Wizi unaofanywa Halmashauri ni matokeo ya madiwani wasiowajibika

Wizi unaofanywa Halmashauri ni matokeo ya madiwani wasiowajibika

Ni kweli kabisa. Ila sasa Diwani hashindwi kuibua hoja yeye mwenyewe hata kama haipo kwenye hoja za ukaguzi. Ndio ishu kama za kina Tumbili Kafulila bungeni, unaibua hoja ambayo haipo ukaguzini na unaichambua na mwizi ataonekana tu. Kwa hiyo kama NAO watakula rushwa na mkurugenzi, bado madiwani wanaweza kuibua hoja wao wenyewe na kuwabana wabadhilifu. Sasa ili uibue hoja lazima bongo yako iwe makini, madiwani wetu no bongo lala.
Tatizo diwani anapataje nyaraka hizo na haingii kwenye mifumo ya malipo hana username wala password? diwani anahusika kwa sehemu ndogo sn
 
Ndiwani anashinda halmashauri kusimamia malipo? Accounting Officer kazi yake nini? tuache utani unamteuaje UVCCM kuwa DED?
Malipo si yanafanyika kwa mujibu wa bajeti mkuu? Ukiwa na bajeti huna haja ya kushinda ofisini maana kwenye kupitia bajeti na tathmini utaona kila kitu - hapo ndipo kuwajibishana kutakapoanza. Mfano umesema madokta wanunuliwa majoho kwa Shilingi milioni 5 lakini DED na DMO wakanunua majoho kwa milioni 15 bila kibali cha kamati cha Halmashauri.. hapo tayari utahoji na kumuwajibisha mtu. Huhitaji kukaa dirishani kwa muhasibu kuangalia vocha

Hata vikao vya michango ya harusi huwa tunabananishana kwa bajeti tu, makusanyo yalikuwa shilingi ngapi, matumizi shilingi ngapi na chenji shilingi ngapi
 
Majukumu ya DAS/DC/RAS/RC ni yapi kwenye usimamizi wa fedha za umma?
 
halmashauri ni mali ya wananchi na wanamiliki halmashauri kupitia baraza la madiwani , ,, halmshauri inasimamiwa moja kwa moja na madiwani , inasikitisha sana halmashauri ndipo pesa zinapigwa sana , huku wasimamizi wapo kila siku na wanaendelea kula posho za vikao , tatizo la kuibiwa ni matokeo ya kuwa na madiwani wa hovyo ambao wamechaguliwa na sisi wananchi, msimu wa uchaguzi wananchi huwa tunajadili sana nafasi ya ubunge na urais huku tukiacha eneo sensitive sana ambao ni madiwani tumejikuta tuna madiwani wa hovyo kiasi kwamba hawawezi kutambua upuzi unaofanywa na wafanyakazi wa halmshauri , nazani uchaguzi wa madiwani ungetenganishwa na uchaguzi wa wabunge na urais ili tu kutengeneza umakini na wananchi kufikiria ni aina gani ya diwani wana mtaka na anastahili kuwa diwani wao, otherwise tutabaki kulalamika miaka na miaka na hakuna kitakachobadilika, how come mimi mtumishi kwetu tandahimba niwe na uchungu na wananchi wa njombe,, diwani ndiye mwenye uchungu na ndiye yupo na wananchi kila siku ,lakini kwa bahati mbaya madiwani wengi vilaza hasa hawa wa CCM matokeo yake ni haya pesa zinapigwa , maendeleo yanasua sua, mwizi ni mtu anayetumia akili so unahitaji mlinzi wa mali awe na akili zaidi ya mwizi, sasa sisi tanznia ni kinyume madiwani wengi uwezo wao upo chini
Sema madiwwni vilaza wwliochaguliwa na CCM na wwjumbe wwke.

Chama tawala ni mpinzani mkubwa wa elimu na taaluma kwa sababu viongozi wake wengi ni vilaza ambao hata uwaelimishe vipi ni sawa na kumfundisha mbuzi kulala kitandani
 
Tatizo diwani anapataje nyaraka hizo na haingii kwenye mifumo ya malipo hana username wala password? diwani anahusika kwa sehemu ndogo sn
Kila robo mwaka, DED analeta ripoti nzima ya utekelezaji wa bajeti. Kila shilingi 10 inaonekana imetumikaje. Ni Kabrasha la kurasa za kutosha, zaidi ya 150, ni kazi ya diwani kusoma item 1 mpaka nyingine, na hapo ndipo wanapopigwa.

Kwanza muda wanaopewa makabrasha ni mchache, siku 7 kabla ya mkutano, lakini pia kusoma ni wavivu, kama ambavyo wengi humu hatutasoma ripoti ya CAG ila tutafanya mijadaka kupitia summary aliyotoa.
 
Mkuu mimi nataka uniambiwe wajibu wa hawa watu kwanza kabla ya hao madiwani( DAS/DC/RAS/RC/KM/Waziri wa TAMISEMI) wajibu wao nini katika kudhibiti na kusimamia fedha za umma?
 
