Wizi unaofanywa Halmashauri ni matokeo ya madiwani wasiowajibika

Tatizo diwani anapataje nyaraka hizo na haingii kwenye mifumo ya malipo hana username wala password? diwani anahusika kwa sehemu ndogo sn
 
Na serikali za awamu zote zimetudhihirishia kuwa CCM imefeli kwa asilimia mia (100%) katika kuzalisha viongozi.

Mpaka pale tutakapoachana na mfumo wa uongozi wa kiCCM CCM,ndipo Tanzania itapiga hatua kimaendeleo ya kweli.
Mfumo umekaa kijinga sn wa hizi teuzi
 
Ndiwani anashinda halmashauri kusimamia malipo? Accounting Officer kazi yake nini? tuache utani unamteuaje UVCCM kuwa DED?
Malipo si yanafanyika kwa mujibu wa bajeti mkuu? Ukiwa na bajeti huna haja ya kushinda ofisini maana kwenye kupitia bajeti na tathmini utaona kila kitu - hapo ndipo kuwajibishana kutakapoanza. Mfano umesema madokta wanunuliwa majoho kwa Shilingi milioni 5 lakini DED na DMO wakanunua majoho kwa milioni 15 bila kibali cha kamati cha Halmashauri.. hapo tayari utahoji na kumuwajibisha mtu. Huhitaji kukaa dirishani kwa muhasibu kuangalia vocha

Hata vikao vya michango ya harusi huwa tunabananishana kwa bajeti tu, makusanyo yalikuwa shilingi ngapi, matumizi shilingi ngapi na chenji shilingi ngapi
 
Majukumu ya DAS/DC/RAS/RC ni yapi kwenye usimamizi wa fedha za umma?
 
Sema madiwwni vilaza wwliochaguliwa na CCM na wwjumbe wwke.

Chama tawala ni mpinzani mkubwa wa elimu na taaluma kwa sababu viongozi wake wengi ni vilaza ambao hata uwaelimishe vipi ni sawa na kumfundisha mbuzi kulala kitandani
 
Tatizo diwani anapataje nyaraka hizo na haingii kwenye mifumo ya malipo hana username wala password? diwani anahusika kwa sehemu ndogo sn
Kila robo mwaka, DED analeta ripoti nzima ya utekelezaji wa bajeti. Kila shilingi 10 inaonekana imetumikaje. Ni Kabrasha la kurasa za kutosha, zaidi ya 150, ni kazi ya diwani kusoma item 1 mpaka nyingine, na hapo ndipo wanapopigwa.

Kwanza muda wanaopewa makabrasha ni mchache, siku 7 kabla ya mkutano, lakini pia kusoma ni wavivu, kama ambavyo wengi humu hatutasoma ripoti ya CAG ila tutafanya mijadaka kupitia summary aliyotoa.
 
Mkuu mimi nataka uniambiwe wajibu wa hawa watu kwanza kabla ya hao madiwani( DAS/DC/RAS/RC/KM/Waziri wa TAMISEMI) wajibu wao nini katika kudhibiti na kusimamia fedha za umma?
 
Kweli kabisa
 
Majukumu ya DAS/DC/RAS/RC ni yapi kwenye usimamizi wa fedha za umma?
Kuingilia kati pale anapoona mradi unaotaka kufanywa hauna tija kwa umma. Pia kusimamia matumizi ya fedha inayokuwa imeletwa kama Ruzuku kutoka Serikali Kuu. Zingatia kuwa pesa zinazopigwa Halmashauri nyingi ni za makusanyo ya ndani (own source) ambapo serikali kuu hawaziingilii sana maana ni za wananchi wenyewe wa halmashauri husika. Yaani mfano Halmashauri ya Kinondoni wakisema wanajenga Swimming Pools kwa mabilioni ili wananchi wake waogelee, Serikali kuu haipaswi kupinga maana huenda hilo ndio takwa la wakazi wa Kinondoni, ndio kipaumbele chao. Diwani yupo kuwasilisha maslahi na matakwa ya wananchi
 
Asante sn, hivi unajua kuna mfumo unaitwa LGIS unasimamiwa na RAS/RC?
 
