Wizi unaofanywa Halmashauri ni matokeo ya madiwani wasiowajibika

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Halmashauri ni mali ya wananchi na wanamiliki Halmashauri kupitia Baraza la Madiwani.

Halmshauri inasimamiwa moja kwa moja na Madiwani, inasikitisha sana Halmashauri ndipo pesa zinapigwa sana, huku wasimamizi wapo kila siku na wanaendelea kula posho za vikao.

Tatizo la kuibiwa ni matokeo ya kuwa na madiwani wa ovyo ambao wamechaguliwa na sisi wananchi, msimu wa uchaguzi wananchi huwa tunajadili sana nafasi ya Ubunge na Urais huku tukiacha eneo sensitive sana ambalo ni madiwani. Tumejikuta tuna madiwani wa ovyo kiasi kwamba hawawezi kutambua upuuzi unaofanywa na wafanyakazi wa Halmshauri.

Nadhani uchaguzi wa madiwani ungetenganishwa na uchaguzi wa Wabunge na Urais ili tu kutengeneza umakini na wananchi kufikiria ni aina gani ya diwani wanamtaka na anastahili kuwa Diwani wao, otherwise tutabaki kulalamika miaka na miaka na hakuna kitakachobadilika.

How come mimi mtumishi kwetu Tandahimba niwe na uchungu na wananchi wa Njombe? Diwani ndiye mwenye uchungu na ndiye yupo na wananchi kila siku ,lakini kwa bahati mbaya madiwani wengi vilaza hasa hawa wa CCM matokeo yake ni haya pesa zinapigwa, maendeleo yanasua sua.

Mwizi ni mtu anayetumia akili so unahitaji mlinzi wa mali awe na akili zaidi ya mwizi, sasa sisi Tanzania ni kinyume madiwani wengi uwezo wao upo chini.
 
Hao madiwani nani aliwachagua mbali na kutangazwa kwa mtutu wa bunduki na wengine kupita bila kupingwa hovyo kabisa.
 
UPO SAHIHI LAKINI PIA NA WAKURUGENZI wasio na ELIMU ya Masuala ya FEDHA.

Wakurugenzi wengi wanateuliwa KISIASA bila kujali kama ana Elimu ya kwenda Kusimamia FEDHA na pia wapo ki UKADA na kwa kuwa wengi wao hawana Elimu ya Masuala ya Fedha WAHASIBU kwa maana ya WAWEKA HAZINA wa HALMASHAURI wanawapotosha na kusababisha WIZI wa FEDHA za HALMASHAURI.
Ushauri

Nafasi za WAKURUGENZI ZITANGAZWE waombe watu kwa SIFA za VYETI VYAO sio huku Kuteuana kwa Kujuana kwani MATOKEO yake ni MKURUGENZI kushindwa kusimamia FEDHA za UMMA na WAJANJA KUZIIBA
 
Nafasi za WAKURUGENZI ZITANGAZWE waombe watu kwa SIFA za VYETI VYAO sio huku Kuteuana kwa Kujuana kwani MATOKEO yake ni MKURUGENZI kushindwa kusimamia FEDHA za UMMA na WAJANJA KUZIIBA
Wakurugenzi wa Halmashauri walikuwa wanateuliwa kutoka miongoni mwa wakuu wa Idara., Uzoefu ukiwa ni miaka 6 ya ukuu wa Idara.

Wakuu wa Idara za Halmashauri walikuwa wanapendekezwa (promoted) na madiwani baada ya kupata sifa za uzoefu kazini usiopungua miaka 7 katika nafasi za afisa wa kawaida. Mtu anapokuwa mkuu wa Idara anakuwa anasimamia watumishi na fedha za idara yake.

naingia vikao vya menejimenti na kuona fedha za idara nyingine na usimamizi wake, anapokuja kuteuliwa kuwa Mkurugenzi anakuwa anajua usimamizi wa fedha yote ya Halmashauri.