UPO SAHIHI LAKINI PIA NA WAKURUGENZI wasio na ELIMU ya Masuala ya FEDHA.
Wakurugenzi wengi wanateuliwa KISIASA bila kujali kama ana Elimu ya kwenda Kusimamia FEDHA na pia wapo ki UKADA na kwa kuwa wengi wao hawana Elimu ya Masuala ya Fedha WAHASIBU kwa maana ya WAWEKA HAZINA wa HALMASHAURI wanawapotosha na kusababisha WIZI wa FEDHA za HALMASHAURI.
Ushauri
Nafasi za WAKURUGENZI ZITANGAZWE waombe watu kwa SIFA za VYETI VYAO sio huku Kuteuana kwa Kujuana kwani MATOKEO yake ni MKURUGENZI kushindwa kusimamia FEDHA za UMMA na WAJANJA KUZIIBA
Kweli kabisa
 
Majukumu ya DAS/DC/RAS/RC ni yapi kwenye usimamizi wa fedha za umma?
Kuingilia kati pale anapoona mradi unaotaka kufanywa hauna tija kwa umma. Pia kusimamia matumizi ya fedha inayokuwa imeletwa kama Ruzuku kutoka Serikali Kuu. Zingatia kuwa pesa zinazopigwa Halmashauri nyingi ni za makusanyo ya ndani (own source) ambapo serikali kuu hawaziingilii sana maana ni za wananchi wenyewe wa halmashauri husika. Yaani mfano Halmashauri ya Kinondoni wakisema wanajenga Swimming Pools kwa mabilioni ili wananchi wake waogelee, Serikali kuu haipaswi kupinga maana huenda hilo ndio takwa la wakazi wa Kinondoni, ndio kipaumbele chao. Diwani yupo kuwasilisha maslahi na matakwa ya wananchi
 
Asante sn, hivi unajua kuna mfumo unaitwa LGIS unasimamiwa na RAS/RC?
 
Mkuu mimi nataka uniambiwe wajibu wa hawa watu kwanza kabla ya hao madiwani( DAS/DC/RAS/RC/KM/Waziri wa TAMISEMI) wajibu wao nini katika kudhibiti na kusimamia fedha za umma?
Halmashauri (madiwani) inaanzisha vyanzo vyake vya mapato, na inaweka bajeti kuwa kupitia vyanzo hivyo ikusanye kiasi kadhaa na ikipatikana itatumika kwa matumizi haya na haya.

Waziri wa Tamisemi anapeleka bajeti hiyo bungeni na bunge linaibariki, makusanyo yanakuwa ni halali. Mapato yamekusanywa na DED, anaanza kuyatumia kama ilivyokuwa bajetini. Kwa makusudi anaacha kufuata bajeti anaanza kufanya yake. Diwani ndio tumemtuma ahakikishe bajeti inafuatwa, yeye anabaki kutoa macho. RC anasema ile hela sio yangu, sijaitoa mimi, wameitoa wananchi na wana mwakilishi wao, mimi nakaa kuangalia, kwenye mapitio ya bajeti nitalisema hili ili diwani achukue hatua, amshtaki huyu DED mahakamani kwa ubadhilifu. Diwani anaambiwa na hachukui hatua, that's it
 
Poor argument, Mfumo wa LGIS unaosimamia mapato ya ndani upo chini ya TAMISEMI na mtendaji mkuu ndani ya mkoa ni RAS, je anashindwaje kuchukua hatua kwa fedha za umma?
 
Poor argument, Mfumo wa LGIS unaosimamia mapato ya ndani upo chini ya TAMISEMI na mtendaji mkuu ndani ya mkoa ni RAS, je anashindwaje kuchukua hatua kwa fedha za umma?
Sio poor argument, hii ni fact mkuu.

Siwezi kuuongelea huo mfumo sababu siufahamu. Halmashauri najua walikuwa wanatumia mfumo wa Epicor kufanya malipo yao. Mfumo hauzuii kutofanyika ubadhilifu, bali unazuia matumizi kutofanyika nje ya bajeti. Sasa wataalamu wanafanya re-allocation ya funds wenyewe bila idhini ya madiwani, kifungu kilichokuwa na milioni 5 kinakuzwa mpaka kifike milioni 50, kwa hiyo unakuta zote zimeliwa kwa shughuli ambayo bajeti ilitaka itumike milioni 5 tu.

Au mtu analipwa posho ya safari kwa kifungu cha ununuzi wa stationery. Sasa ukishajua haya unafanyaje?? Ndio unawawajibisha hao waliokiuka bajeti. Mifumo ya malipo sio ishu kubwa, ishu ni uwajibishanaji. Ukisikia hizi plea bargain zimeliwa au invoice ya ndege imeongezeka, sio kuwa hakuna mifumo, mifumo ipo ila watu wanaamua kutoifuata - sasa je unawachukulia hatua?? Hilo ndio la msingi ambalo madiwani wanafeli
 
Ni mfumo ambao upo chini ya TAMISEMI unasimamiwa na KM TAMISEMI pia na RAS/ huwezi kufanya chochote bila hao watu kujua.
Mkuu, mifumo ipo kwa ajili ya kuhakikisha bajeti inafuatwa. Chukulia mfano huu, wataalamu wamepanga kuwa mwaka huu Halmashauri itajenga darasa kwa Tshs. 10,000,000/=(ufundi na material), ila gharama ya Injinia wa Halmashauri au Mkandarasi Mshauri kusimamia darasa hilo ni Tshs. 25,000,000/= na kwenye bajeti ikapitishwa.

Na baadae kwenye utekelezwaji bajeti ikafuatwa kama ilivyo, je hapa patakuwa na hoja ya ukaguzi?? Jibu ni hapana, maana kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa kibajeti.

Ila sasa wananchi tutahoji, inakuwaje usimamizi uwe na gharama kubwa kuliko kilichojengwa? Hapo si watu wameamua tu kulipana posho pasipo sababu za msingi? Unakuta labda mhandisi alikuwa anaenda site mara 4 kwa siku na kila mara anayoenda analipwa posho, mnahoji kwa nini hakwenda na kukaa huko siku nzima? Nk

Sasa hapo TAKUKURU ndio wanaingia kazini kuwa kulikuwa na matumizi mabovu ya ofisi na fedha ya umma. Kwa hiyo kunakuwa hakuna hoja ya ukaguzi (CAG au Internal) ila kuna ubadhilifu umefanyika.
 
Back
Top Bottom