Mkuu mimi nataka uniambiwe wajibu wa hawa watu kwanza kabla ya hao madiwani( DAS/DC/RAS/RC/KM/Waziri wa TAMISEMI) wajibu wao nini katika kudhibiti na kusimamia fedha za umma?
Halmashauri (madiwani) inaanzisha vyanzo vyake vya mapato, na inaweka bajeti kuwa kupitia vyanzo hivyo ikusanye kiasi kadhaa na ikipatikana itatumika kwa matumizi haya na haya.

Waziri wa Tamisemi anapeleka bajeti hiyo bungeni na bunge linaibariki, makusanyo yanakuwa ni halali. Mapato yamekusanywa na DED, anaanza kuyatumia kama ilivyokuwa bajetini. Kwa makusudi anaacha kufuata bajeti anaanza kufanya yake. Diwani ndio tumemtuma ahakikishe bajeti inafuatwa, yeye anabaki kutoa macho. RC anasema ile hela sio yangu, sijaitoa mimi, wameitoa wananchi na wana mwakilishi wao, mimi nakaa kuangalia, kwenye mapitio ya bajeti nitalisema hili ili diwani achukue hatua, amshtaki huyu DED mahakamani kwa ubadhilifu. Diwani anaambiwa na hachukui hatua, that's it
 
Poor argument, Mfumo wa LGIS unaosimamia mapato ya ndani upo chini ya TAMISEMI na mtendaji mkuu ndani ya mkoa ni RAS, je anashindwaje kuchukua hatua kwa fedha za umma?
 
Poor argument, Mfumo wa LGIS unaosimamia mapato ya ndani upo chini ya TAMISEMI na mtendaji mkuu ndani ya mkoa ni RAS, je anashindwaje kuchukua hatua kwa fedha za umma?
Sio poor argument, hii ni fact mkuu.

Siwezi kuuongelea huo mfumo sababu siufahamu. Halmashauri najua walikuwa wanatumia mfumo wa Epicor kufanya malipo yao. Mfumo hauzuii kutofanyika ubadhilifu, bali unazuia matumizi kutofanyika nje ya bajeti. Sasa wataalamu wanafanya re-allocation ya funds wenyewe bila idhini ya madiwani, kifungu kilichokuwa na milioni 5 kinakuzwa mpaka kifike milioni 50, kwa hiyo unakuta zote zimeliwa kwa shughuli ambayo bajeti ilitaka itumike milioni 5 tu.

Au mtu analipwa posho ya safari kwa kifungu cha ununuzi wa stationery. Sasa ukishajua haya unafanyaje?? Ndio unawawajibisha hao waliokiuka bajeti. Mifumo ya malipo sio ishu kubwa, ishu ni uwajibishanaji. Ukisikia hizi plea bargain zimeliwa au invoice ya ndege imeongezeka, sio kuwa hakuna mifumo, mifumo ipo ila watu wanaamua kutoifuata - sasa je unawachukulia hatua?? Hilo ndio la msingi ambalo madiwani wanafeli
 
Ni mfumo ambao upo chini ya TAMISEMI unasimamiwa na KM TAMISEMI pia na RAS/ huwezi kufanya chochote bila hao watu kujua.
Mkuu, mifumo ipo kwa ajili ya kuhakikisha bajeti inafuatwa. Chukulia mfano huu, wataalamu wamepanga kuwa mwaka huu Halmashauri itajenga darasa kwa Tshs. 10,000,000/=(ufundi na material), ila gharama ya Injinia wa Halmashauri au Mkandarasi Mshauri kusimamia darasa hilo ni Tshs. 25,000,000/= na kwenye bajeti ikapitishwa.

Na baadae kwenye utekelezwaji bajeti ikafuatwa kama ilivyo, je hapa patakuwa na hoja ya ukaguzi?? Jibu ni hapana, maana kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa kibajeti.

Ila sasa wananchi tutahoji, inakuwaje usimamizi uwe na gharama kubwa kuliko kilichojengwa? Hapo si watu wameamua tu kulipana posho pasipo sababu za msingi? Unakuta labda mhandisi alikuwa anaenda site mara 4 kwa siku na kila mara anayoenda analipwa posho, mnahoji kwa nini hakwenda na kukaa huko siku nzima? Nk

Sasa hapo TAKUKURU ndio wanaingia kazini kuwa kulikuwa na matumizi mabovu ya ofisi na fedha ya umma. Kwa hiyo kunakuwa hakuna hoja ya ukaguzi (CAG au Internal) ila kuna ubadhilifu umefanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…