Wizi wa Masega Watua Kwa Rais Samia, Aeleza Mafundi Gereji Wanavyopasua Exhaust

Wizi wa Masega Watua Kwa Rais Samia, Aeleza Mafundi Gereji Wanavyopasua Exhaust

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani Jijini Arusha leo June 25,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba siku hizi kuna mtindo mpya wa Watu kupasua bomba linalotoa moshi wenye sumu kwenye gari na kuchukua unga uliopo ndani yake na kuchanganywa na cocaine au heroin kisha Vijana wanavuta na kupata madhara ikiwemo kufariki.

“Tumepata taarifa kwamba kuna bidhaa zinaingizwa nchini lakini zinachanganywa na dawa za kulevya na nimeona kwenye banda la maonesho wamenionesha wanasema Mtu anaweza kuja na unga lakini ule unga usiwe wa kawaida”

“Kuna bidhaa pia zinachanganywa na cocaine na heroin ambazo zinaweza kuwa sumu, siku hizi kuna mtindo wanapasua bomba linalotoa moshi kwenye gari ndani yake kule kuna unga fulani unaosababisha control ya ule moshi sasa ule unatolewa huko kwenye magereji yetu unapelekwa kwenye maunga Vijana wetu wanayotumia lakini ule moshi una sumu kubwa sasa ukichanganya na unga wanaotumia wakijidunga ndio maana unasikia Mateja wanaanguka wanakufa, niombe Mamlaka zinazohusika tuliangalie hili”

“Wenye gereji pia walitazame hili magari wanayopelekewa Mafundi wao wanapasua wanatoa unga wanakwenda kuua Watu”

 
Back
Top Bottom