Wizi wa mtandao watikisa, benki 7 nchini zapoteza Sh bilioni 150

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
DAR. Watu wanaotajwa kuwa wezi mtandaoni kutoka ndani na nje ya nchi, wameiba zaidi ya Dola za Marekani milioni 49 sawa na takribani Sh bilioni 150 kupitia mtandao wa benki kubwa saba nchini gazeti la Raia Mwema limeeleza.

Tayari Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, imekamata baadhi ya watuhumiwa wakiwamo raia wa kigeni, baada ya uchunguzi na ufuatiliaji mkubwa unaoendelea na uchunguzi wa gazeti hilo umepata orodha ya benki zikiwemo mbili kubwa nchini na kampuni 17 zilizohusishwa na wizi huo.

Baadhi ya kampuni na wahusika wameanza kubanwa na kurejesha fedha hizo.

Gazeti hilo limesema litataja majina ya taasisi, benki na kampuni husika katika matoleo yajayo, baada ya taratibu za kisheria na kimaadili kukamilika.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inatajwa kuwa kinara wa uchunguzi huo unaohusisha wabobezi katika masuala ya wizi mitandaoni na wenzao wa taasisi zingine za ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo, maofisa waandamizi wa TAKUKURU wameliambia gazeti hilo kuwa suala hilo ni nyeti kwa sasa, na si vema kulizungumzia hadi ukamataji na uokoaji fedha zilizoibwa na uzibaji mianya ya wizi huo vitakapokalimika, ili ujisirudie nchini

Imeelezwa kuwa watuhumiwa wa wizi huo walianza kunazwa mwezi jana na kuhifadhiwa katika vituo vya Polisi Arusha na Dar es Salaam na wanaendelea kuhojiwa na kubanwa, ili kurudisha fedha walizohusishwa nazo, akiwamo mmoja anayetajwa kutoka taasisi kubwa ya fedha nchini.

Wizi huo unaodaiwa pia kuzikumba nchi kadhaa duniani, umeelezwa kuwa mkubwa kuwahi kutokea na kutikisa taasisi za fedha, uligundulika baada ya taasisi ya kimataifa ya VISA, kuwasilisha malalamiko kwa Serikali ya Tanzania, kuhusu kadi za wateja wao kudukuliwa na kuibiwa fedha.

Imeelezwa kuwa wizi huo ulifanyika kuanzia mwaka jana hadi Mei mwaka huu, ikidaiwa pia kuwa benki mbili kubwa nchini ndizo zimeathirika zaidi.

Taarifa zilisema wizi huo ulifanyika kwa kuhusisha mtandao wa wahalifu wa kimataifa kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na kampuni, mashinka yasiyo ya Serikali na baadhi ya wanasheria

Kwa mujibu wa chanzo cha gzeti hilo, watuhumiwa wa wizi huo walitumia mtandao kulipia huduma na malipo ya Serikali, na mdaiwa kulipa wahalifu nusu ya fedha anazopaswa kulipa, na wezi hao hulipa fedha kamili kwa njia ya mtandao.

"Mbinu zilizotumika kwenye wizi huo ni kuiba kadi za kidijitali za benki (visa card/master) za wateja kutoka mataifa ya Asia na Marekani, kwa kuzinakili kihalifu na kwa kushirikiana na kampuni husika, kulipia gharama za huduma na malipo mengine," kilieleza chanzo.

Chanzo hicho kiliongeza: "Wizi huo umefanyika pia kupitia malipo yaliyofanywa kwa mfumo wa GePG kupitia mtandao wa benki hizo.”

Wezi hao walibainika kutumia mashine za utoaji huduma za kifedha (POS) za benki husika katika kufanya miamala hiyo ya kihalifu.

Mtoa taarifa aliongeza, kuwa mtuhumiwa namba moja wa wizi huo raia wa China, alinaswa wiki iliyopita Dar es Salaam na anashikiliwa katika kituo cha Polisi, akiendelea na mahojiano na timu ya wachunguzi.

“Kwa mwonekano, ni kijana mdogo asiyezidi umri wa miaka 25 na baada ya kukamatwa, alikutwa na nyaraka zikionyesha ushiriki wake katika wizi huo, watu alioshirikiana naona kiasi cha miamala kilichopitishwa na benki zilimathirika," alieleza.

Pamoja na kuendelea na uchunguzi, imeelezwa kuwa timu ya wachunguzi imepewa maelekezo na Serikali kuhakikisha fedha zilizoibwa zinarejeshwa kabla ya kufikisha watuhumiwa mahakamani.

Uchunguzi unaelezwa kuwa unaweza kuhusisha baadhi ya watumishi wa benki na taasisi zingine zilizoguswa na wizi huo pamoja na kwamba taasisi hizo zinadai kutoathiriwa na wizi huo.

Maofisa wa benki moja kubwa, wanaeleza kwamba wao ndio waliotoa taarifa za kubaini kawapo dalili za kihalifu kwenye miamala iliyopita, kwa kutumia mashine za utoaji huduma za kifedha (POS).

Hata hivyo, wachunguzi wanasema benki husika zinaathiriwa na kutozwa faini na taasisi za fedha za kimataifa, na wizi kama huo unaweza kuathiri pia hadhi na kuaminika kwa benki husika kimataifa.

Aidha, wizi huo pamoja na kutishia usalama wa fedha za wateja katika taasisi za fedha, unadaiwa pia kutishia kuathiri biashara ya utalii nchini hasa kutokana na Visa na Master Card kutishia kusitisha huduma zake nchini.

Awali, Raia Mwema ilipata ushirikiano kutoka kwa maofisa wa benki mojawapo waliojitenga kuguswa na uchunguzi unaoendelea kabla ya kukumbana na vitisho kutoka benki nyingine ambayo nayo ina mtandao mkubwa nchini.

Chanzo: Raia Mwema
 
Si mnawapetipeti wachina na mapumbu yao mnasema wawekezaji..endeleeni tu watawafurahisha.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Game ya long time hii. Nashukuru nilitoka huko salama. Pesa za wizi huwa hazileti maendeleo kabisa zaidi ya anasa tu
 
Tukihubiri Injili watu waache dhambi, waache wizi, watu wana-comment: "Acha ujinga"
Huo wizi ni matokeo ya kuwa na watenda dhambi wengi katika jamii. Acheni Injili iendelee.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Tukihubiri Injili watu waache dhambi, waache wizi, watu wana-comment: "Acha ujinga"
Huo wizi ni matokeo ya kuwa na watenda dhambi wengi katika jamii. Acheni Injili iendelee.
Huko ndo hakuna kitu kabisa, wezi tupu
 
Ndiyo maana mtu unajiuliza huyu mtu amejenga jumba la bilioni 3 fedha anapata wapi? Kumbe ni MAJIZi tu.
 
Back
Top Bottom