Wizi wa wahudumu wa kwenye vituo vya kujaza mafuta

Ni kweli kabisa. Kuna siku nilikwenda sheli nikanunua diseli ya sh. 50,000. Mwanadada mhudumu akaniambia nakuwekea kwanza ya sh. 10,000. kisha nitakuwekea ya 40,000. Nikateremka kwenye gari kuangalia. Mwisho nilikuwa na risiti mbili moja ya sh.10.000 na nyingine ya 40,000. NIlijiuliza kwa nini lakini leo nimepata jibu
 
Mimi kuna siku nimeweka mafuta ya shilingi elf 30 na baada ya kuweka mafuta nikamwambia anipe risiti, basi mhudumi akaanza kujizungusha, nami nakatulia na kusubiri. Baadae akaleta risiti ya elf 23 na chenji elf 7, akasema pump ilikata mafuta mapema. Kwa hiyo nisingedai risiti nilikuwa niibiwe elf 7.
 
Ulivyoandika mwenyewe unajiona una akiiiiili... Kuweka mafuta ukiwa ndani ya gari ni ku risk sana mkuu... Unashauriwa kushuka ndio maana magari ya abiria hayaruhusiwi kuingia gas station likiwa na abiria...
 
Reactions: Cyb
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Sikupatii picha unsvyotumbua hivyo vimacho vyako vya kichina kuangalia misambwanda
Hahahaha, tafadhali rejea uzi unasemaje ewe kikongwe na utuambie kama yaliyozungumzwa yalishakukuta?
 
Swali zuri sana hili maana inashangaza na vipi kuhusu risiti itasomaje?

WaTz kwa kulalamika tu tunaongoza walai.
 
Nilikua na tabia nikifika petrol station nampa hela mhudumu then akiniambia tayari naindoka hata risit sichukui. Siku moja nikampa hela then nikawa nachungulia kupitia kioo cha nyuma nikaona kwenye dispenser ametype hela tofaut na niliyompa (kapunguza 10,000). Nikaacha kamaliza nikamwambia dada ongeza mafuta ya 10,000 kama hela niliyokupa akazuga oooh sikuhesabu vizuri hela zilishikana..... wezi kweli hawa watu.
 
Mmmh yote hayo umeyajuaje?
Mbona hukusema huko juu kua kuna namna wanategesha kwanza wanategeshaje?

Na Tz ifike mahala watu wawe wanajipimia wenyewe mafuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali zuri sana hili maana inashangaza na vipi kuhusu risiti itasomaje?

WaTz kwa kulalamika tu tunaongoza walai.
... Mkuu; limeshajibiwa. Kwamba, kuna namna wanaegesha ile handle haifiki mwisho hivyo alipoishia namba hazifutiki; zinabaki vile vile. Inakuwa kama ame-hold on.
 
Kimwanamke hicho... kina jeuri balaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…