JPM alipoingia akaanza kuteua wanasiasa, na imeendelezwa mpaka sasa, ndio wanaenda hao wasio na uzoefu wa usimamizi wa fedha. Viongozi wafuate sheria na miongozo, wakurugenzi wateuliwe kutoka kwa wakuu wa Idara.
 
Katibu wa UVCCM kata anateuliwa kuwa DED, mambo ya hovyo kabisa
 
99% ya DEDs ni makada wa CCM ni mambo ya hovyo kabisa
 
huku tukiacha eneo sensitive sana ambao ni madiwani tumejikuta tuna madiwani wa hovyo kiasi kwamba hawawezi kutambua upuzi unaofanywa na wafanyakazi wa halmshauri ,
Kata yangu ya Gangilonga, diwani wetu ni mhitimu wa kidato cha 4 (form four), kazi yake ni kinyozi, huyu ndio anaenda kusoma hizi ripoti za ukaguzi za ndani na za CAg, huyu ndiye anayesimamia mapato ya Manispaa ya Iringa. Mwenyekiti wa mtaa pia ni kinyozi na elimu yake ni darasa la 7. Hii ndiyo Kata ambayo ikulu ndogo ipo, Mahakama kuu, mahakama ya Wilaya, Hospitali ya Rufaa, Chuo cha Ualimu, Chuo Kikuu nk

Ndio kata inayoongoza kuwa na miundombinu mibovu ya barabara, ina mitaa 10 lakini ina zahanati moja tu ya kichovu, hakuna kituo cha afya. Tunaambiwa kigezo cha udiwani na uenyekiti ni kujua kusoma na kuandika. Uzoefu wa kazi walionao ni unyozi, wataweza kuona mipigo kwenye ripoti za ukaguzi??
 
Diwani anaibaje na wakati siyo signatory? chain ya wizi inaanzia wizarani kwenyewe mkuu
Diwani anaibiwa na wataalamu kwa kuwa juha. Akisomewa ripoti anasema imepita. Diwani akiibiwa maana yake tumeibiwa sisi.
 
Diwani anaibiwa na wataalamu kwa kuwa juha. Akisomewa ripoti anasema imepita. Diwani akiibiwa maana yake tumeibiwa sisi.
Diwani siyo mtaalamu wa mambo ya fedha, DED/DAS/DC/RAS/RC/TISS/TAKUKURU kazi yao ni nini? wanalipwa mishahara ya nini? Internal Auditor anafanya nini? mtu akiandika dokezo haombi kwa diwani anaomba kwa DED, diwani anaingiaje?
 
Uko sawa lakini sio sawa sana,kuna watu wameomba nafasi kwa elimu zao serikalini wamekosa uzalendo na ndio wanaongoza kwa kupiga,kiongozi wetu mkubwa alikwishatuambia tule kwa tule kwa urefu wa kamba zetu ila tusivimbewe hivyo kama wa kumwambia atupishe ktk uchaguzi ujao ni huyu.
 
Mkurugenzi anateuliwa fresh from school kwenda kusimamia watu waliokalia ofisi miaka na miaka Kwa nini asiibiwe. Hata yule binti aliyekuwa anasifiwa Morogoro waliomsifu waliokuwa wanamzunguka.
 
Diwani siyo mtaalamu wa mambo ya fedha, DED/DAS/DC/RAS/RC/TISS/TAKUKURU kazi yao ni nini? wanalipwa mishahara ya nini? Internal Auditor anafanya nini? mtu akiandika dokezo haombi kwa diwani anaomba kwa DED, diwani anaingiaje?
DED kazi yake ni kusimamia utendaji kazi wa wataalamu hapo halmashauri na pia kazi yake ni kukusanya mapato na kuandaa bajeti. Matumizi ya fedha iliyokusanywa yanapangwa na madiwani, ndio yanaingia kwenye bajeti.

Dokezo haliombwi kwa fedha ambayo haipo kwenye bajeti, ukiona mtumishi anaomba hela ya kula maandazi maana yake diwani alipitisha bajeti hiyo. Lawama ziende kwa mtumishi au kwa Diwani kupitisha bajeti za vitu vya ajabu ajabu??


