Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta

NZALA HIYO
 
Nyingine ni kuchomeka mkonga wa pamp kwenye dumu la lita tano kwanza ndipo anakuwekea kwenye gari ukiwa na upungufu wa lita kadhaa! Ukiwa makini ww unapitia na kigaloni chake unasepa nacho! Hawa wahudumu wengine ni wa hovyo sana! Hii ipo sana Soweto Mbeya 'infinity'! Kuna mabinti pale makauzu kweli!
Mie niliona mchezo huo nikapotezea, nikalipa yote tu na kusepa!
Nyingine nilishuhudia ni pale wanamuwekea wa bodaboda kisha bila kuanzisha upya wanakuwekea na ww! Kimsingi ni umakini tu!
 
Daah! Asante kwa somo nikienda kununua mafuta ya taa nitakuwa makini na mita. Maana huwa nakuwaga bize na msambwanda pamoja na kile kifungo cha kwanza kilichoachwa wazi makusudi!
Jaman si tumekubaliana mafuta ya gari
 
Kuona aibu tu haitoshi,ulichukua hatua gani kulipia hayo mafuta uliyozidishiwa?
 
Nilimwona mmoja amelipa 65.000 akawekewa mafuta ya 55K
 
Ndo maana kweny kapikipiki kangu nikiweka ta 15k inajaa karibia full tank lakn juz kat ikawa yapo chin kiaina
 
Mimi nina kakangu watu wanasema ni bahiri sana akienda sheli anaenda na madumu yake ya lita 60 anawekewa wese anaenda kujiwekea mwenyewe kwenye gari lake,ukimuuliza anasema ni mjanja baada ya kuibiwa kwa mda mrefu na wauza mafuta sheli
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa umri huo mkuu hukujua kwamba gauge haipandi ghafla?
 
Hizo Petrol Station za ajabu ajabu huwa sijazagi mafuta labda itokee gari imenizimikia karibu na hizo sheli. Kwa sasa sheli za uhakika ni Oryx na Total zimekaa ki proffessional zaidi ila kwengine ambako napaamini ni Lake Oil!
Unaachaje kuitaja Puma baba lao?
 
Asante sana kwa thread iliyoshiba na yenye maelezo mazuri
 
Wewe nawe unakurupuka. Hili la kweli na kuna namna wanaweka ule mkono. Unabisha nini sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…