Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta

Kuna namna wanaitegesha haifiki mwisho na kuruhusu kutoa risiti, wale binadamu wa mbinu sana, nami nilidhani nawasingizia ila nimekuja kugundua wameshagundua kuwa kuna namna ule mkonga ukiutegesha bila kuufikisha mwisho basi haita-clear zile digits pale kwenye meter reading na risiti haitoki.
 
Hivi ni Umeandika bila kujua unachoandika na sijui hujui kweli au unafanya makusudi kupotosha ili uchangamshe jukwaa..

Wizi unaosema haupo na hakuna namna yoyote uneweza ukaibiwa Kwa staili hiyo uliyoileta .mkono wa pampu ukirudishwa kwenye mashine wakati wa kutoa unaanza zero mpaka bei uliyoset au utakapoishia

Kuibiwa ni kama ataendelea kupima bila kurudishwa mkono kwenye mashine tena ikiwa mwanzoni hakuset bei wakati anampimia mteja wa kwanza
 
Elfu 5 tu unalialiaaaa. We tip huwa unaacha kweli
Kaka nitumie basi kwenye namba yangu 0621 111 123, nalia kwa sababu jasho nnalotoka kuipata linaniumiza sana, elfu 5 kwangu napata matunda ya kutosha sana kwenda kuwaongezea vitamin wanangu na kujenga heshima kwa mama yoyoooo. Mimi sitoi tip na wala huwa siendi hizo sehemu za kuacha acha tips, ninakula kwa mama ntilie, huko hakuna tip, tunadai hadi mia inayobaki baada ya kunywa kandoro!
 
Kaka au dada, hata mimi nilidhani kuwa macho yangu yananidanganya kama unavyobisha wewe, nakuhakikishia kuwa makini, mpaka naamua kuandika nimefanya utafiti na kujiridhisha, mimi nina uhakika 100% ya nilichoandika, vinginevyo nawe ukitaka kunibishia vema fanya nawe utafiti mdogo kama wangu!
 
Kuna namna wanategesha ule mkonga wa kuwekea mafuta hausukumi ile lock na kwa hivyo risiti haitoki, na hii hutokea sana kwa watu wasiohitaji risiti.
Mkonga huwezi kukaa nafasi yake bila lock kuingia mkuu pia kama inawezekana ndani ya sekunde tano ukichomoa mkonga mafuta hayatatoka mpaka ustart tena

Wizi unaongela ni wa miaka ya zamani kabla pump hazijhamia kwenye digital pump Kwa sasa pump za namna hakuna mahali popote ndani ya Tanzania
 
Ndugu yangu, naomba tutafutane, twende pamoja pale na tukawahoji walioniibia kwa style hiyo watupe uzoefu, najua yaweza kuwa ngumu kupata ushirikiano, ila nakuhakikishia mimi ntawapa hata pesa ya kula waweze kutupitisha kwenye uzoefu huo.
 
Ngoja Kiduku lilo aje atufokee
 
Hii style nimepigwa juzi aysee kile kituo cha Temboni! Ntamrudia yule dogo nimpe makavu live
 
... this makes sense! Hii tafsiri yake kuna mtu hatimizi jukumu lake ipasavyo - Weights and Measures Agency (WMA) wazee wa "flow-meters". Na wamiliki wa vituo wanatakiwa pia kuhakikisha pump zao haziwezi kuchezewa na wahudumu maana michezo hiyo haina faida yoyote kwao (wenye vituo) zaidi ya kuharibu reputation ya biashara zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…