Wizi unaofanywa Halmashauri ni matokeo ya madiwani wasiowajibika

Ni mfumo ambao upo chini ya TAMISEMI unasimamiwa na KM TAMISEMI pia na RAS/ huwezi kufanya chochote bila hao watu kujua.
Mkuu, mifumo ipo kwa ajili ya kuhakikisha bajeti inafuatwa. Chukulia mfano huu, wataalamu wamepanga kuwa mwaka huu Halmashauri itajenga darasa kwa Tshs. 10,000,000/=(ufundi na material), ila gharama ya Injinia wa Halmashauri au Mkandarasi Mshauri kusimamia darasa hilo ni Tshs. 25,000,000/= na kwenye bajeti ikapitishwa.

Na baadae kwenye utekelezwaji bajeti ikafuatwa kama ilivyo, je hapa patakuwa na hoja ya ukaguzi?? Jibu ni hapana, maana kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa kibajeti.

Ila sasa wananchi tutahoji, inakuwaje usimamizi uwe na gharama kubwa kuliko kilichojengwa? Hapo si watu wameamua tu kulipana posho pasipo sababu za msingi? Unakuta labda mhandisi alikuwa anaenda site mara 4 kwa siku na kila mara anayoenda analipwa posho, mnahoji kwa nini hakwenda na kukaa huko siku nzima? Nk

Sasa hapo TAKUKURU ndio wanaingia kazini kuwa kulikuwa na matumizi mabovu ya ofisi na fedha ya umma. Kwa hiyo kunakuwa hakuna hoja ya ukaguzi (CAG au Internal) ila kuna ubadhilifu umefanyika.
 
Kupigwa kwa pesa za Halmashauri ni ngumu sana kudhibiti, maana unakuta diwani anajuwa tu kusoma na kuandika halafu anamsimamia msomi mwenye degree zake na masters., hapo unategemea nn. Unakuta diwani anaambiwa saini hapa 5,000,000 then ikaachwa wazi huko mbele bila kufungwa jamaa wanakuja wanaongeza yao inakuwa 5,000,000,000/= wanafunga nakufunga ha ha haaaaa daaaah hatare sana.
 
Diwani ana polisi au gereza mkuu? kwanini DC/RC ambao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wasifanye hizo kazi? Epicor haipo kuna MUSE na LGIS, lakini DED anateuliwa na Rais kwanini asiwe mwaminifu kwa mamlaka iliyomteua mpk diwani ambaye hana mamlaka? diwani hata akikamata wizi hawezi kumfukuza DED, DED anasimamiwa na hawa DAS/DC/RAS/RC/KM/Waziri/PM hawa ndiyo wasaliti wa wananchi.
 
Majukumu ya RAS(Katibu Tawala Mkoa) unayajua vizuri mkuu? google
 

Hao hao Wakurugenzi ndo wezi wakubwa, fedha itaidhinishwa vipi pasipo Mkurugenzi kuwa na taarifa?
 
Utaratibu wa kuwapata hawa watendaji ndio janga kuu
 
Hao madiwani wapo kwa mujibu wa katiba, "ujue tu kusoma na kuandika" matatizo yanaanzia pale. Wanaongea kwa kugonga meza.
 
Hao hao Wakurugenzi ndo wezi wakubwa, fedha itaidhinishwa vipi pasipo Mkurugenzi kuwa na taarifa?
Mkuu, hawa wakurugenzi ndio wezi, lakini wa kalamu. Sasa utawawajibisha vipi huku hutambui kuwa wanakuibia?
 
Hao madiwani wapo kwa mujibu wa katiba, "ujue tu kusoma na kuandika" matatizo yanaanzia pale. Wanaongea kwa kugonga meza.
Na wataalamu hawataki kabisa msomi agombee udiwani. Hata ukigombea kwa chama tawala, jina lako litakatwa waende wanaojua kusoma na kuandika.
 
diwani hata akikamata wizi hawezi kumfukuza
Wafanyakazi wa Halmashauri wanawajibishwa na Baraza la madiwani. Madiwani ndio wanaothibitisha ajira, wanaopandisha vyeo na wanaoadhibu kwa kukata mshahara, kushusha cheo au kufukuza kazi mtumishi mpaka ngazi ya mkuu wa Idara, isipokuwa DED tu.
 
Wafanyakazi wa Halmashauri wanawajibishwa na Baraza la madiwani. Madiwani ndio wanaothibitisha ajira, wanaopandisha vyeo na wanaoadhibu kwa kukata mshahara, kushusha cheo au kufukuza kazi mtumishi mpaka ngazi ya mkuu wa Idara, isipokuwa DED tu.
Diwani akita kumchukulia hatua mtumishi RAS/Katibu mkuu TAMISEMI anamhamisha kwenda sehemu nyingine ambayo diwani hana mamlaka nayo, nilitamatani tulilie kuondoa huu mfumo ovu.
 
Mkuu, hawa wakurugenzi ndio wezi, lakini wa kalamu. Sasa utawawajibisha vipi huku hutambui kuwa wanakuibia?

Ni sahihi kabisa. Wakurugenzi wengi wameingizwa kutoka ukadani, hawana hofu juu ya wizi, wana jeuri ya kufanya wanayoyataka wao. Hawana uoga kabisa. Hata zile taratibu za kiutumishi tu hawazifahamu…Cha kusikitisha zaidi wanapatiwa jeuri na walio juu (Mafungu yanafanya kazi). Ni kama wamewekwa kwa mission.
 
Madiwani wenyewe ni Darasa la Saba.

Kuna halmshauri Moja hivi, mwenyekiti wake ni Mwalimu wale wa shule ya Msingi enzi zilee, akastaafu yaan ana cheti tu Cha ualim ule wa Daraja Sijui langapi wale wanaofundisha A E I O U.


basi, Mkugenzi wake na DC, wanakula helaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…