jana mbichii... nimeenda petro station. nikamwambia weka elfu 30, basi akaclear number akaandika 3,000... nikamwangalia tu akachomeka mpira wake mafuta yakaanza kutoka akajifanya bize akazunguka upande wa pili... mashine imeshakata yeye anajifanya bize.... akaenda funga kifunik akatoa risiti akaniletea, nikampa 30,000 akapokea na kuniambia karibu tena... akashangaa siondoki nikamwambia bado mafuta yangu hayajakamilika umeweka ya elf tatu.... bila hata kuangalia akajifanya kujichangamsha eti samahani daaa kumbe nimeandika elfu tatu.... dah... nina mawazo.... akakuta nimekunja uso namwangalia tu.... nikafungua tank akaandika 27,000 akajaza yaliyobaki..... nikaondoka bado anajichekesha mie simjibu kitu. Huu ni wizi kuweni waangalifu.