amaregesii
Member
- Jun 17, 2022
- 5
- 2
Kuna wizi unafanywa na mawakala wanaokata gate pass za kukuruhusu wewe abiria kuingia kwenye stendi hiyo. Kawaida ukifika kituo hicho inabidii ukate gate pass yenye thamani ya Tsh 200, na unapewa risiti na kisha unaruhusiwa kuingia.
Tumefika stendi hiyo tukiwa wawili tukatoa 500, wakala akatupa gate pass alafu akatuambia hakuna sh 100, kwahyo inabidii mwende, jambo hilo sikupendezwa nalo kwahyo nikaanza kudai chenji yangu kwa vile ni haki yangu, yule wakala alikuwa akijibu kuwa hana 100 ana 200 tu nyingi kwahyo inabidii tuondoke tuingie stendi. baada ya majibizano tukaamua kurudisha ile tiketi aturudishie hela yetu tujaribu kuingia kwa mageti mengine.
Tumeenda geti la pili ila tukaja na mpango wa kuwa kama wana 200 nyingi basi tuwape 2000 waturudishie 1600 kwavile gate pass moja ni 200 na sisi tuko wawili. basi kwenye hilo gate la pili tukampa wakala 2000, na yeye akaturudishia 1500, tukamuuliza " kwa nini umerudishia hii wakati tumekusikia ukimwambia wa mbele yetu kuwa huna 100 una 200", na yeye madai yake akaanza kusema kuwa hana 100 wala 200 wakati ametoka kumpa chenji mtu wa mbele yetu ya 200 kwa vile yeye alitoa 500.
Sasa jambo hilo ndio hatukufurahishwa nalo kabisa, baada ya majibizano hapo pia ilibidii tuingie stendi kwasababu tulikuwa tumesha poteza muda sana.
Sasa najiuliza Je, wanafanya ivi mara ngapi kwa wiki au kwa mwezi, maana wanakuwa wanatuibia sisi abiria na kujinufaisha wao. na je, wakuu wa kituo hicho wanajua kinachofanyika na mawakala hao? na kama wanajua kwa nini wasihakikishe upatikanaji wala hela hizo katika kituo hicho ili kuepusha wizi huo tunaofanyiwa sisi abiria.
Tunaomba mamlaka husika ifatilie vitendo hivi katika stendi hiyo na pia ihakikishe chenji izo ziwe zinapatikana mahali hapo, kwani nikupotezeana muda pamoja na kunyima haki ya abiria anapoingia katika stendi hiyo.