...
Kwanini hamkuweka mtego mumkamate iwe mwisho wa utapeli wake?
 
Uyo jamaa nimewahi chat nae aniuzie PC ila sikutuma hela nilimuagiza mtu aliyepo Dodoma akachukue ndio nimtumie hela alizima simu siku nzima.... nikaachana nae
 
Habari za leo wakuu.

Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo husika.

Kuna wizi mkubwa sana unaendelea kasi kubwa sana hasa kwenye mtandao wa Facebook Kuna jamaa wanatumia trick ya kupost laptop computers wakidai wanauza. Hawa jamaa wanauza computer kwa bei ndogo sana ukilinganisha na bidhaa yenyewe, na hiyo ni kumshawishi mtu ili aingie mkenge.

Mara nyingi ukiwauliza kwamba mnapatikana wapi watakutumia namba ili muwasiliane kwa WhatsApp.
Na badae watakupa number ya kufanya malipo, Mara nyingi sana wanasema wanapatikana dodoma, Barabara ya nane,Jengo la capital city mall,Floor 1,duka All Muzamill PC solutions,Flame B6.

Number za simu wanazotumia.
0676976799
0678448681
0678376783
Tuchukue tahadhari....

Naomba kuwasilisha hoja.
Palipo na mapungufu mnisamehe
huu ni wizi mpya au wewe ndo mgeni wa mitandao?
 
Hapa kuna wengine mnatupiga za Uso, unakuta ni kweli Mtu unafanya biashara ya kuuza Laptop, tena kwa bei chee, Ila kuna watu wanaharibu. Mimi nauza Laptop, Kwahivyo ni makubaliano mimi na mteja, Kama ana ndugu yake anamuagiza anaijia ofisini, Wengine nawatumia. Kwahivyo msiharibu biashara za watuz unatakiwa ujihakikishie kwanza.
 
Unatumaje pesa kwa bidhaa uliyoiona kwa picha tu bila kuona kiuhalisia na kuimiliki?

UJINGA.
 
Ni ujinga tu mi nimekutana kupatana mchizi yuko machinga complex nikaenda mwenyewe ofisini nikaiona nikalipa nikasepa nayo ofcoz bei rahisi tu we unalipaje hujaona mzigo?.
 
Habari za leo wakuu.

Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo husika.

Kuna wizi mkubwa sana unaendelea kasi kubwa sana hasa kwenye mtandao wa Facebook Kuna jamaa wanatumia trick ya kupost laptop computers wakidai wanauza. Hawa jamaa wanauza computer kwa bei ndogo sana ukilinganisha na bidhaa yenyewe, na hiyo ni kumshawishi mtu ili aingie mkenge.

Mara nyingi ukiwauliza kwamba mnapatikana wapi watakutumia namba ili muwasiliane kwa WhatsApp.
Na badae watakupa number ya kufanya malipo, Mara nyingi sana wanasema wanapatikana dodoma, Barabara ya nane,Jengo la capital city mall,Floor 1,duka All Muzamill PC solutions,Flame B6.

Number za simu wanazotumia.
0676976799
0678448681
0678376783
Tuchukue tahadhari....

Naomba kuwasilisha hoja.
Palipo na mapungufu mnisamehe
Mimi huwa nawaambia nakuja ofisini wanaanza kujing'ata ng'ata... nawapotezea
 
TCRA na Makampuni ya Simu yatanatakiwa yaje na mfumo 1

Namba ukishapewa hakuna kuibadilisha, mbona TIN zipo milele.

Mtu awe na namba za kampuni husika 1 tu kwa kila kampuni...

Kwa wafanya biashara na makampuni wao namba zao zisajiliwe na kampuni husika ila anayepewa hiyo namba ya kampuni yatokee majina yake na kampuni kwa wakati 1

Ukifanya utapeli TCRA wablock namba zote zilizowahi tumia simu husika, wafunge NIDA etc
 
Hao watu nawajua, kuna hp spectre x360 walikua wanauza kwa 450k, wakasema wapo dom jengo hilo hilo, kidg nitume hela, bt kuna ndugu yangu yupo jengo hilo hilo nikamuomba anichunguzie, ndo kunishtua kwamba kweli wapo kwenye jengo hilo, na hiyo pc ipo, ila ni 3.5mil, huyo jamaa anamfaham ni tapeli, ukimtumia hela tu imekula kwako...hiyo ndo ilikua pona yangu...
Kuna mzee mmoja alikuwa na kawaida ya kusema ''mijitu mijinga hata ingeuawa kila siku lakini haitaisha''. Kweli dunia ya leo unatuma fedha ya kununua bidhaa kwa mtu ambaye humjui bali amekuonyesha tu picha? Kweli binadamu tunatofautiana!
 
TCRA na Makampuni ya Simu yatanatakiwa yaje na mfumo 1

Namba ukishapewa hakuna kuibadilisha, mbona TIN zipo milele.

Mtu awe na namba za kampuni husika 1 tu kwa kila kampuni...

Kwa wafanya biashara na makampuni wao namba zao zisajiliwe na kampuni husika ila anayepewa hiyo namba ya kampuni yatokee majina yake na kampuni kwa wakati 1

Ukifanya utapeli TCRA wablock namba zote zilizowahi tumia simu husika, wafunge NIDA etc
Hili litaleta usumbufu kwa watu wasio na hatia. Utaratibu uliopo wa kusajili line unaweza kumaliza au kupunguza hili tatizo iwapo usajili wa simu ungefanyika kwa umakini. Ingekuwa rahisi sana kunasa matapeli. Hili ni kosa la serikali yetu iliyojaa watu wavivu na vilaza.
 
Wabongo wanapenda virahisi

Kitu cha 600,000 yeye anaitaka

Kwa 200,000

Acha wapigwe tu

Ova
Kwenye utapeli wowote chanzo kikubwa ni tamaa. Hata wale wazee wa kanyaboya hupata watu kwa sababu watu wanapenda rahisi. Kuna dada mmoja alirudi nyumbani na ''iphone'' yake kuifungua akakuta ni kipande cha mbao. Anadai aliyemuuzia alimwambia ''ameipiga'' sehemu hivyo anataka fedha kidogo tu ya chapuchapu. Tukamuuliza: sasa wewe ulifurahia mwenzako kuibiwa ili ufaidike wewe huoni unastahili kabisa lililokupata?
 
sasa kuufunga uzi huu:

kupenda bei ndogo = kuwa na akili ndogo
 
Back
Top Bottom