Diwani ndiye anajua wananchi wamemtuma akaombe nini Halmashauri, anapopitisha vitu vya kijinga atalaumiwa DED wakati DED kazi yake ni kukusanya mapato tu, mpanga matumizi ni Baraza la Madiwani.

Angalia Iringa stendi ya Igumbilo wamejenga jengo la abiria kwa Bilioni 2 na hakuna abiria anayetaka kulitumia maana watu hawaipendi stendi ya Igumbilo. Hapo wenye shida ni madiwani vilaza kupitisha hoja wanazoletewa na wataalamu.
 
Diwani siyo mtaalamu wa mambo ya fedha, DED/DAS/DC/RAS/RC/TISS/TAKUKURU kazi yao ni nini? wanalipwa mishahara ya nini? Internal Auditor anafanya nini? mtu akiandika dokezo haombi kwa diwani anaomba kwa DED, diwani anaingiaje?
Diwani ni lazima awe msomi, ajue kusoma ripoti za ukaguzi. Ataona wapi anapopigwa. Mfano mimi napoambiwa shirika la ndege limeendeshwa kwa hasara, haijitaji mimi kujua mambo ya ndege ndio nione kuwa ni ujinga kuendelea na biashara inayoingiza hasara.
 
Diwani ni lazima awe msomi, ajue kusoma ripoti za ukaguzi. Ataona wapi anapopigwa. Mfano mimi napoambiwa shirika la ndege limeendeshwa kwa hasara, haijitaji mimi kujua mambo ya ndege ndio nione kuwa ni ujinga kuendelea na biashara inayoingiza hasara.
Hakuna ofisi inakula rushwa kama ofisi ya CAG mikoani, ukiona wamekuandika ujue mmeshindwana dau, kazi ya TISS na TAKUKURU nini?
 
Siyo kweli, diwani anaingia kwenye mfumo wa MUSE/Planrep? kinachofanyika wataalamu wanaanda budget wakiwa na DED madiwani wanakuja kupewa summary ya budget, hawa watu DAS/DC/RAS/RC/TISS na TAKUKURU kazi yao nini kama siyo kudhibiti fedha za umma mpk diwani ahusike ambaye siyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama?
 
Yaani mkuu ipo hivi. Planrep nk ni kama fundi anavyojenga nyumba, mtaani tutasema ile nyumba anajenga fulani (wewe) kwa maana ya umiliki na ulipaji ila anayechanganya simenti ni fundi, vivyo hivyo kwa Halmashauri, anayepanga bajeti ni Diwani ila anaandaliwa na wataalamu, inapopita tunasema Baraza la madiwani limepitisha bajeti.

Nyumba inapobomoka tutakusikitikia wewe kuwa ulitafuta fundi mbovu au hukusimamia vyema, bila kujali kuwa wewe huna utaalamu wa ujenzi, maana wewe ndio mwenye mali ilitakiwa uwe na uchungu nayo - sasa ndivyo ilivyo Halmashauri, wataalamu ni kama mafundi na diwani ndio mwenye nyumba. Anaambiwa alete mifuko 10 halafu inajengewa mitatu tu, saba inapigwa na yeye yupo.
 
Hakuna ofisi inakula rushwa kama ofisi ya CAG mikoani, ukiona wamekuandika ujue mmeshindwana dau, kazi ya TISS na TAKUKURU nini?
Ni kweli kabisa. Ila sasa Diwani hashindwi kuibua hoja yeye mwenyewe hata kama haipo kwenye hoja za ukaguzi. Ndio ishu kama za kina Tumbili Kafulila bungeni, unaibua hoja ambayo haipo ukaguzini na unaichambua na mwizi ataonekana tu. Kwa hiyo kama NAO watakula rushwa na mkurugenzi, bado madiwani wanaweza kuibua hoja wao wenyewe na kuwabana wabadhilifu. Sasa ili uibue hoja lazima bongo yako iwe makini, madiwani wetu no bongo lala.
 
Ndiwani anashinda halmashauri kusimamia malipo? Accounting Officer kazi yake nini? tuache utani unamteuaje UVCCM kuwa DED?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…