KERO Wizi wa Mpunga na Mchele katika mashine za kuchakata mchele maeneo mbali mbali nchini

KERO Wizi wa Mpunga na Mchele katika mashine za kuchakata mchele maeneo mbali mbali nchini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
344
Reaction score
350
Hii ni mada ya kukufumbua macho mkulima.

Dhima kuu ya mada hii "Kulinda maslahi binafsi ya mkulima mdogo mdogo"

Kufuatia ukuaji wa teknolojia nnchini na duniani! Mkulima sasa amehama katika ile zama ya kutwanga mpunga katika kinu asili na kuenda katika mashine.

Ni hatua kubwa na nafuu na muokozi wa muda kwa mkulima na mlaji. Lakini nyuma ya shangwe na furaha hii ya kurahisishiwa kazi, limeibuka kundi la wafanya biashara(wamiliki wa mashine) wasio waaminifu wanaotumia mwanya huu kuwaibia wakulima.

Wizi unafanyikaje

Wizi katika mashine za kukoboa mpunga hufanyika hatua kwa hatua:

A-Wizi wakati wa kuanikwa na kupakia mpunga katika magunia baada ya kuanikwa.
Hapa kuna kamsemo maarufu mashineni ka "kutikisa gunia". Ujazwaji wa magunia kwa mtindo wa kutikisa, hupeleka maumivu kwa mkulima. Gunia la debe sita likitiliswa barabara linaweza kumeza debe 7/8! Mkulima shtuka.

B- Wizi muda wa kukoboa mpunga.
Hapa napo mkulima asipokua makini, huibiwa mpunga na yeye akiwa pale pale karibu na kinu cha mashine!
Mwizi/ mkoboaji asie mwanifu ama hufungulia chekeche/ chujio za mashine na kuruhusu mpunga mwingi kumwaga nnje kupitia pumba ngumu nnje ya mashine.

Pumba hizi kupitia "ubia" wa wapepetaji( ambao nao si waaminifu) hupepetwa na kukusanya mpunga woote nyuma ya mashine katika stoo za pumba.

Wizi wa mchele
Mchele huibiwa kupitia mkoboaji asie mwanifu kwa kuruhusu mchele kupitia katika chekeche za pumba laini na hivyo kupeleka hasara kwa mkulima.Mchele/chenga hizo huuzwa kwa wapishi wa vitumbua na wateja wa kawaida wanaopendelea bei rahisi.

C-Wizi muda wa kupima mchele
Mkulima mjanja mjanja yeye huibiwa kupitia upimaji usio sahihi; mizani iliyochezewa na wafanyabiashara ndio nyenzo kuu ya kukamilisha wizi huo.

Mapendekezo

1) Mamlaka husika, piteni na mfanye kaguzi shtukizi huko mashineni kuwabaini watu hawa.

2) Mkulima kabla huja koboresha, fanya ki utafiti binafsi, tembelea eneo la mashine za ukoboaji na jitahidi kupeleleza. Hapa unaweza kupata taarifa kwa kujenga ka urafiki ka "kinafiki" kwa madarali na wapepetaji - wafanyie ka udadisi wakupe ABC za ni mashine zipi zina ka mchezo ka wizi,(Kuwa makini usishtukiwe).

3) Mkulima, kuwa macho na saa zingine kuwa "mkali" haswa kwenye mali yako. Nendeni mashine watu zaidi ya wawili watatu, ili iwe rahisi kwenu kujigawa muda wa kusamia zoezi la ukoboaji wa mpunga.

4) Mkulima apewe makisio ya kwa debe/gunia ni kiasi cha kilo ngapi makadirio ya juu& chini ya mchele tarajiwa baada ya ukoboaji.

Mkulima kagua mzani jiridhishe una "balance" kabla hawajaweka mzigo wako kuanza upimaji. Hakikisha mzani haujaegamia upande mmoja( kuwa jasusi).

Ni muda sahihi sasa wakulima kulindiwa maslahi yao kwa gharama zote. Kilimo si lelemama, wakulima walindwe.

NB: Andiko hilo limeandikwa chini ya uzoefu na shuhuda katika mashine za mpunga zilizopo Shinyanga.
 
Hii ni mada ya kukufumbua macho mkulima.

Dhima kuu ya mada hii "Kulinda maslahi binafsi ya mkulima mdogo mdogo"

Kufuatia ukuaji wa teknolojia nnchini na duniani! Mkulima sasa amehama katika ile zama ya kutwanga mpunga katika kinu asili na kuenda katika mashine.

Ni hatua kubwa na nafuu na muokozi wa muda kwa mkulima na mlaji. Lakini nyuma ya shangwe na furaha hii ya kurahisishiwa kazi, limeibuka kundi la wafanya biashara(wamiliki wa mashine) wasio waaminifu wanaotumia mwanya huu kuwaibia wakulima.
Wizi unafanyikaje

Wizi katika mashine za kukoboa mpunga hufanyika hatua kwa hatua:
A-Wizi wakati wa kuanikwa na kupakia mpunga katika magunia baada ya kuanikwa.
Hapa kuna kamsemo maarufu mashineni ka "kutikisa gunia". Ujazwaji wa magunia kwa mtindo wa kutikisa, hupeleka maumivu kwa mkulima. Gunia la debe sita likitiliswa barabara linaweza kumeza debe 7/8! Mkulima shtuka.
B- Wizi muda wa kukoboa mpunga.
Hapa napo mkulima asipokua makini, huibiwa mpunga na yeye akiwa pale pale karibu na kinu cha mashine!
Mwizi/ mkoboaji asie mwanifu ama hufungulia chekeche/ chujio za mashine na kuruhusu mpunga mwingi kumwaga nnje kupitia pumba ngumu nnje ya mashine.

Pumba hizi kupitia "ubia" wa wapepetaji( ambao nao si waaminifu) hupepetwa na kukusanya mpunga woote nyuma ya mashine katika stoo za pumba.
Wizi wa mchele

Mchele huibiwa kupitia mkoboaji asie mwanifu kwa kuruhusu( mchele kupita) kupitia chekeche za pumba laini na hivyo kupeleka hasara kwa mkulima.
C-Wizi muda wa kupima mchele

Mkulima mjanja mjanja yeye huibia kupitia upimaji usio sahihi; mizani iliyochezewa na wafanyabiashara ndio nyenzo kuu ya kukamiliaha wizi huo.

Mapendekezo
•Mamlaka husika, piteni na mfanye kaguzi shtukizi huko mashineni kuwabaini watu hawa.
•Mkulima, kuwa macho na saa zingine kuwa "mkali" haswa kwenye mali yako. Nendeni mashine watu zaidi ya wawili watatu, ili iwe rahisi kwenu kujigawa muda wa jusamia zoezi la ukoboaji wa mpunga.
•Mkulima apewe makisio ya kwa debe/gunia ni kiasi cha kilo ngapi makadirio ya juu& chini ya mchele tarajiwa baada ya ukoboaji.
Ni muda sahihi sasa wakulima kulindiwa maslahi yake kwa gharama zote. Kilimo si lelemama, wakulima walindwe.
Nb: Andiko hilo limeandikwa chini ya uzoefu na shuhuda katika mashine za mpunga zilizopo Shinyanga.
Njaa mbaya sana.
Reform inatakiwa kila sekta
 
Mzee unataka umiliki Harrier kwa fedha zetu kwa njia ya udanganyifu?
 
Back
Top Bottom