sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Mkuu, mifumo ipo kwa ajili ya kuhakikisha bajeti inafuatwa. Chukulia mfano huu, wataalamu wamepanga kuwa mwaka huu Halmashauri itajenga darasa kwa Tshs. 10,000,000/=(ufundi na material), ila gharama ya Injinia wa Halmashauri au Mkandarasi Mshauri kusimamia darasa hilo ni Tshs. 25,000,000/= na kwenye bajeti ikapitishwa.Ni mfumo ambao upo chini ya TAMISEMI unasimamiwa na KM TAMISEMI pia na RAS/ huwezi kufanya chochote bila hao watu kujua.
Na baadae kwenye utekelezwaji bajeti ikafuatwa kama ilivyo, je hapa patakuwa na hoja ya ukaguzi?? Jibu ni hapana, maana kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa kibajeti.
Ila sasa wananchi tutahoji, inakuwaje usimamizi uwe na gharama kubwa kuliko kilichojengwa? Hapo si watu wameamua tu kulipana posho pasipo sababu za msingi? Unakuta labda mhandisi alikuwa anaenda site mara 4 kwa siku na kila mara anayoenda analipwa posho, mnahoji kwa nini hakwenda na kukaa huko siku nzima? Nk
Sasa hapo TAKUKURU ndio wanaingia kazini kuwa kulikuwa na matumizi mabovu ya ofisi na fedha ya umma. Kwa hiyo kunakuwa hakuna hoja ya ukaguzi (CAG au Internal) ila kuna ubadhilifu umefanyika.